Raia Mwema
JF-Expert Member
- Jun 30, 2008
- 535
- 79
.Je wajua kwamba wakili A.Kitururu anaye mtetea Mporwa mke wa Dr Slaa ni mgombea udiwani wa CCM kata ya ubungo.Je CCM mnataka wananchi wajifunze nini?.
La muhimu kama walioana kisheria je waliachana kisheria ??? Je taratibu za kukimbia na sababu aliziripoti ,kuna hati zinazoonyesha kulikuwa na matatizo kati yake na mumewe ,aliwahi kuyaripoti iliamuliwaje huko alikoripoti ?? Hakuna hata moja kati ya hilo ,mke na aliemchukua mke wote watakuwa wamefanya au wamemfanyia uhuni huyo masikini wa Mungu , ila sasa kama jamaa ameamua kuamka na baada ya kumjua mbaya wake ,kila kitu kitakuwa shwari hapo sheria zitakapochukua mkondo wake ,ninachowaomba msiwe mnamtetea Slaa tu bali muwe mnatoa maauzi yenye kutoa haki kwa wote wawili au watatu ,kisheria ,bila ya upendeleo ,yaani hapa hapa JF tunaweza kujua ni nani mwenye makosa ambae hukumu itabidi itwalishwe juu yake ,hapa hapa JF ,tuache tabia ya CCM kulindana kwa kuwa tu ni mwenzetu na kumnyonga mnyonge asiestahili :mad2:
.Du! ndo mana hakuwa na comfo bwana, inaelekea kalazimishwa na "mampira" hakuwa tayari kabisa!
.Hivi huyu bwana ameporwaje mke wake? Mimi bado hii kitu haijaingia akilini!
Rejea sheria ya ndoa, hii sio kesi ya kisiasa. Na kama Dk Slaa anafanya mchezo badala ya kujibu hoja itamfikisha pabaya na hata kumchafua zaidi. Huwezi kuwa na kesi ya ndoa ya kujibu mahakamani ukamwambia hakimu ni CCM wamenipakazia. Hii inawezekana tu hapa JF lakini sio mahakamani.Another great mistake kwenye anga za sheria hii itachukuliwa ni kesi ya kisiasa zaidi.
.Afadhali umeuliza mkuu maana hata mimi ninavyojua mke wako siyo mali yako ni mwenza wako na ni binadamu aliyevuka umri wa miaka 18 hivyo ana uwezo wa kufanya maamuzi yake. Sasa ukisema kitu kuporwa ni kwamba kinachukuliwa kwa nguvu na kitu kinachoporwa hakina utashi wa kujua kinaporwa. Tukija kwa upande wa binadamu labda mtoto mchanga anaweza kuporwa lakini si mtu mzima mwenye akili zake timamu, unless anatekwa. Tamko kama hizi ni udhalilishaji wa wanawake na pia ni kudanganya umma kwani ni kitu ambacho hakiwezekani.
.kaaaazi kwelikweli, kaporwa mke , ndo kajua sasa au keshapewa mshiko? si hasa za bongo bwana. nshachoka, natamani utawala wa kidikteta japo miezi sita watu wachapwe viboko ndo tutanyooka
.Inavyoelekea Josephine hamtaki tena huyo jamaa.
Kama hamtaki alipaswa kufuata sheria
lalalalal! Ipendeni CCM kiroho lakini msiruhusu tabia za akina JK (kupita na waandishi wa habari, wasanii wa kike kisha kuwazawadia ukuu wa wilaya na ajira BOT) kutawala akili zenu, lazima kuwe na mipaka!Fanyeni kila mnaloweza ,najua mnaweka dharau sana na kutudharau wengine kuwa hatujui kitu na nyie waChadema ndio mnaojua na kujifanya ni watu wa mahakama ,ila mkae na kukumbuka msije mkalaumu kuwa hamkupewa tahadhari ,wakati hakimu atakapogonga meza ,Mkuu hapa amenasa na zaidi kesi hii ya uzinzi kwa kiongozi mkuu wa Chama na pia mgombea uraisi. Sijui niseme huku ni kuchamba kwingi kwa Slaa au ni kuhadaika na giza akanya njiani ?
Hivi Slaa alipomnadi yule mwanamke alikuwa anauonyesha nini umma wa WaTanzania ,kama CCM inaatufanya WaTz wajinga ,Slaa anatufanya mambutwai au , ipendeni Chadema kiroho lakini msiziruhusu tabia za akina Slaa kuwatawala akili zenu ,lazima kuwe na mipaka.
.
Je wajua kwamba wakili Mabere Marando aliyetetea chadema kesi ya pingamizi dhidi ya kikwete ni kada wa chadema. Je chadema mnataka wananchi wajifunze nini?
Kwa mujibu wa sheria, Rose Kamili ni mke wa ndoa wa Dk. Slaa, ni busara zake tu yule mama hajafungua mashitaka. Dk. Slaa anasema hakufunga ndoa na yule mama lakini sheria inasema watu wa jinsia tofauti (mwanamke na mwanaume) wakiishi pamoja kama mke na mume kwa miezi 6 automatically sheria ya ndoa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawatambua watu hao kuwa ni mume na mke. Kitendo cha Dk Slaa kusema hakufunga ndoa na Rose Kamili ni habari za mtaani na sio za kisheria. Nina mashaka hapo baadaye Kamili anaweza kufungua kesi dhidi ya Josephine na Dk. Slaa. Kamili anaonekana amesita kufungua mashitaka dhidi ya Dk Slaa kwa sababu za kisiasa, akipita ubunge Hanang hatafungua mashitaka na akishindwa anaweza kufungua kwani kwa sasa anaweza kuwa anacheza kete ya kisiasa kwa kutompinga mgombea wa urais wa chama chake cha chadema.
siyo wote humu ni maamuma wa sheria mkuu..
Kwa mujibu wa sheria, Ndoa iliyounganishwa kisheria ni lazima ivunjike kisheria. Kama Dk. Slaa alianzisha mahusiano ya kimapenzi na mwanamke ambaye ndoa yake haijavunjika kisheria ana kesi ya kujibu mbele ya mahakama. Jamani tuache ushabiki ambao hautaki kuzingatia sheria inasemaje? wote tunampenda Slaa lakini ili kumsaidia ni lazima tuseme ukweli.
Si ndio nyinyi Wakristo munaosema ndoa hazivunjwi? Leo tena mambo yamekuwa vipi? Au mkuki kwa nguruwe lakini kwa binaadamu huwa mchungu?
Mimi nauliza tu jamani!!!!!!!!!!!!!