Tatizo la Africa / Tanzania ni vipaumbele & wizi
Hii methali huwa ninaupenda.
Mfano kuna haja gani ya mkurugenzi , DC , RC katika mikoa 26 yote kutembelea gari za milioni 500+ .
Je gharama za kuhudumia hizo gari , misafara isiyo na tija , matengenezo na mafuta nani anafanya??
Ukiona hilo utajua mzigo unamuangukia mwananchi wa chini hata hicho anachokamuliwa kikitoka bado [ mafisadi/majizi] yanakitolea mate na yanakikwapua ushahidi ni upi jibu ni ripoti ya CAG!
Je ikifikia hatua matumizi ya anasa kama hayo tu ya gari tuseme watembelee gari tu za milioni 10-20 nini kitapungua ?
Pesa kiasi gani itakuwa imeokolewa kwenye gari zinazohitaji pesa nyingi kuzitunza !
Hebu fikiria hayo mamilioni yakiokolewa na kwenda kuwa "subsidized " kwenye mradi wa umeme watu wapate umeme kwa gharama nafuu utahitaji kukodi vikundi vya wasifiaji eti " Mama anaupiga mwingi"??
Juzi tu hapo tumeona vilio vya kodi ya jengo kwenye umeme imeongezeka 500/= tu imekuwa story ya siku.
Watawala hawajali maana wananchi sio kipaumbele chao na hizo gharama watawala hao hata hawajui zinalipwaje maana ni jasho la wananchi linawalipia pesa ya ununuI wa gari, bili za maji, umeme, usafiri, posho, mishahara.
Halafu baadae mtu anakuja kusema "Mama ametoa bilioni......"
Bajeti ukiona pesa za maendeleo ni kiduchu ila "matumizi mengine" ni rundo la pesa kwenye mengine humo ndio wezi wanajipakulia.
Kiufupi watawala wanaiibia nchi kwa kuwarubuni wananchi kuwa wako vizuri kwa kuwapa vitu wasivyo na uhitaji navyo huku vilivyo na uhitaji hawapewi.
Niishie hapo kwa leo.