Wakishua tu: Ipi sentensi sahihi kati ya hizi mbili?

Wakishua tu: Ipi sentensi sahihi kati ya hizi mbili?

1 ndio grammar niionayo kwangu kuwa ndo ina sound vizuri ila niongezea neno 'his' mimi ningesema "i m sorry for him having spent 'his' life uselessly", anyways point yako ni nini?
 
Halafu kusoma na kuishi kwa shida ama kiumaskini sio sifa wala si ushujaa ni matatizo tu ya maisha ambayo kipindi mtu mwenye akili timamu hawezi kujivunia na kujisifia huwa ni sehemu ya maisha ya kupita tu ambako mtu hujifunza jambo ili kuja jenga mustakabali mzuri baadae
 
No 1 ipo correct ila kuna makosa kidogo hapo kwenye "Having spent"
 
Mbona sentensi zote hizo zipo sawa tu jamani, Hakuna maswali nilikua siyapendi pale Kwenye CL Yani unapewa sentensi eti unaambiwa zimekosewa uzirekebishe, wakati mimi mwenyewe naziona zipo sawa tu vizuri, mi nilikuaga naongeza nukta tu.
 
Kwanza kabisa me ni miongoni mwa wale ambao kwenda shule ilikuwa lazima uwe na bakora ya kupigapiga umande huku uniform naziweka kwenye mfuko wa rambo ili zisilowe kwa umande..Kinachonishangaza ni kuona hao tabaka la wakishua kupishana.Naona zoote wamezikosoa..Ushauri naomba kwa wale waliojibu waende edit waongeze parandesi na ndani yake waseme shule walizosoma...na watakaojibu sasa basi kwenye parandesi weka na shule....ili tujue vzr
 
Hii inawahusu wale tuliokuwa tunawaita wa kishua enzi zile

20131105_--53.jpg.450x0_q85.jpg


Wale wa St Kayumba wenzangu tulieni kama tulivyokuwa tunatulia shule zisizo na walimu wakati wa debate

Wale ambao wakati me nipo shule ya msingi Minazi Mirefu nyie mlikuwa mnasoma Olympio,Diamond,Heritage au tusiime na zinazofanana na hizo Ndio nawataka mnijibu hapa

10671399_588319254613851_5615997445119658005_n.jpg


Nataka nyie mliokuwa mnasoma wanafunzi 45 dasarani kila mtu kiti na meza yake wakati sisi darasan tulikuwa 120 ukiongeza na Mwl tulikuwa 121 ndio mnijibu.

Hili swali nataka mjibu nyie mliokuwa mnavaa uniform za rangi rangi wakati sisi tulipovaa rangi mbili tu ambazo ni blue (chini) na nyeupe (juu) ndio mjibu.

Najua mpo humu wale ambao uji wa maziwa mlikuwa mnakunywa shule,Ndio nawataka mnijibu hapa.

Nyie ambao mnadhani madumu ya mafuta ya korie hayawezi kutumika kubeba mji kupeleka shule ndio mnijibu hili swali.

Nyie ambao hamjawahi kuwasalimia walimu kwa kuweka kidole gumba juu ya kichwa na vidole vingine vikiwa vimenyooshwa wakati wa kumsalimia mwalimu ndio mnijibu

Nyie ambao kingereza kwenu ilikuwa sio tatizo ila tatizo kubwa ni hesabu ndio nahitaji majibu yenu hapa leo hii

Nyie ambao hamkuwahi kupanda daladala na mbolea kupeleka shule ndio mnijibu hili na msikose tafadhali

Nataka swali hili lijibiwe na nyinyi mliokuwa waongeaji kwenye debate tulipokutana sec tukawa tunawashangilia bila kuelewa mlimaanisha Nini Ndio mnijibu na ole wake majibu yenu yatofautiane

Swali ni hili

IPI ni sentence sahihi kati ya hizi 2 za Kingereza

1.I am sorry for him having spent life uselessly.

2.I am sorry for his having spent life uselessly

Haya karibuni sana wazungu wa Kibongo!
1.I am sorry for him having spent life uselessly.

2.I am sorry for his having spent life uselessly

Zote ni sahihi.

No. 1. Unamhurumia yeye mwenyewe kwa kitendo cha kupoteza muda wake maishani. (UNAMHURUMIA ALIEKIFANYA HICHO KITENDO)

No. 2. Unahurumia kitendo cha kupoteza muda wake maishani. (UNAKIHURUMIA KITENDO)
 
Back
Top Bottom