Tanzania Samia Connect inayotarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 21- 23, 2025 inatarajiwa kuwakutanisha katika jukwaa moja wasanii zaidi ya 50 kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Arusha, ikiwemo wakongwe wa muziki kutoka Jijini Arusha Fido Vato anayetamba na wimbo wa 'Chuga hiyo' pamoja na JCB aliyevuma na Wimbo wa 'Ukisikia paah'.
Kulingana na Wasanii hao kwaniaba ya Wakongwe wengine wa Muziki Mkoani Arusha wameahidi kutoa burudani ya kutosha kwa kila mwananchi atakayefika kwenye viwanja vya Mgambo, Uzunguni Jijini Arusha, wakihimiza Vijana pia wenye Vipaji kujitokeza kwa wingi kuja kuonesha vipaji vyao kwenye Tamasha hilo lililoasisiwa na kuratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Kenani Laban Kihongosi.
Kadhalika JCB na Fido Vato wamempongeza pia Kihongosi kwa ubunifu wake huo, wakisema Tanzania Samia Connect ni mkombozi kwa wananchi wenye kuhitaji huduma mbalimbali za serikali ikiwemo matibabu, hati na nyaraka nyingine za serikali ikiwemo Vitambulisho vya Taifa, Wakilitaja Tamasha hilo pia kama kichocheo muhimu cha sanaa na Muziki wa Arusha pamoja na kuchangia katika kukuza uchumi wa Mkoa kutokana na ugeni utakaokuwepo kwenye Tamasha hilo la Tanzania Samia Connect 2025.