Wakili wa Tigo adai kwao Compliance (Utii) kwa mamlaka ni kipaumbele kuliko Privacy (faragha) za Wateja

Wakili wa Tigo adai kwao Compliance (Utii) kwa mamlaka ni kipaumbele kuliko Privacy (faragha) za Wateja

Wakati nchi nyingi makampuni ya mawasiliano yakiwa yanaweka kipaumbele sana kwenye usiri wa taarifa za wateja wao, hapa kwetu hali ni tofauti kabisa.

Hilo limethibitishwa leo na Wakili Msomi Fred Kapara, ambaye ni Wakili wa Kampuni ya Tigo, alipoulizwa Mahakamani wakati akitoa ushahidi katika kesi inayomuhusu Mwenyekiti wa CHADEMA na wenzake wanne, kwamba kati ya Utii kwa mamlaka na Usiri wa taarifa za wateja kipaumbele kwao ni nini, bila kupepesa macho akajibu Utii (Compliance) kwao ndiyo kipaumbele (Priority) zaidi.

Sasa majibu ya kwanini kumekuwepo na uzimaji wa baadhi ya mitandao ya kijamii na kupanda mara dufu kwa gharama za bando za data yameshapatikana. Sababu kubwa ni kwamba huko kwenye hizo social networks zingine kwao Privacy za Wateja ndiyo Priority hivyo mamlaka zitashindwa kupata kile wanakitaka kwa urahisi.

Hii kesi mpaka waje wamalizike mashahidi wote 24 tutakuwa tumeshapata siri nyingi sana ambazo raia wa kawaida tulikuwa tunafichwa.

View attachment 1995845
Duh! Hatuko safe kabisa kumbe nchi hii. Inawezekana hata HAPA JF pia ndio hivyo hivyo.
 
Yani inamaana pamoja na kujinasibu kama watu wanaozijua Sheria, hawakuwa wanajua kama mamalaka zimepewa uwezo huo pale inapolazimu? Na kwa hii kesi ilikuwa ni lazima kuexpose ushahisi wowote unaoweza kurahisha kesi, maana kama ushahidi mzuri wa kuthibitisha makosa ulikuwa unapatikana huko, huwezi kuuacha kwa kigezo cha privacy.

Ningeona wamefaya makosa kama wangefatilia taarifa za siri ambazo hazihusiani kabisa na makosa anayokabiliwa nayo mtuhumiwa, kosa ni kosa tu liwe ni la kifichoni au la wazi.

Nadhani ni kwakua inang'ata kwao ndomaana hawakutaka taarifa za uovu wa jamaa yao zivujishwe.Angekuwa ni Sabaya hapo, ungeona hoja tofauti kabisa kwenye mitandao.
Kwako Wewe kutuma laki 5, kupitia Tigo, ni uovu?! Ameulizwa kuna kosa limeahinishwa kwenye barua ya kuomba hizo taarifa, akasema hakuna! Jiulize alitoaje taarifa za mteja ‘kibwege’ hivyo, kisa ni polisi wanataka?! Au siku wakiku-huck Wewe ndo utapata akili?!
 
Umempendelea sana huyo ngedere kwa kumuita Wakili Msomi! Anaulizwa maswali mengine anajikanyaga kanyaga tu! Halafu eti ni Mwanasheria wa kampuni kubwa kama tigo!
Unaweza ukakuta ndo kapachikwa pale na system hata kama position yake siyo kubwa.

Ila nimeshangaa kuona anauwezo mkubwa (powers) kupokea barua yeye na akaishughulikia yeye mwenyewe bila vetting wala approval yoyote ndani ya kitengo cha sheria bila hata kuwashirikisha watu wa Security/IT na wakubwa zake kazini!

Swali langu: Leo kabadilisha jina. Je, kwenye barua ya awali kuna majina gani??
 
Duh! Hatuko safe kabisa kumbe nchi hii. Inawezekana hata HAPA JF pia ndio hivyo hivyo.
Jamii Forums tuko safe sana! Na shukrani za kipekee zimwendee huyu Mzalendo wa kweli Maxence Melo!

Angekuwa na akili za kuku kama za huyu Mwanasheria uchwara wa tigo, kitambo angeshawaumiza wengi humu. Na mfano mzuri ni ile kesi aliyo sumbuliwa kwa miaka mingi kwa kukataa kwake kutoa taarifa za mjumbe aliyetakiwa na hiyo mipoliccm!
 
Kwa kwako Wewe kutuma laki 5, kupitia Tigo, ni uovu?! Ameulizwa kuna kosa limeahinishwa kwenye barua ya kuomba hizo taarifa, akasema hakuna! Jiulize alitoaje taarifa za mteja ‘kibwege’ hivyo, kisa ni polisi wanataka?! Au siku wakiku-huck Wewe ndo utapata akili?!
Mnatabia ya kuchambua kamstri kamoja na kukasimamia ili kutafuta uchochoro wa kutokea, bila kusimamia hoja yote niliyoandika.

Kwahiyo hapo umeona wapi nimeandika kutuma 500K ni kosa???

Kutuma 500K sio kosa,swala ni unatuma laki tano ili kifanikisha shughuli gani?? Kama kwenye kesi imesemekana kuwa kuna kiasi kilichotumwa kwaajili ya kitu fulani, kuna ubaya gani mahakama ikithibitusha ili kujua kama ni kweli Mbowe anasingiziwa?
 
Fake id
Inazuia utambulisho wako kwa member wenzio ila info zipo
Kwani wewe ulijiungaje Jf?
Jf wakiulizwa kuhusu mimi wanaweza kutetea kwakua, hata kama niliweka info zangu bado ni ngumu kwa mtu aliye nje ya mfumo wa Jf kutambua kuwa zile info ni zangu.Kwamfano, hata kama Mbowe au SHH ni ngumu sana kujua moja kwa moja kuwa SSH anatumia I'd fulani kwahiyo unajua ngumu kumpoint mtu directly.

Huko kwenye huduma za simu, mimi nikihakikisha tu kuwa wewe unatumia line ya tigo hakuna namna ambayo Tigo wanaweza kukataa kuwa hawakutambui. Unless otherwise uwe umesajili kwa kitambulisho cha mtu , kitu ambacho kitaamsha kesi nyingine.
 
Kwani Chadema ingekuwa nyie ndo wamiliki wa Tigo TZ alaf serikali ikaja inamtuhumu mtu mngegoma kutoa ushirikiano?
Kumbukeni tu jinai ni mambo yanaweza kuhatarisha usalama wa nchi na hiyo serikali inayoomba hizo data ndiyo imekupa leseni.

Chadema mngegoma kutooa hizo taarifa ingekuwa nyie ndo Tigo TZ?
Barua haikuandikwa kosa,alipokea yeye,aka print majibu yeye,akaenda mahakamani yeye kutoa ushahidi.Jambo la pili la kuangalia ni kuwa alielezwa ya kuwa makao makuu ya Tigo yapo jirani na ofisi za usalama wa Taifa na akakubali!!!Umeelewa lakini.....
 
Majibu haya hayana afya sana kwa kampuni husika. Ingekuwa huko Dunia ya kwanza hii kampuni ingepoteza wateja sana
Kuna alot of people huko nje ambao hawajui hata kama Mbowe ana kesi, seuze hili sakata la Tigo?

Hapo ndo ugumu unapo anzia.
 
Mnatabia ya kuchambua kamstri kamoja na kukasimamia ili kutafuta uchochoro wa kutokea, bila kusimamia hoja yote niliyoandika.

Kwahiyo hapo umeona wapi nimeandika kutuma 500K ni kosa???

Kutuma 500K sio kosa,swala ni unatuma laki tano ili kifanikisha shughuli gani?? Kama kwenye kesi imesemekana kuwa kuna kiasi kilichotumwa kwaajili ya kitu fulani, kuna ubaya gani mahakama ikithibitusha ili kujua kama ni kweli Mbowe anasingiziwa?
Siyo Wewe tu, shahidi wa leo amekuja kuiambia mahakama kwamba Mbowe alituma laki 5! Mnang’ng’ania ni za ugaidi, kwa kigezo gani? Huyu shahidi yenu amehusishaje hiyo laki 5 na ugaidi?
 
Kwa maana hiyo chadema walitaka hata mtu mwovu akitumia mtandao ALINDWE TU NA UOVU kwa kuwa sheria ya usiri na faragha inamlinda.
#Hata ulaya hakuna kitu ya namna hii.
Nae huyo ni mwanasheria! Lazima nimshangae; aliamua kutumiwa na tanpol au mwajiri wake??
Kwasababu anaumbua pande zote mbili.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Siyo Wewe tu, shahidi wa leo amekuja kuiambia mahakama kwamba Mbowe alituma laki 5! Mnang’ng’ania ni za ugaidi, kwa kigezo gani? Huyu shahidi yenu amehusishaje hiyo laki 5 na ugaidi?
Nafikiri sio kazi yangu kuthibitisha hilo, wewe kama unataarifa zaidi kuhusu hilo unaweza kuweka hapa ili kila mtu asome.
 
Nchi nyingine Wana sheria Kali za data protection na lazima kuingia makubaliano kati ya pande mbili, ila bongo swala la data protection inabidi liende bungeni maana watu wanaingilia privacy za watu kimasihara sihara tu na hamna Cha kuwabana
Watunga sheria wetu hawaoni shida hii ndani ya jamii, mpaka siku speaker mahojiano yake na kimada chake yavuje ndio wataona tatizo linalohitaji sheria mahususi.

Na wengine ni wana sheria sio wajasiriamali kabisa, makampuni yote ya simu ukitoa TTCL ni subsidiary ya makampuni makubwa, yenye operation nchi tofauti na yanajua umuhimu wa data protection.

So technically ata kama kungekua hakuna sheria kabisa you can bring a claim against any of them using ‘customery laws’ za industry norms duniani na jinsi hayo makampuni yanavyoendeshwa nchi zingine.

Mbona Msando aliwabadili tabia kampuni simu kwa kutumia hati miliki za wasanii kabla ya kuwa na sheria by using industry norms, tatizo nalo lawyers wengi sio wajasiriamali.

Tanzania hakuna sheria inayosema usitoe siri za mgonjwa (maana ili pia ni swala la data protection), but medical ethics ‘industry norms’ ndio inayotumika kwa sasa na inaheshimiwa kwa kiasi kikubwa.

Kwanini management za kwenye makampuni ya mawasiliano wasifanye ivyo kwenye kulinda info za wateja for ethical reasons as industry norms.

Hawa watu wamezidi ili swala kwaweli sio la kufumbia macho, inaanza kuonekana ni kawaida kuingilia mawasiliano ya watu na serikali kama aioni vile ili tatizo.
 
Kwa maana hiyo chadema walitaka hata mtu mwovu akitumia mtandao ALINDWE TU NA UOVU kwa kuwa sheria ya usiri na faragha inamlinda.
#Hata ulaya hakuna kitu ya namna hii.
Hao Chadema ni wapumbavu tu. Mbona kwenye kesi wa Ole Sabaya walikuwa wanasherehekea Voda walipokuwa sana "comply"? Sasa imekuja kwa Mbowe wanajifanya kushangaa? Wapumbavu kweri kweri.
 
Back
Top Bottom