Wakina Dada/ Wanawake ni vitu gani huwa mnaviangalia haraka mnapokutana na Wanamume?

Wakina Dada/ Wanawake ni vitu gani huwa mnaviangalia haraka mnapokutana na Wanamume?

Hakika huyo kaka ndo Mimi huwa sipendi watu wapate shida katika mwendo kasi
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Watu wa daslama walivyo na roho mbaya
Hawapishi hata wazee.
Unakuta kaka anagombea siti zile za wagonjwa na Mzee..ni aibu.

......
Wewe tajiri shuruba za mwendokasi unazipatia wapi?
Hizi tunazo sisi wakazi wa Mbezi,hizi gari hadi zitunyonge.
 
Saint Anne Mkaka anayenukia โœ…
Mwingine nilipanda naye Bus
Kwenda Dodoma

Alipanda akanikuta,nilikuwa siti ya dirishani....
Akakaa pembeni
Alikuwa ananukia sana,
Bahati alivyopanda akanisalimia.

Kaka wa watu amevaa na saa yake
Shati lake safi ananukia hatari...
Safari ilikuwa fupi aisee...

Tumefika mafinga,
Kaka wa watu kanunua mishkaki alinikaribisha sana nile...mie siku hiyo nilikuwa kama na homa, hivyo niliishia kula biscuits tu.
Akanigawia biscuits

Mimi mtu wa kulala...Kuna muda nilikuwa nalala hadi najikuta nimekaribia kumlalia.
Kaka wa watu alinilindia simu zangu,nilichat nikalala yaani nastuka nalala kama mwehu hadi tunafika Dodoma.

Akashuka ,kumbe alidondosha wallet yake kwenye kiti palepale.. tulikuwa siti za mbelembele..sasa mimi huwa si mtu wa kukimbilia kushuka haraka,huwa nasubiri population ipungue nishuke zangu taratibu especially nikiwa sina mzigo kwenye buti.
Nikaona wahuni wale wavaa sendoz za manyoya na boksa zinachoambaa matakoni na viduku kichwani walipokuwa wanashuka
Wakataka wapite nayo.
Nikawaambia acheni,mwenye nayo yupo anakuja..wakaacha.

Nikaichukua ile wallet..
Nikachungulia nje dirishani nikaona simuoni yule kaka..
Nikahamia upande wa pili nikamuonea yule anataka kutokomea.
Nikamwita akarudi kwenye gari..nikampa wallet yake.
 
Back
Top Bottom