Wakongwe wenzangu mnakumbuka wapi?

Wakongwe wenzangu mnakumbuka wapi?

Bado dogo tu kumbe na wewe kama 2004 ulikuwa Primary. 2004 nilikuwa nikeshamaliza degree yangu pale SUA na nilikuwa mwaka wa 3 kazini kule Kanda ya Ziwa mkuu kabla sijaanza kuuza madafu.
Si haba, 2004 hapo nimerudia, si unajua zamani la saba ilikuwa dili ..hahahah... shule nzima mnafaulu 10...
 
MODEM za US Robotics and Dialup connection ya TTCL..
Tumetoka mbali mzee..

TTCL nakumbuka kwenye website yao walikuwa na huduma ya broadband, wakisema ni high speed 2006 hio.
download speed ilikuwa 512kb/sec hio ni 5G kwa sasa...
Halafu upload speed ilikuwa 128kb/sec...
Unlimited waliuza kwa dola 700 kila mwezi, na installation charges ilikuwa ni dola 500... 5GB mwezi mzima installation ni dola 150 huku kila mwezi unalipa dola 167...

Si mchezo watu wametoka mbali...

Hapo chini nimeweka bei zao kipindi hiko


ttcl.png

ttcl2.png
 
Back
Top Bottom