Wakili wa Tigo adai kwao Compliance (Utii) kwa mamlaka ni kipaumbele kuliko Privacy (faragha) za Wateja

Wakili wa Tigo adai kwao Compliance (Utii) kwa mamlaka ni kipaumbele kuliko Privacy (faragha) za Wateja

ingekuwa nchi za maana hao jamaa sasa hivi soko la hisa wangekuwa wanapumulia mashine
 
Kwa maana hiyo chadema walitaka hata mtu mwovu akitumia mtandao ALINDWE TU NA UOVU kwa kuwa sheria ya usiri na faragha inamlinda.
#Hata ulaya hakuna kitu ya namna hii.
Ficha basi ujinga wako, Sasa hivi Dunia inapambana na haki ya ulinzi wa Siri za mteja kwenye ulimwengu wa tekinaolojia ya habari na mawasiliano ndio maana watu kama Edward Snowden dunia inawaangalia kama mashujaa sio wahalifu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
kama wewe sio Gaidi unaogopa nini?
magaidi ndio watakao ogopa maana wana tumia vibaya mawasiliano.
 
Wew mburula Kingai huna ujualo kaa utulie Kibwetele. Huyo wakili kihiyo wa tigo amekiri Mahakamani kuwa hakuna barua aliyopewa na polisi inayo omba afanye uchunguzi kwa kosa fulani. Na hata yeye barua aliyo ijibu pia haioneshi kuwa amechunguza na kubaini makosa hayo.
Ndio maana wanamuuliza kwa nini unatoa taarifa za wateja pasipo na sababu za kisheria.
Jamaa kakutana na wajuvi wa sheria sasa kajivua nguo
 
Hii kesi inaenda kufichua mengi.

Alafu pia inaonekana watanzania tunadharaulika sana, huyo jamaa ameropoka hivyo akijua wateja wao hawawezi kuchukua maamuzi yoyote ya kuitikisa kampuni.

Watanzania wengi wanaweka ushabiki kwenye kila jambo.
Sasa wapinzani wakiamua kujitoa huko si ndiyo watabaki kama ttcl?
 
Sasa wewe, iwapo mtu na genge lake wanataka kupindua nchi, raia mwema akatoa siri na achilia mbali kampuni zikagundua kuna mpango wa kufanya vitendo viovu. Ina maana hiyo kampuni ya mawasiliano ikae kimya kisa eti wana linda siri za mteja?? kweli nyumbu mumechanganyikiwa. Mr DJ ni gaidi
Gaidi ni Hamza mwana ccm
 
Kwa maana hiyo chadema walitaka hata mtu mwovu akitumia mtandao ALINDWE TU NA UOVU kwa kuwa sheria ya usiri na faragha inamlinda.
#Hata ulaya hakuna kitu ya namna hii.
Aliulizwa Kama alijua kuwa aliyeletewa namba achunguze Kama ni mwalifu kadai yeye hakujua Kama anamchunguza mhalifu.
 
This is why tunahitaji katiba mpya. Katiba ambayo itamlinda mwananchi kulinda privacy yake, muda wa mtu kukaa remand na kesi kusikilizwa
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Hebu tujiulize kidogo halafu tuendelee kubishana mpaka kesho....

Zipi ni requirements za serikali haya makampuni yanapoomba leseni kwa serikali..?
Tunaponunua laini kuna fomu ya makubaliano kati yetu na tigo kwa tigo kulinda haki zetu tunajaza na kusign?

JF tukijiunga huwa kuna requirement za JF tunapewa then tuna click agree ~ TUNAZISOMA HIZI REQUIREMENTS.. au tuna agree tu..
 
Tuyaone kwanza masharti ya leseni ya kufungua kampuni ya simu Tanzania halafu ndio tuanze kurusha mawe, isije ikawa tunarisha mawe kwa asiyehusika..
 
Back
Top Bottom