Practically huwezi kusema hapana Single mothers
1. Je wanaojikuta kupeana mimba na baba anafaliki kwa bahati mbaya?
Hawa wanaitwa wajane mradi wawe walifunga ndoa, kama hawakufunga ndoa ni matokeo ya ukahaba. Unajua mtoto wa nje ya ndoa anaitwaje kiingereza?
2. Wanaoachwa kwa sababu pengine za msingi na mama kubakia single na mimba yake
Sababu zipi hasa ambazo unaziita za msingi? Kama ni suala la talaka huwa kuna utaratibu wa jinsi ya kulea watoto, huyo sio single mother maadam amezaa ndani ya ndoa.
3. Wanaobakwa nakujikuta wanabeba mimba zisizotarajiwa
Sheria zipo, lakini suala la ndoa haliangalii huyu alibakwa. Narudia, ndoa sio taasisi ya huruma, kuishi na mwenza maisha yako yote si suala la mzaha kwamba umhurumie mtu kwa sababu ya yaliyomkuta. Binti wa namna hii imempasa kujiungamanisha na Mungu ili kwa mwenendo wake apate mume wa kumfaa. Kubakwa ni tendo la mara moja, hivyo isiwe sababu ya kuingia kwenye ukahaba bali kushika mwenendo mwema.
4. Wanaotapeliwa na wanaume kisha kukimbiwa baada ya mimba
Hakuna mwanamke anatapeliwa na mwanaume. Ukiona binti anatongozwa halafu anatoa mzigo kwa kisingizio cha kudanganywa jua huyo hafai kuwa mke, hana msingi bora wa malezi. Binti ambaye ni wife material kamwe hawezi kujiweka kwenye mazingira ya kudanganywa. Aina hii ya mabinti ni wale wanaodanganyana kusaka wanaume wa kuwaoa, hawajui kwamba mwanamume ndiye anayepaswa kusaka mke. Tumia ufahamu huu kupima aina ya mke mwema, kwa wakristu andiko linasema hivi:
Mithali 19
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana.
Mithali 31
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁰ Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
Mithali 18
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²² Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana.
>>>> Biblia inasema mke mwenye busara anatoka kwa Bwana, maana yake huyu ni mwanamke mwenye hofu ya Mungu, anaishi maisha ya kumcha Mungu, anasubiri wakati wake ampate mume mwenye kumfaa.
Mume atakaye mpata ni yule atafutaye mke, kwani Biblia inasema
apataye mke apata kitu chema, yaani mwanamume hawezi kupata mke labda kama anatafuta katika Bwana. Huyu ni mwanamume mcha Mungu, naye atampata mke huyu aliyejificha katika Bwana. Ndipo Biblia imeuliza ni nani awezaye kumwona? Si mwingine ila yule tu aliye katika Bwana. Si kwa kuombewa na manabii wala kwa kuhudhuria makanisani, huko wamejaa wwnawake waliokosa uelekeo ndipo wakaona wajaribu kutafuta wachumba huko.
Ile kusema "
apataye MKE maana yake si kila mwanamke ni afaa kuwa mke. Hao wengine wanaishia kuwa makahaba tu, bali mke halisi w ndoa atatoka kwa Bwana, yaani ni yule mwenye hofu ya kweli ya Mungu. Kumbe ili kuolewa ni lazima uwe na sifa za kuwa mke, kuwa mwanamke sio sifa ya kuolewa, bali ni kuwa wife material.
A) Single mothers hawawezi kulaumiwa bila kuwepo lawama kwa watia mimba yaani wanaume
Hakuna anayelaumu single mother ila tunatahadharisha vijana waepuke kuoa single mothers kama wanaweza. Majuto ni mengi kuliko. Lakini bado tunasema wanawake wanaochagua kuzalishwa hovyo wasitegemee huruma ya jamii, maadam wwmeamua hivyo basi na wawalee watoto wao.
B) Binadamu tunamapungufu yetu, hakuna aliyemkamilifu 100%. Kujikwaa kupo na sio kosa la anayebeba mimba tu....usimsahau mtiaji mimba.....
Mlee mwanao katika njia impasayo naye hatoiacha. Hakuna lugha nyepesi katika hili. Suala la uasherati halina cha mapungufu, ni chaguo. Biblia inasema dhambi zote hufanyika nje ya mwili isipokuwa uzinzi. Ndio maana tunawaasa binti zetu wajieoushe na uzinzi kwani huathiri mwili na roho pia.
Duniani tuwe na genuine finger pointing than unrealistic one. Sio sahihi mama kubebeshwa lawama za u-single mothers bila kubebisha lawama watia mimba na kuzikimbia au kuzikataa au kuwakataa waliowatia mimba.
Ingawa thread haijasema tuwalaumu single mothers bali vijana mjiepushe kuwaoa nitakujibu tu. Suala la usingo mther linamwathiri mwwnamke zaidi ndio maana tunazidi kuwaonya. Wakati wewe unaweza kuhesabika mwenye huruma, lakini ukweli mchungu ndio tuba kwa vizazi vijavyo. Huruma yako ni mbaya na ya kulenga kuwaangamiza mabinti wajao, bali wakijua ukweli kwamba kujichanganya na kuzalishwa hugeuka mateso kwa mwanamke mwenyewe na kubaki kukimbizana na aliyemzalisha. Sasa niambie wewe, busara ni ipi, azae aonewe huruma ama aonywe kwamba asijefanya upuuzi huo?
Na kwa waliokwisha kuzaa, wanahitaji neema ya Mungu na si wanadamu. Kwetu tumeambiwa mke mwema anatoka kwa Bwana, sasa huyu aliyekiuka maagizo na kuzaa nje ya ndoa tumuweke daraja lipi? Akishikamana na Bwana aweza kupata mume pia, lakini sio sahihi kusema vijana oeni single mothers wakati madhara yako wazi kabisa na ndio sababu ya maonyo ya kwenye Biblia.
Nimalize kwa kukuonyesha mstari huu:
Mithali 10
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.
Ndivyo ilivyo hata kwa single mothers, mtoto akiwa mwenye hekima baba atajivunia naye atashikamana naye (ukubwani) lakini akiwa mjinga mjinga basi mama atajibeba na huyo mwanaye. Hivyo masingle mothers jitahidini kuwalea watoto wawe wenye hekima, hakika mtawaona baba zao wakijitokeza vifua mbele.