Wakili wa kina Halima Mdee aelezea kwanini Spika hajawaondoa Bungeni Wabunge hao wa Viti Maalum

Huyu wakili njaa anachelewesha haki tu. Mahakama ilishasema kuwa haya maombi ya akina Mdee ni michosho na dharau kwa mahakama.

That the application is frivolous, vexatious and an abuse of court
process.
 
Wakili muongo.

Kama wakili alijua kuhusu hilo suala kwanini hakumwambia Spika juu ya uamuzi wake ili autangaze bungeni kama alivyofanya mara ya kwanza?

Tarehe 23 alfajiri ilikuwa Alhamisi, kwanini mpaka jana Ijumaa tarehe 24 Spika anaahirisha bunge alikuwa kimya kuhusu hilo suala la wanawake 19?
 
Mahakamani kesi ilishatupwa na mahakama bado kusema rasmi kama imeipokea tena kesi hiyo!! Hizi sarakasi ni aibu sana kwa Taifa letu!!! As it stands they are not CDM members unless the decision is overturned by court of which it has not up to now!
 
Mbona jambo lipo clear kuwa wamerekebisha makosa na kuwasilisha hivyo judge atatazama upya!

Kuna shida kidogo hapa! Jaji anatakiwa kutoa amei mpya kuwa akina Mdee waendelee kukaa mpaka atakapotoa uamuzi mwingine. Kufungua kesi tu hakuwapi haki akina Mdee wala anayeshitakiwa.

Ningependa kusikia wamefungua kesi mpya kwa hati ya dharura na Jaji kaweka zuio jipya!!

Kufunguliwa kwa kesi haiwezi kuwa ni advantage kwa mshitaki. Uamuzi wa mahakama ndio hutoa advantage! Bado tuna safari kubwa sana kwenye swala la haki!!
 
Ikifika 2025, Halima Mdee atakuwa amekaa bungeni kwa miaka 20; inatosha sana. Shida ni hao wenzake ambao ndio safari yao ya siasa inaanza

Kumbuka, kimsingi, yeye ni career politician. Umewahi kuona wapi career politician akistaafu at the age of 47?
 
Mahakamani kesi ilishatupwa na mahakama bado kusema rasmi kama imeipokea tena kesi hiyo!! Hizi sarakasi ni aibu sana kwa Taifa letu!!! As it stands they are not CDM members unless the decision is overturned by court of which it has not up to now!

Tangu lini mahakama imekuwa na jukumu la kuutangazia umma kila inapopokea kesi mpya?
 

Unachoongea ni sahihi kabisa. Hivyo, sidhani kama watakuwa wameacha kuomba stay order nyingine; they’re smart enough to know the importance of that!
 
Nchi yangu Tanzania,waliokula kiapo kulinda katiba ya nchi yetu kwa mujibu wa Sheria, huku wakiwa wameshika Bibilia na Masahafu, ndiyo wanaovunja katiba ya Tanzania.Ewe Mwenyezi Mungu, tusaidie.
 
Aliyewaingiza bungeni ndio atakayewatoa. Kama aliweza kumtoa mtu jela usiku na asubuhi akawa mbunge. Hata huyo wakili ni vile njaa inamsumbua, ukiwa mtu wa principles hupaswi kujiingiza kwenye vikesi vya kukuharibia cv.
Mazezeta ya faru John mnahamgaika sana.
 

Shida sio kufungua kesi. Unafungua kesi kuomba urudishiwe uanachama, halafu Hapo hapo unadai wewe bado ni mwancha wa Chadema. Kama haki ingetendeka akina Halima Mdee wangefungua kesi wakiwa sio wanchama wakisuburi maamuzi ya mahakama kuhusu uanachama wao.
 
Unateseka sana
 
Kumbe alianzia viti maalumu?Sikuwa na kumbukumbu na hilo

Tatizo Viongozi wengi wa Chadema hawana shukrani. Mdee chadema imemjenga na kumtengeneza lakini akaja kuwasiliti dakika za mwisho na kuungana na watesi wake.
 
Mbona jambo lipo clear kuwa wamerekebisha makosa na kuwasilisha hivyo judge atatazama upya!

Please msipotoshe. Wamefungua kesi Mpya sio marekebisho. Marekebisho yangetokea Kama makosa ni yakurekebishwa. Hapo rulling ilishatoka.
 
Sasa kwani chadema hawajawai kukosea pamoja na kuwa na mawakili wengi wanaosemwa ni wenye uwezo?

Kufungua kesi bila kujua unamshtaki nani ni utahira. Hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza sheria hawezi kushindwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…