PendoLyimo
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 969
- 1,055
Wakili wa Kujitegemea, Joseph Mahando, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakikukiuka Katiba wala sheria yoyote kwa kumteua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wake wa Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.Akizungumza kuhusu mjadala ulioibuka kuhusu uhalali wa mchakato huo, Wakili Mahando amesema baada ya kupitia Katiba ya CCM, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Sheria ya Vyama vya Siasa, ameridhika kuwa hakuna sheria iliyokiukwa."Kuna kauli zinadai kuwa mchakato huo ulichukua hatua kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini Katiba hiyo, kupitia Ibara ya 39(1)(c), inaeleza tu kuwa mgombea wa nafasi ya Rais lazima atokane na chama cha siasa. Haielezi namna mgombea huyo anavyopatikana ndani ya chama, bali hilo linaachwa kwa Katiba na kanuni za vyama vya siasa," amesema Mahando.Katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika Januari mwaka huu, chama hicho kilipitisha rasmi jina la Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa Urais wa Tanzania, pamoja na Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kama mgombea mwenza wake. Pia, Dkt. Hussein Ali Mwinyi alipitishwa kutetea nafasi yake ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.