Kranium
Senior Member
- Oct 20, 2014
- 130
- 376
Lakini wanakuwa wamekusanya pesa za kutosha uzeeni hawapati tabu. Huku kwetu wanakomaa hadi uzeeni kisa njaa
Tatizo wa kwetu wanaingia kichwa kichwa kuhusu mikataba ya label au kupromote bidhaa au huduma flani ya kampuni....hawana hata mwanasheria wa kuwatafasiria sheria/taratibu za mkataba...kiufupi wametanguliza sana njaa mbele, mwisho wa siku wanakuja kulia wamedhulumiwa au wanahitaji mchango wa matibabu n.k. kutoka kwa mashabiki pindi wanapopata maswaibu.
Kitu kingine, hawawekezi kwenye biashara zingine. Wao hufikiria watadumu milele kwenye music industry. Hata wakianzisha biashara huamini jina lao pekee litatangaza. Kwenye biashara kuna mambo mengi ya kufanya kuliko wanavyofirikiria....
Kilichobakia sasa hivi wanaangalia nani anaongoza views nyingi youtube, followers wengi instagram na shangwe nyingi za jukwaani ukijumlisha na kiki za maisha fake kwa kusema wamenunua nyumba au gari. Bila kuangalia uhalisia wa kipato chao wanachoingiza na maisha yao halisi wanayoishi kwenye social media...ni vitu viwili tofauti. Wanaishi kufurahisha mashabibiki kwamba wana maisha ya juu.