and 100 others
JF-Expert Member
- Feb 3, 2023
- 3,707
- 12,367
Msn Messenger 2007, kipindi hiko watoto wadogo mnafundishwa "that is an orange" sisi tulikuwa humu msn tukisoma habari za mambele na kufuatilia ulimwengu unaendaje..
Hii marafiki, juu hapo kuna kitangazo cha Buzz, miaka ya 2005/2006 kama sijasahau... mwanzoni iliitwa darchat kama sijasahau... watoto wengi humu kipindi hiki mnajisaidia kwenye nguo... kwa kipindi hiko hii ndio ilikuwa kama tinder sasa, nilipata manzi anaitwa Mwaju miaka hio sintosahau..
Bongo5 miaka ya 2007/2008..
Darhotwire miaka ya 2007/8/9... hapa wakongwe wengi mnakumbuka vingi sana kabla ya jamiiforums...
Tanzatl, hii nadhani ilikuwa miaka ya 2004 kama sijasahu niko primary school ,.. kipindi hiko unamaliza darasa la saba una ndevu ushanyoa hadi upele kwenye kidevu..
Jamboforums kabla haijavamiwa na watoto wa 2000s, hapa ni 2006/2007 nadhani kabla haijawa jamiiforums...
Jamboforums 2006.... now jamiiforums, kipindi hiko wanafanya na donation ku run site...
Business times au bcstimes.com--- hapa miaka ya 2004/2005 hata jamiiforums haipo, humu ndipo tulikuwa tunaingia kusoma habari, udaku, magazeti n.k
Hii ni hi5 miaka ya 2002 kama sijasahau au 2003...
Hii ni jambonet miaka ya 2004 i think so... hapa ilikuwa page under maintenence... nakumbuka...
Hii ilikuwa ni YoungAfricans, miaka ya early 2000s.. kipindi hicho wengine ndio mnazaliwa halafu leo mnatutukana humu jamiiforums...