Wakongo wanashambulia madereva wanaokwenda kusafirisha shaba, hali ni mbaya

Wakongo wanashambulia madereva wanaokwenda kusafirisha shaba, hali ni mbaya

mambio

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2017
Posts
2,668
Reaction score
3,428
Kama kichwa cha taarifa hapo juu. Hali si shwari Kongo




====

Kongo kumechafuka, na hali si shwari toka tarehe 2/2/2024, Wakongo hawataki shaba (copper) itoke nchini mwao, gafi yako ikibeba shaba kusafirisha nje inashambuliwa.

Gari hiyo inayoonekana kwenye video inasemekana ni kutoka kampuni ya Azania Group, ambapo dereva na utingo wake walishambuliwa wakiwa njiani kusafirisha shaba, inasemekana dereva alifariki ila utingo wako haijulikani ana hali gani.

Baadhi ya Watanzania waliokwama huko waomba msaada kwa serikali kutoa tamko na kuwapatia msaada ili waweze kurudi nchini, pia wamewatahadhirisha madereva wengine kutokwenda Kongo kwa sasa.
 
Raia zimevurugwa ni mwendo wa kuchoma magari na kushambulia madereva.
Tuwaombee uzima madereva wa wabongo walioupande wa KONGO
 
Huyo hapo juu ni dereva wa kutoka zambia.
Kapigwa mawe km nyoka hivi sasa ni marehemu. Damu imemtoka nyingi sana na msaada hakuna.
 
Huyo hapo juu ni dereva wa kutoka zambia.
Kapigwa mawe km nyoka hivi sasa ni marehemu. Damu imemtoka nyingi sana na msaada hakuna.
Inasikitisha sana. Naombaga nisikutwe kwenye matukio kama haya.
 
M23 wanatembezewa kichapo kizito sana wametoa tamko la kuwalalamikia jwtz na kuapa kuhamishia nguvu zao zote kwa jwtz walio kwenda Congo.

Kwa ufupi hali itakuwa mbaya sana, Kwa sasa Maeneo ya Congo yenye waasi si salama
 
Back
Top Bottom