Wako wapi wale waliokuwa wanatetea umeme wa maji utakuwa bei rahisi?

Wako wapi wale waliokuwa wanatetea umeme wa maji utakuwa bei rahisi?

wakafikia hatua wakasema kupikia umeme kutakuwa nafuu kuliko gharama gesi na mkaa.
Walaaniwe wote
 
Nyie ndio wanaccm, na akajaza wabunge wa ccm ili wasimkwamishe. Je hilo bunge la chama kimoja aliloliweka linaloendana na falsafa zake nalo limezikwa naye?

Isitoshe yeye ndio aliyenunua ndege, mbona hazikuwa na nauli ndogo kama ilivyokuwa fastjet, ili tujue kwenye miradi yake bei ingekuwa nafuu?
Jiulize kwanza ye bado yupo?? Si kila mtu anaweza kubeba maono..
 
Sijui kwanini wajinga wana penda kuwabishia wenye akili
 
Wakati ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere unaanza, watetezi wake walikuwa wanatoa mishipa ya shingo kuwa bwawa hilo likianza kazi umeme utashuka bei. Nikawa nasema miaka yote tumekuwa tukitumia umeme wa maji, lakini hatukuwahi kuwa na sifa ya umeme wa bei rahisi, maana sababu ya umeme kuwa ghali hapa nchini haiendani na gharama za uzalishaji, bali sababu nyingine kabisa.

Watetezi wakawa wanasema gharama kubwa haiwezi kupungua kwa kutumia umeme wa mafuta. Wakajiapiza umeme wa maji ukianza automatically bei itashuka.

Wakati umefika na kile nilichosema kinaonekana. Bwawa limeanza kazi, umeme unazidi kupanda bei, na kibaya zaidi bado sio wa uhakika maana mgao bado upo, hata kama sio kwa kiwango kikubwa. Kwenye hili la bei wote ni mashahidi kwa walioanza kununua umeme hivi karibuni. Na hapo bado.

Paskali Mayalla Choicevariables, Lucas Mwashamba
Unakumbuka pia mradi wa gesi asilia ya Mtwara ulipoanza mbwembwe zilivyokuwa? Leo husikii tena mambo kama yale yaliyokuwa yakizungumuzwa wakati ule. Huwa tunaweka ushabiki mwingi kwenye mambo ya kitaalamu.
 
Back
Top Bottom