Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Umeeleza vizuri wazazi husononeka kwa sababu ya hilo swali kwann aliachwa na aliyemzalisha so unachotakiwa kuwa makini nacho ni hicho
 
Akija kulea wajukuu atajua tu
 
Wewe pokrei na wenzio mnaotaka pingana nami endeleeni. Kwanza mjue huu uzi mods wameubadilisha title mara 2. Title niliyoweka mimi mara ya kwanza (original) wameitoa...wakaweka nyingine, wakabadilisha tena na kuweka nyingine. Title iliyopo sasa imekaa kimabishano kuliko dhamira niliyokuwa nayo mimi.
 
Usimtukane mamba kabla hujavuka mto,haijalishi umeoa tayari au bado😀
 

Unaanzaje kuoa mwanamke aloshazaa.
 
Ukweli ambao ni mchungu Sana kwa vijana ambao hawajaoa.
Wachumba unaokutana nao miaka ya Leo tegemea haya.

Chini ya miaka 20 asilimia 98 wanakuwa hawajazaa au kuwa na watoto

Chini ya 25 unakutana na karibu 70% hawana watoto ila wanatoa mimba

25-30 unakutana na 40% hawana watoto ila wametoa mimba Sana tu.

30-35 ni 20% ndio hawajawahi kuzaa au kuwa na watoto.
Zaidi ya 35 yaani ni msichana mmoja Kati ya 100 ndio atakuwa hajazaa.

Sasa jiulize utawakwepaje hao ambao wameshazalishwa?
Utawajuaje?
 
Pia hakikisha we kijana unaetaka kuoa binti unaemwoa hakikisha anatokea nyumbani kwao...kwa baba yake na mama take ama walezi.
 
Pia hakikisha we kijana unaetaka kuoa binti unaemwoa hakikisha anatokea nyumbani kwao...kwa baba yake na mama take ama walezi.
Ha ha ha ha.
Mkuu siku hizi watu wapo mitaani wanafanya kazi zao na kutafuta kipato.

Na wengine tunakutana vyuoni nk.
Wa kumtoa kwao sidhani Kama wanapatikana
 
Naomba nijitolee kumpa maji kwanza. Akishavuta pumzi ndipo atuhadithie yaliyomsibu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Umenichekesha sana leo Mumy. [emoji23][emoji23][emoji23]
Alipanic vibaya sana
 
1. Mwanaume anaeamua kuoa single mother kashakuwa tayari kukabiliana na changamoto zote kutoka kwa mtoto /watoto wa mkewe yupo tayari kuwalisha, kuwasomesha, kuwavalisha na kuwatibia pindi wanapofikwa na maradhi.....

2. Yupo tayari kukabiliana na machungu ya mawasiliano baina ya mkewe na mzazi mwenzie...huu ni urijali na ukomavu wa kifikra wa hali ya juu kwa mwanaume....

3. Mwanaume alikubali kumuoa single mother anakuwa hana wivu wa kijingajinga kwa mkewe maana anajua mkewe alishapitia kwenye mahusiano mbalimbali mpaka kuja yeye kwa hiyo km akitaka kumsaliti hana njia ya kumzuia....

3. Mwanaume huyu anakuwa haogopi ni jinsi gani baba mtoto wa mkewe alivyokuwa ana participate on bed na mkewe kwamba kujiona yeye atakuwa dhaifu kuliko jamaa aliepita kwa maana hiyo anajiamini

4. Mwanaume wa Karba hii haogopi madongo na mashambulizi yoyote kutoka kwa mzazi mwenzie wa mkewe pindi pale inapotokea mzozano baina ya mkewe na mzazi mwenzie yeye anauwezo wa kuingilia kati na kuyamaliza na mwanaume mwenzie (baba mtoto /watoto) kistaarabu....

5. Mwanaume alikubali kuoa single mother anakuwa sio mbea na kukaa vijiweni maana anaogopa atakandiwa na wenzie so anakuwa busy na maisha yake na wala humkuti akiwasemasema ma single mother kwani yeye mwenyewe anae ndani.....

Naomba niishie hapa

NOTE
Mimi kama mwanaume wa kweli rijali siku moja nilimkuta manzi wangu ambae ni single mother amenuuna vibaya kuja kumuuliza nini tatizo akaniambia amegombana na baba nanihii kisa alimpigia simu na kumlaumu mzazi mwenzie kwanini hampigii simu kumjulia hali mwanae....wakaanza kukorofishana na jamaa kutupia maneno machafu kwahiyo manzi akawa na hasira sana ikabidi mi nimpoze kwa maneno mazuri kwa kweli iliniuma saana ila nitafanyaje na moyo ulishakuwa kwake, ila mpaka sasa tumeshaachana na ninampango wa kuingia kwa single mother mwengine maana najua utamu wao wanakuwa watulivu sana ktk maisha sio km hawa watoa mimba nadhani wanakuaga na laana ya vile vitendo vya abortion wanavyovifanya huwa siwaelewi kabisa na huwa sidumu nao km hawa single mother

NB
Wanaume wenzangu marijali tusiwakejeli hawa Dada zetu single mother ni wazuri sana kwenye maisha achaneni na hawa wachoropoaji hawana uchungu kabisa
 
Uloongea nikweli, ila bado najiuliza kama kweli huu ndio Urijali kwann Ulimuacha ??? ... Nakwann hukumuoa? Ukaishia kumfanya "Demu a.k.a Manzi"?? Na sasa unatafuta mwingine ambaye naye bila shaka unataka umfanye "Manze au Demu" , kwann usitafute na Ukamuoa kweli??.

Ulichosema nikweli ila kitakua 100% proved ikiwa Urijali huo upo kwa Mwanaume aloamua kwa Akili yake kabisa KUMUUOA huyu mama mtu, Lkn sio kumfanya mama mtu kua Demu.

Kinyume nahapo. nikikazia Aya yako ya mwisho.,, nina kila sababu ya kuamini kabisa kabisa 100% kua unapenda kudate nao kwasababu ni wanyonge/ wengi hawajikubali kwaiyo kwa habari ya Kupewa Sex ni Rahisi sana nahilo ndo Hitaji lako.

UKIMPATA MUOE ILI MANENO YAKO YAWE VERIFIED!!!!. lkn sio kuruka ruka na hawa wamama bure nakila siku kuishia kutafuta Excuse ya Kumuacha mara tu baada ya kula Mzigo.
 
Yule wa Mara ya kwanza nia yangu haikuwa kumchezea na kumuacha. Baada ya kuchoka kurukaruka na hawa wasichana wa kawaida na kuona hawaeleweki nikazama kwa single mother yule na nia ni kumuoa na nilidumu nae kwa muda wa miaka miwili na yeye ndie aliyekuwa akinikwamisha kufanya suala la ndoa akisema muda bado kwanza subiri kilichokuwa kinaniuma na kuona napoteza muda ni kwamba Huduma zote yeye na mwanae nilikuwa nampatia alafu then analilia shida kwa mzazi mwenzie so nikaona kama ananicheza shere lakini sina lengo baya na hawa single mother kwanza ni wagumu kukukubali km huna nia njema nao kwani wanaogopa mambo yanaweza kujirudia
 
NMEKUELEWA NKM ILIKUA IVO BASI WEE NI RIJALI WAUKWELI.

Ndomaana jana nikasema "Kijana soma nyakati ,usipotezewe muda"..mtu unamshirikisha mpango wa kumuoa yeye anakuwekea ugumu..... Unamjali sanaaa lkn bado anawasiliana na Ex wake na kumtaja taja mbele yako ovyoovyo ....for sure huyo ni demu mswahili na HAKUA ANAKUFAA.


Nikweli waschana wadogo ni wasumbufu Sanaa nahisi sababu anakua bado anajua nyuma yake anafukuziwa mnooo na usiombr awe nimschana "Mweupe au ana makalio" ... Utaomba pooo.


Fresh Mkuu, endelea kutafuta, ukimpata na akawa mwema OA , akiwa nikm alipita, Usipoteze muda wako bureee ,badala yake utumie tena huo muda kumtafuta anayekufaa mpaka utakapompatia.
 
Mna stress za ngono sasa mnajaribu kupata maoni kwa nguvu.

Nyie tumama mtoto msio na waume, ikiwa sio wajane basi pambaneni na hali zenu, ikiwa ni wajane nawaombea kwa allah mpate waume wa kuwasitiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…