Wakili wa kina Halima Mdee aelezea kwanini Spika hajawaondoa Bungeni Wabunge hao wa Viti Maalum

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Wakili Edson Kilatu anayesimamia suala la Halima Mdee na wabunge wenzake 18 amenukuliwa akisema:

“Baada ya kesi ya wateja wangu Halima Mdee na wenzake kutupwa, tulirudi kufanya marekebisho, alfajiri ya jana (Juni 23, 2022) tukawasilisha nyaraka Mahakamani kwa njia ya mtandao, hivyo Spika asingeweza kutoa maamuzi ya kuwaondoa wateja wetu Bungeni huku kesi ikiwa Mahakamani."



Source: DarMpya
 
Kheri yenu nyie mnaowasilisha nyaraka mtandaoni na zinafika, wenzenu huyeyuka zikifika.
 
2005 - 2010 Mbunge viti maalumu CHADEMA
2010 - 2020 Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA
2020 - 2025 Mbunge wa Spika

Ni mingapi hapo?
Kumbe alianzia viti maalumu?Sikuwa na kumbukumbu na hilo
 
Aliyewaingiza bungeni ndio atakayewatoa. Kama aliweza kumtoa mtu jela usiku na asubuhi akawa mbunge. Hata huyo wakili ni vile njaa inamsumbua, ukiwa mtu wa principles hupaswi kujiingiza kwenye vikesi vya kukuharibia cv.

Mbona jambo lipo clear kuwa wamerekebisha makosa na kuwasilisha hivyo judge atatazama upya!
 

Acheni ujinga. Kwani tayari mahakama hiyi imeshatoa "stay order" kwa hao covid kuendelea kuwa wanachama wa cdm?
Lini nchi itaanza kufuata sheria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…