Saint Anne Mkaka anayenukia β
Mwingine nilipanda naye Bus
Kwenda Dodoma
Alipanda akanikuta,nilikuwa siti ya dirishani....
Akakaa pembeni
Alikuwa ananukia sana,
Bahati alivyopanda akanisalimia.
Kaka wa watu amevaa na saa yake
Shati lake safi ananukia hatari...
Safari ilikuwa fupi aisee...
Tumefika mafinga,
Kaka wa watu kanunua mishkaki alinikaribisha sana nile...mie siku hiyo nilikuwa kama na homa, hivyo niliishia kula biscuits tu.
Akanigawia biscuits
Mimi mtu wa kulala...Kuna muda nilikuwa nalala hadi najikuta nimekaribia kumlalia.
Kaka wa watu alinilindia simu zangu,nilichat nikalala yaani nastuka nalala kama mwehu hadi tunafika Dodoma.
Akashuka ,kumbe alidondosha wallet yake kwenye kiti palepale.. tulikuwa siti za mbelembele..sasa mimi huwa si mtu wa kukimbilia kushuka haraka,huwa nasubiri population ipungue nishuke zangu taratibu especially nikiwa sina mzigo kwenye buti.
Nikaona wahuni wale wavaa sendoz za manyoya na boksa zinachoambaa matakoni na viduku kichwani walipokuwa wanashuka
Wakataka wapite nayo.
Nikawaambia acheni,mwenye nayo yupo anakuja..wakaacha.
Nikaichukua ile wallet..
Nikachungulia nje dirishani nikaona simuoni yule kaka..
Nikahamia upande wa pili nikamuonea yule anataka kutokomea.
Nikamwita akarudi kwenye gari..nikampa wallet yake.