Wakimbizi wa Kiafrika wapigwa mpaka kifo huko nchini Hispania

Wakimbizi wa Kiafrika wapigwa mpaka kifo huko nchini Hispania

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
Wahamiaji 37 waliuawa na wengine 150 wakijeruhiwa vibaya na vikosi vya polisi katika mpaka wa Morocco na Hispania.

Kulingana na shirika la kutetea haki za wakimbizi UNHCR linaeleza kuwa wakimbizi hao wengi wao wakitokea katika nchi za Chad, Niger, Sudan kusini wangetakiwa kuchukuliwa kama watafuta hifadhi kulingana na sheria za kimataifa.

Kinachoendelea huko kinaumiza sana na mbaya zaidi dunia inaonekana kutokujali, wala vyombo vyote vya habari havioni uvunjifu huu wa haki za binadamu. It's shameful kwa kweli.
#PrayforUKRAIN ndicho dunia inakijua.

======

Hapa tunaweza kutambua ni namna gani waafrika wanachukuliwa wakiwa wakimbizi huko ulaya kulinganishwa na wakimbizi kutokea UKRAIN.

20220629_174630.jpg
20220629_174634.jpg

Picha zikionyesha rundo la maiti na walio mahutuki chini ya ulizi wa askari wa Hispania

Video ikionyesha kipigo kilichotembezwa kabla.
 
wengi ni wafuasi wa Mudy. Kutwa kucha kuwatukana wazungu, cha ajabu kila siku wanadakwa wakikimbilia kwa haohao wazungu 😁😁😁😁 kwani Saudi Arabia pamejaa?😁😁
Wewe na hao mna tofauti gani? na nini kinakufanya uamini wewe ukienda hapo hautafanyiwa walichofanyiwa hao?

Na wao kuwa waislamu kunawaondolea vipi uafrika wao?

Na nani amekwambia waislamu wana uhusiano wowote na waarabu?
Uislamu ni dini tu au unataka kusema wewe mkristo una uhusiano wowote na wazungu?

Kwamba kwakua wewe ni mkristo basi kiasili kwenu ni Europe na ukienda hawatokubagua sababu wewe ni mkristo haijalishi kama ni mwafrika mweusi?

Hakuna mtu anayejali dini yako na ukilinganisha huko nje mostly ni atheists au ni dini kama jina tu, ila watakubagua sababu wewe ni mweusi, au unaona wale black americans wanaokuwa oppressed na kubaguliwa kule marekani ni waislamu?

Waafrika wenyewe tunachukiana namna hii unafikiri nani kutoka race nyingine atakupenda na kukuthamini wewe.

Huna akili.
 
Mimi ndio maana nasema ni vizuri kubaki na kupambana Afrika kama kwenda nje ya nchi za watu utaenda vacation tu na kurudi nyumbani. kuliko kupenda rahisi kwenda huko kudharirika na kudhihakiwa namna hiyo.

Hao wamehangaika kujenga kwao na kupafanya bora ila waafrika wanaenda tu kutumia na kula bure matokeo yake ndio hayo. ujinga, uvivu na umasikini vitu kibaya sana.
Waafrika tujenge kwetu na nyumbani ni nyumbani tu.

Mungu awalaze wanapostahili.
 
Sehemu ambayo inakufanya ujihisi salama ni nyumbani, ukiona mtu anakimbia nyumbani kweli hakukaliki. Njaa mbaya sana watu wangekuwa wanakula wanashiba hata wasingekimbia. Serikali za Africa hazina huruma kabisa. .
 
Na ukitaka kujua akili za waafrika ni mbovu angalia hata ndani ya huu uzi.

Hapa kungekuwa ni picha za watu weupe au wanajeshi wa ukraine ungeona "rest in peace" na "walaze mahali pema peponi" kibao.

Cha ajabu ni Waafrika wenzao lakini hauoni chochote. kweli kabisa?

Waafrika wana nini vichwani mwao?
 
Wahamiaji 37 waliuawa na wengine 150 wakijeruhiwa vibaya na vikosi vya polisi katika mpaka wa Morocco na Hispania.

Kulingana na shirika la kutetea haki za wakimbizi UNHCR linaeleza kuwa wakimbizi hao wengi wao wakitokea katika nchi za Chad, Niger, Sudan kusini wangetakiwa kuchukuliwa kama watafuta hifadhi kulingana na sheria za kimataifa.

Kinachoendelea huko kinaumiza sana na mbaya zaidi dunia inaonekana kutokujali, wala vyombo vyote vya habari havioni uvunjifu huu wa haki za binadamu. It's shameful kwa kweli.
#PrayforUKRAIN ndicho dunia inakijua.

======
Hapa tunaweza kutambua ni namna gani waafrika wanachukuliwa wakiwa wakimbizi huko ulaya kulinganishwa na wakimbizi kutokea UKRAIN.
View attachment 2276572View attachment 2276573

View attachment 2276575
na mm nna week ya 3 sasa nimeshanza kuwa nyanyapaa hawa nyangau nmekuwa siwapendi tu naturally na wenyewe wanalijua hilo
 
Walaaniwe waAfrica na viongozi wetu wapumbavu waliodumaza maendeleo na uchumi uchumi mpaka maisha yamekuwa unbearable for many kiasi kwamba wako desperate kukimbilia popote huko kutafuta unafuu WA maisha , hii inatakiwa iwe ni alarm ya kufanya tufikiri na si kuanza kutafuta sympathy Kwa watu , Africans don't owe anything Spain or Europe , let that sink in you big ugly heads.

Viongozi na mifumo mibovu ya uongozi ndio matokeo yake hayo , fuatilia , nchi kidogo zilizofahikiwa kutengeneza mifumo mizuri ya uongozi ndio prosperous atleast Kwa standards zetu za KiAfrica huwezi kuta mhamiaji haramu toka Namibia au Botswana Kati ya hao , kila siku wanakufa kwenye maboti kutafuta Europe ,ni aibu mno
 
Back
Top Bottom