Wakili Wasonga: Tuwe na private investigation, Sio kila mtu tu ameiba kuku ni mhaini

Wakili Wasonga: Tuwe na private investigation, Sio kila mtu tu ameiba kuku ni mhaini

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Wakili Godfrey Wasonga, amependekeza Serikali kuangalia upya mfumo wa upelelezi na uendeshaji wa kesi za ugaidi na uhaini, akisema makosa hayo ni makubwa na yanahitaji viashiria vya kutosha kabla mtu hajafikishwa mahakamani.

Akizungumza na Jambo TV, Wasonga amesema Serikali inapaswa kuweka sheria itakayoruhusu private investigation, ili uchunguzi usibaki mikononi mwa Serikali pekee, bali kuwe na nafasi ya uchunguzi huru ambao unaweza kusaidia Mahakama kupima ushahidi wa pande zote.

Pia amependekeza kuwepo kwa mwongozo wa Jaji Mkuu kuhusu kesi za ugaidi na uhaini, ukiweka viashiria vinavyopaswa kuonekana kabla mtu hajafunguliwa mashtaka hayo.

“Sio kila mtu tu ameiba kuku, mhaini. Amefanyaje uhaini? Haitakiwi kwenda hivyo.”

Wasonga amesema mifumo hiyo inapaswa kuangaliwa upya ili iendane na mabadiliko ya teknolojia na mfumo wa maisha, akisisitiza umuhimu wa kuweka utaratibu unaohakikisha mashtaka ya ugaidi au uhaini yanafunguliwa pale ambapo viashiria na ushahidi wa awali vinajitosheleza.



​
 
Serikali inayoKANDAMIZA raia wake haiwez kuruhusu kuwa na mwendesha mashtaka binafsi..katiba mpya LAZIMA itoe ridhaa kuwepo private prosecutor..!
 
Back
Top Bottom