Lamomy hapo kwenye red mwambie Nkamu wako atuelekeze vizuri 🤣🤣🤣
Kuna mijitu mingine
Hadi Kwa watu huwa wanajichoresha tu walivyo wa hovyo pasi hata na kuangalia mavazi Wala sijui viatu perfume.
Siku chache kama wiki 3 hivi nyuma zinepita.
Nilikuwa na mgonjwa hospital amelazwa,hivyo nikawa naenda kumpelekea chakula.
Alfajiri sana nikawahi nimebeba kikapu Cha chakula,na kifungashio na pochi .
Nikawa natembea barabarani ,bahati nzuri gari ikasimama kunichukua sehemu ambayo siyo kituo,nilikuwa sijafika kituoni pa kupandia.
Nimepanda kwenye gari mule na mizigo yangu,gari imejaa
Kama mnavyojua,daladala nyingi coaster,pale mbele uwazi kati ya siti ya dereva na siti ya abiria upande mwingine huwa Kuna wanakaa pale..
Kuna kaka alikuwa amekaa siti ya mwanzo kabisa kutokea Kwa dereva,alikuwa anashuka kituo Cha mbele ambapo nilipaswa kupandia gari...alivyoniona tu nahangaika na mizigo akaniambia dada njoo ukae hapabna mizigo,Mimi nashuka hapo kituoni gari ikisimama..nikamwambia Asante.
Ile ameinuka,nasogea sasa ili nikae....mara kainuka kaka likuwa amekaa ile sehemu ya katikati niliyoisema pale mwanzo,akahamia kwenye ile siti niliyopishwa bila hata aibu.
Nikamwambia kaka naomba nikae
Akanijibu kakae pale nilipohama..
Sasa pale aalipohama ni padogo hapatoshi mm kupakatia vitu vyangu vyotee naye anaona kabisa.
Mimi sikutaka kubishana naye,nikaenda pale nikakaaa...nikapakata mzigo mmoja
Huu mwingine nikamkalishia kwenye miguu yake.
Sasa jitu kama hilo
First impression Kwa watu ni roho yake mbaya...
Huyo hata kama alikuwa na plan ya kuongea na mdada yeyote humo kwenye gari..Kwa roho yake mbaya tayari alishakosa credit.
.....
Uungwana utakupa credit kwa watu.