Wakili wa kujitegemea jijini Mwanza, Willbard Kilenzi ameishauri serikali kuwasaka na kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya watendaji wa umma wanaovujisha nyaraka za serikali kwa watu walio nje ya mfumo wa utumishi serikali, jambo linalosababisha nyaraka hizo kupotoshwa na kuleta taharuki kwa jamii
Kilenzi ametoa kauli hiyo leo jijini Mwanza wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii yanayoendelea nchini huku pia akiitaka serikali kuongeza ukali kwa kuchukua hatua kwa watendaji wanaokwamisha miradi ikiwemo usimamizi mbovu na kupelekea miradi hiyo kushindwa kuleta tija kwa jamii
"Baadhi ya watendaji wanajiingiza katika kutoa nyaraka za Serikali kwa watu wa nje ya serikali, na watu wenye nia mbaya wakizipata wanazihariri na kuzisambaza zinaleta taharuki. Hapa niombe Serikali watumishi wachache wa namna hii wamulikwe na wchukuliwe hatua zinazostahiki kwasababu wanasababisha hali ambayo jamii nzima inapata taharuki," amesema Kilenzi
Sambamba na hilo, Wakili huyo ambaye amewahi kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, amewashauri wananchi kutochukua Sheria mkononi ikiwemo kufanya maandamano, badala yake wawe wamoja na kutafuta suluhu ya changamoto za kijamii katika njia ya amani