Wakili wa Tigo adai kwao Compliance (Utii) kwa mamlaka ni kipaumbele kuliko Privacy (faragha) za Wateja

Kampuni ya tigo imejitia doa sana ambapo itawachukua muda mrefu sana kurudisha imani kwa wateja zao ambayo wameipoteza
 
Hapo ndipo wanapotukosea inaamaana utii ni zaidi kuliko privacy ya mtu?
 
Kuna taratibu zake mkuu, hakuna anayekataa kwamba sheria zinawaruhusu kutoa taarifa za wateja.

Kwanza kabla hawajatoa taarifa za mteja ni lazima wajue zinaenda kutumika kwa sababu ipi.

Pili lazima kuwe na court order.

Tatu lazima mteja afahamishwe, ili kuconfirm kama kweli kuna kitu cha namna hiyo.

Police hawezi kuomba taarifa za mteja kisha ww lawyer ukatoa kisa tuu ni police.
 

Hapo Tigo hawawezi kufunguliwa kesi na kudaiwa mabilioni ya shillingi kwa kutofuata taratibu za utoaji taarifa za mteja?..
Kupitia hiyo kesi pia wateja wengine kwa kukusanya sign hata 10000 kuishitaki Tigo kwa kushindwa kulinda taarifa za wateja....ref ikawa kesi hii na ile ya Abdul Nondo...
 

Japo hakuna sheria maalum ya ‘Data Protection’ (ukiniuliza mimi hii ilitakiwa kuwa imetungwa muda mrefu) lakini kuna sheria nyingine kadhaa zinazolinda faragha enough to sue ‘phone companies’.

Unashangaa mtu kama Haji Manara kulalamika hadharani namna mawasiliano yake yalivyonyakuliwa; serikali kimya (wizara ya mawasiliano na Technology) na yeye mwenyewe pamoja na ujanja wake kushindwa kuishitaki kampuni husika.

Ni hivi kila kampuni inabeba lawama za matendo ya wafanyakazi wake (vicarious liability). Isitoshe kumfungilia kesi mfanyakazi akulipe billion kadhaa hiyo hela hana so it’s waste of time, lakini TiGo wanazo hizo hela.

Kwa kanuni za ‘tort law’ ni jukumu la kampuni kulinda wateja sio mwajiriwa that include info za wateja na usalama wao.

Ningekuwa mwanasheria nchi hii ningekua tajiri sana, habari kama hizi nakusanya wahanga 20 hivi no legal fees, twendeni dai tsh billion 5 tukishinda 40% yangu.

Sijui kuna ajali chanzo dereva au basi lenyewe lilikuwa mkweche natafuta familia za abiria twendeni kudai fidia. Yaani sina muda kabisa na kesi za wanasiasa zenye malipo uchwara.

Hila kunaitajika ‘data protection legislation’ imefikia hatua hawa watoto awaogopi kabisa mtu anatangaza biashara ya ku hack mawasiliano kama vile ni kitu normal instagram.
 
Kwa hiyo mlitaka Migaidi na Mijambazi ijifiche kwenye hii mitandao ya simu kwa kisingizio cha USIRI kwa wateja?
 
Kwa hiyo mlitaka Migaidi na Mijambazi ijifiche kwenye hii mitandao ya simu kwa kisingizio cha USIRI kwa wateja?
Kuna taratibu za kisheria zinazoruhusu vyombo vya usalama kupata info kwenye investigation zao nchi zote duniani. Na wakitaka hizo info inabidi wapitie kwa uongozi wa kampuni.

For security reasons hivi polisi aende kuomba info za mtu kwa mfanyakazi wa kawaida si anafichua upelelezi wenyewe, unajuaje jamaa ata mtonya muhisika.

Makampuni ya Tanzania kila sakapoko kwenye IT department anatoa info za wateja kwa urahisi sana, hili jambo alikubaliki, including mods wa JF.
 
Maxence Melo alisimama imara pamoja na kulazwa lupango kwa wiki kadhaa kutetea haki ya wanachama wa JF.

alijitetea kwamba hawajui,sababu mnavaa chupi zisizo zenu.

tigo wakufiche na umefanya uduanzi!!!my brother kachunguze kwanini ulisajiri line kwa taarifa za nida,haikuwa ili tuwe tunasoma jina lako ukitaka kutumiwa hela.
 
Kwa maana hiyo chadema walitaka hata mtu mwovu akitumia mtandao ALINDWE TU NA UOVU kwa kuwa sheria ya usiri na faragha inamlinda.
#Hata ulaya hakuna kitu ya namna hii.
Unaropokawewe, unaongolea Ulaya ipi?
 
Kwa maana hiyo chadema walitaka hata mtu mwovu akitumia mtandao ALINDWE TU NA UOVU kwa kuwa sheria ya usiri na faragha inamlinda.
#Hata ulaya hakuna kitu ya namna hii.
Hapana ndugu Crocodiletooth, unawahi mno kutoa conclusion ili ukidhi kiu ya utakacho wewe...

Hoja hapa siyo kumlinda au kutomlinda mhalifu kwa sababu mpaka hapa tulipo sasa hakuna aliyekwisha kuthibitishwa na mahakama kuwa ni mhalifu...

Msisitizo hapa ni kuwa, hata kama mamlaka za kudhibiti uhalifu zina hisi mtu fulani anatumia mitandao kwa nia ya kufanya uhalifu, basi utaratibu wa kisheria ufuatwe ili kupata taarifa za mtu huyo...!

Hili ndilo tatizo la ushahidi wa Freddy Kapala..!

Kwa kifupi, polisi wamemtumia "mhalifu au hacker" Freddy kujipatia taarifa za mteja wa Tigo TZ ili zitumike kama ushahidi wa kisheria mahakamani...!!

Sasa fikiri mwenyewe matokeo yake yatakuwaje..
 
Kwani Chadema ingekuwa nyie ndo wamiliki wa Tigo TZ alaf serikali ikaja inamtuhumu mtu mngegoma kutoa ushirikiano?
Kumbukeni tu jinai ni mambo yanaweza kuhatarisha usalama wa nchi na hiyo serikali inayoomba hizo data ndiyo imekupa leseni.

Chadema mngegoma kutooa hizo taarifa ingekuwa nyie ndo Tigo TZ?
 
Kwa maana hiyo chadema walitaka hata mtu mwovu akitumia mtandao ALINDWE TU NA UOVU kwa kuwa sheria ya usiri na faragha inamlinda.
#Hata ulaya hakuna kitu ya namna hii.
Sialiulizwa Kama iyo no inakosa au ameona hatia yyte kwa uyo mteja akasema hamna, hat y hajui Ni kwa nn anatoa ushahid kwa no ambayo yy hajaona kosa
 
Nchi nyingine Wana sheria Kali za data protection na lazima kuingia makubaliano kati ya pande mbili, ila bongo swala la data protection inabidi liende bungeni maana watu wanaingilia privacy za watu kimasihara sihara tu na hamna Cha kuwabana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…