Wakopeshaji umiza kwa watumishi wa umma ni matokeo ya sera za CCM

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Mara kwa Mara ukiiangalia taarifa za habari utakutana na watu wanaoitwa wakopeshaji umiza. Hawa ni shylocks kwa lugha ya Kiingereza au ukipenda waite "mashailoki". Hawa jamaa wanawakopesha watumishi wa uma kwa masharti makali na ya aibu mno.

Kwanza riba ni kubwa sana inaanzia 40%+ lakini pia watumishi wa umma wanatakiwa kuacha kadi kwa Shylock huyo pamoja na namba ya Siri halafu mshahara ukitoka yule Shylock ndio anaenda kumchukulia mtumishi mshahara. Hii ni aibu mno kwenu watumishi wa umma.

Cha kushangaza hata wastahafu maskini ya Mungu wanapigwa mno na Hawa jamaa. Yani wakijua mwalimu Makonda mfano anastahafu mwezi ujao wanamfwata au wanatuma madalali wao kumshawishi mwalimu Makonda akope hela na wanampa mfano kwakuwa riba Yao ni 40% wanamfwata mwalimu Makonda mwenye shida lukuki wanamwambia sisi tunakupa milioni kumi Ila hela yako ikitoka utatulipa milioni 14 mwalimu Makonda anapiga hesabu anaona kiinua mgongo chake akilipwa mwezi ujao atapata 60,000,000/= anaona kutoa milioni nne ni Jambo dogo Bora avute hiyo kumi fasta.

Maskini ya Mungu kiinua mgongo hakitatoka kwa muda aliodhani hivyo atapigwa riba kila mwezi labda ya laki Saba hivyo Kama kiinua mgongo kitakaa miezi kumi inamaana atalipa milioni Saba Kama penalty ya kuchelewesha mkopo.

Mwisho wa siku mwalimu anajikuta anapoteza milioni 21 kwa Shylock kea njia ya kitapeli.

Baadae mwanasiasa anakujankumtetea mwalimu huyo ili arudishiwe hela zake tumeona haya yakifanywa na wakuu wa mikoa kupitia takukuru.

Mwalimu Makonda anaenda kuanikwa mbele ya kamera dunia nzima inamuona kwamba alikopa kea mkopeshaji umiza na akapigwa hela nasasa mkuu wa mkoa kamsaidia hela zimerudi. Hii ni fedheha kubwa mno kwa walimu wetu na manesi maana ndio wakopaji wakubwa. Chaneli zote za TV Tanzania zinamwonyesha mwalimu Makonda alieacha kadi kwa Shylock aibu mnooooo.

Mbaya zaidi.

Nasikia watumishi wa mabenki wanamgao wao kutoka kwa hawa jamaa.

Watumishi wa mabenki wanafanya kazi mbili.

1. Kuwaambia mashylock kwamba Leo mshahara unaingizwa usiku hivyo mkae tayari na kadi.

2. Watumishi wa mabenki huwatonya mashylock chochote kinachoendelea katika akaunti ya mwalimu Makonda au hata akitaka kuattempt kubadilisha kadi.

Wasichojua watumishi wa umma ni Nani kawasababishia haya yote?

Watumishi wa umma mpaka mnadhalilishwa mbele ya kamera kwamba mnakopa kwa wakopeshaji umiza hamumjui mbaya wenu?

Niliona eti mtwara polisi wamekamata kadi za benki 600 ambazo nyingi ni za walimu na manesi.

Wengi wa wakopeshaji umiza Hawa wanatoka mkoa wa Mara fita ni find muraaaaa.

Poleni sana walimu na manesi mkipata nafasi ya kutumia akili kila baada ya miaka mitano itumienii.

Mashylock oyeeeeeeee.

Kama mayahudi yaniiii.
 
Kama mkopeshaji umiza mmoja anakuwa na kadi 600 za watumishi je itakuwa kosa kusema 80% ya kadi za watumishi wa umma Tanzania zipo kwa wakopeshaji umiza?
 
Wasipoongeza mishahara itafikia 100%
 
Huyo Mwalimu Makonda uliyemtolea mfano ana uhusiano na huyu Mh. Paul Makonda Rais wa Dar?

Anyway Serikali ya awamu ya 5 inayo ongozwa na Chama Cha Mapinduzi a.k.a Ccm, haina budi kuona haya kwa uonevu inaowafanyia Wafanyakazi Wazalendo wa Nchi hii!

Yaani kwa Miaka 5 ya kwanza ya utawala wao hakuna cha nyongeza ya Mshahara, hakuna Annual Incriment, Madaraja yanapanda kwa kusuasua, wamewaongezea makato ya Bodi ya Mikopo kutoka asilimia 8 mpaka 15,

Hakuna ajira mpya kwa Walimu wa masomo ya Sanaa! Hao Walimu wa masomo ya Sayansi na wenyewe wamejazana mtaani! Halafu utashangaa na Mwaka huu 2020 bila hata aibu wataingia mtaani na yale manguo yao ya Kijani kuomba tena kura!

Si bora hata wangemuachia walau miaka 5 tu Mh. Hashim Rungwe Spunda ili tuishi maisha ya peponi! Kila Mtanzania angekua na shibe masaa 24!
 
Niliwani kukopa pale Platinum million 2 wakanilamba million sita kwa miaka miwili, kumbe kuna form wanakupa nyingine wanakuja kuijaza wenyewe wanaifoji na sahihi ya mkurugenzi na mhuri alafu unashngaa mshahara wa kwanza unakatawa hela nyingi, nilienda kufuta deli palikuwa hapatoshi. kikakuta na wanajeshi wawili wamewasha moto , walikuja kurudisha hela kwa fujo kali sana, wana wanasheria wao wa kiwizi wizi, cha kushangaza mkurugenzi mkuu ni, alyekuwa msemaji wa kikwete, pamoja na Jaji walioba hapo nilichoka
 
Mbowe anaikopesha chadema kila mwaka kwa riba kubwa Sana na anajilipa million 50 kila mwezi Kama riba ya mkopo aliokikopesha chadema. Sasa huyu Mbowe anatekeleza service za CCM?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kali aisee Yani watumishi wanalizwa vibaya mnoooo na hawana mtetezi
 
Mbowe anaikopesha chadema kila mwaka kwa riba kubwa Sana na anajilipa million 50 kila mwezi Kama riba ya mkopo aliokikopesha chadema. Sasa huyu Mbowe anatekeleza service za CCM?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza nchi ipo chini ya serikali gani?? Kama ingekuwa kosa hilo kwa mujibu wa sheria mbona hashtakiwi? Uwe unatumia akili wakat mwingine...
 
Sasa Kama wakopeshaji umiza siyo tatizo kwanini huyu mleta mada anailaumu CCM? Wachangia I wengi hata wewe ulikubali kuwa Hawa wanatokana na Sera mbovu za CCM. Kukumbushwa kuhusu Mbowe kuwa nae ni mkopeshaji umiza unaanza ooh mbona hashtakiwi Sasa hao wengine nao waachwe Kama alivyoachwa Mbowe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara kwa Mara ukiiangalia taarifa za habari utakutana na watu wanaoitwa wakopeshaji umiza. Hawa ni shylocks kwa lugha ya Kiingereza au ukipenda waite "mashailoki". Hawa jamaa wanawakopesha watumishi wa uma kwa masharti makali na ya aibu mno.

Kwanza riba ni kubwa sana inaanzia 40%+ lakini pia watumishi wa umma wanatakiwa kuacha kadi kwa Shylock huyo pamoja na namba ya Siri halafu mshahara ukitoka yule Shylock ndio anaenda kumchukulia mtumishi mshahara. Hii ni aibu mno kwenu watumishi wa umma.

Cha kushangaza hata wastahafu maskini ya Mungu wanapigwa mno na Hawa jamaa. Yani wakijua mwalimu Makonda mfano anastahafu mwezi ujao wanamfwata au wanatuma madalali wao kumshawishi mwalimu Makonda akope hela na wanampa mfano kwakuwa riba Yao ni 40% wanamfwata mwalimu Makonda mwenye shida lukuki wanamwambia sisi tunakupa milioni kumi Ila hela yako ikitoka utatulipa milioni 14 mwalimu Makonda anapiga hesabu anaona kiinua mgongo chake akilipwa mwezi ujao atapata 60,000,000/= anaona kutoa milioni nne ni Jambo dogo Bora avute hiyo kumi fasta.

Maskini ya Mungu kiinua mgongo hakitatoka kwa muda aliodhani hivyo atapigwa riba kila mwezi labda ya laki Saba hivyo Kama kiinua mgongo kitakaa miezi kumi inamaana atalipa milioni Saba Kama penalty ya kuchelewesha mkopo.

Mwisho wa siku mwalimu anajikuta anapoteza milioni 21 kwa Shylock kea njia ya kitapeli.

Baadae mwanasiasa anakujankumtetea mwalimu huyo ili arudishiwe hela zake tumeona haya yakifanywa na wakuu wa mikoa kupitia takukuru.

Mwalimu Makonda anaenda kuanikwa mbele ya kamera dunia nzima inamuona kwamba alikopa kea mkopeshaji umiza na akapigwa hela nasasa mkuu wa mkoa kamsaidia hela zimerudi. Hii ni fedheha kubwa mno kwa walimu wetu na manesi maana ndio wakopaji wakubwa. Chaneli zote za TV Tanzania zinamwonyesha mwalimu Makonda alieacha kadi kwa Shylock aibu mnooooo.

Mbaya zaidi.

Nasikia watumishi wa mabenki wanamgao wao kutoka kwa hawa jamaa.

Watumishi wa mabenki wanafanya kazi mbili.

1. Kuwaambia mashylock kwamba Leo mshahara unaingizwa usiku hivyo mkae tayari na kadi.

2. Watumishi wa mabenki huwatonya mashylock chochote kinachoendelea katika akaunti ya mwalimu Makonda au hata akitaka kuattempt kubadilisha kadi.

Wasichojua watumishi wa umma ni Nani kawasababishia haya yote?

Watumishi wa umma mpaka mnadhalilishwa mbele ya kamera kwamba mnakopa kwa wakopeshaji umiza hamumjui mbaya wenu?

Niliona eti mtwara polisi wamekamata kadi za benki 600 ambazo nyingi ni za walimu na manesi.

Wengi wa wakopeshaji umiza Hawa wanatoka mkoa wa Mara fita ni find muraaaaa.

Poleni sana walimu na manesi mkipata nafasi ya kutumia akili kila baada ya miaka mitano itumienii.

Mashylock oyeeeeeeee.

Kama mayahudi yaniiii.
Mbowe nae mkopeshaji umiza kaikopesha Chadema kwa riba kubwa na anajilipa 50ml kwa mwezi Kama riba. Sasa hao waalimu na manesi ambao waeumizwa na wakopeshaji umiza wanaotokana na Sera za CCM unawashauri Nini baada ya kupata hii nafasi adimu ya miaka mitano? Kati ya CCM na Mbowe Kuna anayefaa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nadhani hapa tatizo siyo MTU KUKOPA ama KUKOPESHA....

KUKOPESHANA binadamu ni jambo la kawaida sana na ni sehemu ya maisha ya kusaidiana pale mmoja anapokuwa amekwama.....

Shida iliyopo siku hizi kwa binadamu kuingiliwa na pepo la tamaa. Na kwa sababu hii, "NIA" ya "MIOYO" watu imechafuliwa na tamaa hizi. Hii ni kwa pande zote "Mkopaji" na "Mkopeshaji"...

Sasa, tatizo lililopo ni wakopeshaji ambao kwa kweli wengi wao wako kisheria na wamesajiliwa na BoT chini ya sheria ya "Micro finance services " kukiuka masharti yayowaongoza kufanya kazi zao....

Hivi vitaasisi vya fedha vidogo vidogo vya kukopesha vikifuata utaratibu ulioko kisheria, hawataweza kuhimili kuwepo sokoni kwa sbb wateja wengi wako absorbed na mabenki ambazo zinafanya jukumu hili kwa uwazi zaidi na kwa riba ndogo zaidi....

Wanachofanya hawa Mashailoki ni kutumia shida na "ujinga" wa watu wanaowakopesha kuwaibia kwa njia hii....

Wote tunafahamu kuwa shida haina adabu. Mtu ukiwa na shida inayohitaji fedha kutatuliwa, mara chache huwa hatukirii namna bora na salama ya kupata fedha hiyo. Njia yoyote inayokuja mbele yako inaweza kuwa sawa tu kwa wakati huo, madhara baadae...

Na kwa sababu hiyo ndiyo maana watu tunajikuta tumejiingiza kwenye madeni ya hatari kutoka kwa hawa jamaa na namna ya kujichomoa huko inakuwa ngumu kwelikweli....

Na mtu hugundua kuwa nilifanya maamuzi yasiyo sahihi huku akiwa tayari anaogelea kwenye madhara ya maamuzi yake yanayomuathiri yeye binafsi, kazi na familia ya wote wanaomtegemea....

Na hawa jamaa (Shylocks) wamefanya mambo yafuatayo kuvuta ndege wengi wajinase wenyewe.......;

1. Kwanza ukienda, wao wanazo keshi hapo hapo ofisini kwao. Huhitaji mzunguko wala mchakato kama ule wa kibenki amabao huchukua hadi wiki kupata fedha yako...m

2. Hawana mlolongo sijui usainishe fomu kwa mwajiri wako, ama serikali ya mtaa ama mahakamani nk nk

3. Wao fomu zao walishakula "deal" tayari na viongozi hawa na wana wanasheria wao na pengine mahakimu kabisa wa mahakama za chini ambao wote hawa wana fungu lao katika wizi na hujuma hii dhidi ya raia hawa masikiñi wa kipato na akili na upande mwingine Serikali kukosa mapato

4. Kinachotakiwa ni mteja kuwa na vitu viwili ama vitatu tu;
å Valid kadi ya benki unakopitia mshahara wako
å Bank statement ya unakopitia mshahara wako kuithibitisha hiyo akaunti yako

å Copy ya kitambulisho chako cha kazi

Ukiwa na hivi vitu utajaza fomu yao hapo hapo fast fast na kupewa fedha yako CASH hapo hapo. Kama utaenda baa kunywa, unaenda. Kama una akili utazielekeza kwenye kusudi la kukopa....

KWA HIYO;

å Ni kweli kabisa riba (accumulated interest) yao ni kubwa kupita kiasi na ni kati ya 40% na 50%......

√• Mfano, unachukua Tsh. 1,000,000 kwa muda wa miezi 6 na kama interest ni 50% , maana yake utarejesha Tshs. 1,500,000 ÷ 6 = 250,000 kila mwezi...!!

5. Sharti moja ni kuwa WEWE MTEJA HAWAKuRUHUSU UENDE AMA KUKUPA NAKALA YA MKATABA ULIOJAZA...!!

Hivi ndivyo biashara hii nono inavyofanyika...

Hata hivyo wakopeshaji wengi wameshaingia kwenye mgogoro na baadhi ya wateja wao (wajanja na wenye akili) waliowakopesha baada kuigundua janja hii na kugoma kulipa....

Nimeishudia kesi hii mwenyewe ikimhusu mtumishi wa umma (idara kapuni) na mkopeshaji (jina kapuni) ktk wilaya ya Shinyanga...

Kilichofanyika, ndugu huyu alienda akakopa Tshs 1,000,000 kwa riba ya 40% kwa marejesho ya miezi 5 sawa na Tshs 1,400,000 ÷ 5 = 280,000....

Ndugu huyu akafanya rejesho moja tu.....

Miezi iliyofuata na kwa kuwa kadi ya benki aliacha kwa mkopeshaji kama dhamana, alichofanya ni kwenda benki na kui - block kadi hiyo na akapewa kadi mpya.....

Mkopeshaji kila alivyoenda benki kuchukua chake, akawa hana access, kupata fedha, Card blocked....!

Baada ya muda fulani wakamfungulia kesi ya madai huyu ndugu. Kosa moja wakafanya hawa jamaa. Wakatumia kanuni na ujanja janja wao wa kimahesabu na kuliongeza deni hadi ikazidi principal amount aliyokopa huyu ndugu mara mbili....!

Alikuwa anadaiwa 1,120,000, sasa deni ni karibu 3,500,000+....!!

Kesi iliunguruma kwa kama miezi miwili hivi. Amini usiamini, mkopaji alishinda na kuamuliwa na mahakama alipe hela ileile aliyokopa....

Hapa tatizo hili kweli lipo na haliwahusu walimu ama manesi tu bali ni watumishi wote kada ya umma ama binafsi na hata watu wa kawaida tu wenye shughuli/biashara zao binafsi ili mradi wanakopesheka na wana dhamana fulani....

TUKUMBUKE PIA KUWA;

å Kisheria mtu mwingine kukaa na kadi ya benki ya mtu mwingine ni kosa....

å Vivyo hivyo katika Sera ya fedha na mikopo za taasisi za fedha hakuna riba ya kiwango cha 40%+....

å Kwa tafsiri ya haraka na ya wazi ni kuwa, wanachofanya hao Mashailoki ni WIZI kwa wateja wao na ni WIZI wa mapato ya serikali....!!

Narudia tena KUKOPA na KUKOPESHANA wala siyo tatizo na siyo dhambi....

Tatizo linakuja NIA na DHAMIRA za pande zote mbili (mkopaji & mkopeshaji) ni nini....

ALL in ALL, biashara hii ni nzuri sana lakini it's totally illegal....

Maana kama una mtaji wa 10,000,000 tu na ukawa na wateja 100 tu na unawakopesha kwa staili hii na wote wakawa wanakurejeshea bila shida.....

Kwa kweli ndani ya muda mfupi sana wewe unakuwa milionea...!!

Tatizo ni WIZI...
 
Mara kwa Mara ukiiangalia taarifa za habari utakutana na watu wanaoitwa wakopeshaji umiza. Hawa ni shylocks kwa lugha ya Kiingereza au ukipenda waite "mashailoki". Hawa jamaa wanawakopesha watumishi wa uma kwa masharti makali na ya aibu mno.

Kwanza riba ni kubwa sana inaanzia 40%+ lakini pia watumishi wa umma wanatakiwa kuacha kadi kwa Shylock huyo pamoja na namba ya Siri halafu mshahara ukitoka yule Shylock ndio anaenda kumchukulia mtumishi mshahara. Hii ni aibu mno kwenu watumishi wa umma.

Cha kushangaza hata wastahafu maskini ya Mungu wanapigwa mno na Hawa jamaa. Yani wakijua mwalimu Makonda mfano anastahafu mwezi ujao wanamfwata au wanatuma madalali wao kumshawishi mwalimu Makonda akope hela na wanampa mfano kwakuwa riba Yao ni 40% wanamfwata mwalimu Makonda mwenye shida lukuki wanamwambia sisi tunakupa milioni kumi Ila hela yako ikitoka utatulipa milioni 14 mwalimu Makonda anapiga hesabu anaona kiinua mgongo chake akilipwa mwezi ujao atapata 60,000,000/= anaona kutoa milioni nne ni Jambo dogo Bora avute hiyo kumi fasta.

Maskini ya Mungu kiinua mgongo hakitatoka kwa muda aliodhani hivyo atapigwa riba kila mwezi labda ya laki Saba hivyo Kama kiinua mgongo kitakaa miezi kumi inamaana atalipa milioni Saba Kama penalty ya kuchelewesha mkopo.

Mwisho wa siku mwalimu anajikuta anapoteza milioni 21 kwa Shylock kea njia ya kitapeli.

Baadae mwanasiasa anakujankumtetea mwalimu huyo ili arudishiwe hela zake tumeona haya yakifanywa na wakuu wa mikoa kupitia takukuru.

Mwalimu Makonda anaenda kuanikwa mbele ya kamera dunia nzima inamuona kwamba alikopa kea mkopeshaji umiza na akapigwa hela nasasa mkuu wa mkoa kamsaidia hela zimerudi. Hii ni fedheha kubwa mno kwa walimu wetu na manesi maana ndio wakopaji wakubwa. Chaneli zote za TV Tanzania zinamwonyesha mwalimu Makonda alieacha kadi kwa Shylock aibu mnooooo.

Mbaya zaidi.

Nasikia watumishi wa mabenki wanamgao wao kutoka kwa hawa jamaa.

Watumishi wa mabenki wanafanya kazi mbili.

1. Kuwaambia mashylock kwamba Leo mshahara unaingizwa usiku hivyo mkae tayari na kadi.

2. Watumishi wa mabenki huwatonya mashylock chochote kinachoendelea katika akaunti ya mwalimu Makonda au hata akitaka kuattempt kubadilisha kadi.

Wasichojua watumishi wa umma ni Nani kawasababishia haya yote?

Watumishi wa umma mpaka mnadhalilishwa mbele ya kamera kwamba mnakopa kwa wakopeshaji umiza hamumjui mbaya wenu?

Niliona eti mtwara polisi wamekamata kadi za benki 600 ambazo nyingi ni za walimu na manesi.

Wengi wa wakopeshaji umiza Hawa wanatoka mkoa wa Mara fita ni find muraaaaa.

Poleni sana walimu na manesi mkipata nafasi ya kutumia akili kila baada ya miaka mitano itumienii.

Mashylock oyeeeeeeee.

Kama mayahudi yaniiii.
NAUNGA MKONO HOJA.WALIMU,MANESI WANAUMIZWA SANA.WENGINE WANAACHA NA ATM CARDS ZAO
 
Mimi nadhani tatizo hapa siyo MTU KUKOPA ama KUKOPESHA ama KUKOPESHANA watu.....

Tatizo lililopo ni wakopeshaji ambao kwa kweli wengi wao wako kisheria na wamesajiliwa na BoT chini ya sheria ya "Micro finance services " kukiuka masharti yayowaongoza kufanya kazi zao....

Hivi vitaasisi vya fedha vidogo vidogo vya kukopesha vikifuata utaratibu ulioko kisheria, hawataweza kuhimili kuwepo sokoni kwa sbb wateja wengi wako absorbed na mabenki ambazo zinafanya jukumu hili kwa uwazi zaidi na kwa riba ndogo zaidi....

Wanachofanya hawa Mashailoki ni kutumia shida na "ujinga" wa watu wanaowakopesha kuwaibia kwa njia hii....

Wote tunafahamu kuwa shida haina adabu. Mtu ukiwa na shida inayohitaji fedha kutatuliwa, mara chache huwa hatukirii namna bora na salama ya kupata fedha hiyo. Njia yoyote inayokuja mbele yako inaweza kuwa sawa tu kwa wakati huo, madhara baadae...

Na kwa sababu hiyo ndiyo maana watu tunajikuta tumejiingiza kwenye madeni ya hatari kutoka kwa hawa jamaa na namna ya kujichomoa huko inakuwa ngumu kwelikweli....

Na mtu hugundua kuwa nilifanya maamuzi yasiyo sahihi huku akiwa tayari anaogelea kwenye madhara ya maamuzi yake yanayomuathiri yeye binafsi, kazi na familia ya wote wanaomtegemea....

Na hawa jamaa (Shylocks) wamefanya mambo yafuatayo kuvuta ndege wengi wajinase wenyewe.......;

1. Kwanza ukienda, wao wanazo keshi hapo hapo ofisini kwao. Huhitaji mzunguko wala mchakato kama ule wa kibenki amabao huchukua hadi wiki kupata fedha yako...m

2. Hawana mlolongo sijui usainishe fomu kwa mwajiri wako, ama serikali ya mtaa ama mahakamani nk nk

3. Wao fomu zao walishakula "deal" tayari na viongozi hawa na wana wanasheria wao na pengine mahakimu kabisa wa mahakama za chini ambao wote hawa wana fungu lao katika wizi na hujuma hii dhidi ya raia hawa masikiñi wa kipato na akili na upande mwingine Serikali kukosa mapato

4. Kinachotakiwa ni mteja kuwa na vitu viwili ama vitatu tu;
å Valid kadi ya benki unakopitia mshahara wako
å Bank statement ya unakopitia mshahara wako kuithibitisha hiyo akaunti yako

å Copy ya kitambulisho chako cha kazi

Ukiwa na hivi vitu utajaza fomu yao hapo hapo fast fast na kupewa fedha yako CASH hapo hapo. Kama utaenda baa kunywa, unaenda. Kama una akili utazielekeza kwenye kusudi la kukopa....

KWA HIYO;

å Ni kweli kabisa riba (accumulated interest) yao ni kubwa kupita kiasi na ni kati ya 40% na 50%......

√• Mfano, unachukua Tsh. 1,000,000 kwa muda wa miezi 6 na kama interest ni 50% , maana yake utarejesha Tshs. 1,500,000 ÷ 6 = 250,000 kila mwezi...!!

5. Sharti moja ni kuwa WEWE MTEJA HAWAKuRUHUSU UENDE AMA KUKUPA NAKALA YA MKATABA ULIOJAZA...!!

Hivi ndivyo biashara hii nono inavyofanyika...

Hata hivyo wakopeshaji wengi wameshaingia kwenye mgogoro na baadhi ya wateja wao (wajanja na wenye akili) waliowakopesha baada kuigundua janja hii na kugoma kulipa....

Nimeishudia kesi hii mwenyewe ikimhusu mtumishi wa umma (idara kapuni) na mkopeshaji (jina kapuni) ktk wilaya ya Shinyanga...

Kilichofanyika, ndugu huyu alienda akakopa Tshs 1,000,000 kwa riba ya 40% kwa marejesho ya miezi 5 sawa na Tshs 1,400,000 ÷ 5 = 280,000....

Ndugu huyu akafanya rejesho moja tu.....

Miezi iliyofuata na kwa kuwa kadi ya benki aliacha kwa mkopeshaji kama dhamana, alichofanya ni kwenda benki na kui - block kadi hiyo na akapewa kadi mpya.....

Mkopeshaji kila alivyoenda benki kuchukua chake, akawa hana access, kupata fedha, Card blocked....!

Baada ya muda fulani wakamfungulia kesi ya madai huyu ndugu. Kosa moja wakafanya hawa jamaa. Wakatumia kanuni na ujanja janja wao wa kimahesabu na kuliongeza deni hadi ikazidi principal amount aliyokopa huyu ndugu mara mbili....!

Alikuwa anadaiwa 1,120,000, sasa deni ni karibu 3,500,000+....!!

Kesi iliunguruma kwa kama miezi miwili hivi. Amini usiamini, mkopaji alishinda na kuamuliwa na mahakama alipe hela ileile aliyokopa....

Hapa tatizo hili kweli lipo na haliwahusu walimu ama manesi tu bali ni watumishi wote kada ya umma ama binafsi na hata watu wa kawaida tu wenye shughuli/biashara zao binafsi ili mradi wanakopesheka na wana dhamana fulani....

TUKUMBUKE PIA KUWA;

å Kisheria mtu mwingine kukaa na kadi ya benki ya mtu mwingine ni kosa....

å Vivyo hivyo katika Sera ya fedha na mikopo za taasisi za fedha hakuna riba ya kiwango cha 40%+....

å Kwa tafsiri ya haraka na ya wazi ni kuwa, wanachofanya hao Mashailoki ni WIZI kwa wateja wao na ni WIZI wa mapato ya serikali....!!

Narudia tena KUKOPA na KUKOPESHANA wala siyo tatizo na siyo dhambi....

Tatizo linakuja NIA na DHAMIRA za pande zote mbili (mkopaji & mkopeshaji) ni nini....

ALL in ALL, biashara hii ni nzuri sana lakini it's totally illegal....

Maana kama una mtaji wa 10,000,000 tu na ukawa na wateja 100 tu na unawakopesha kwa staili hii na wote wakawa wanakurejeshea bila shida.....

Kwa kweli ndani ya muda mfupi sana wewe unakuwa milionea...!!

Tatizo ni WIZI...
Ubarikiwe sana. Umenipa elimu kubwa sana, itanisaidia jamaa yangu alikopa shilingi milioni 4 kila mwezi tiba ni 670,000/= mwisho atapaswa alipe principal ya milioni 4. Kwa vile katikati ya muda wa marejesho, kapagawa kwa vile malipo wanataka alipe milioni 4 jumlisha rejesho miezi 10 ni 6,700,000/= na faini ya kuchelewa kulipa rejesho ni laki 4 kwa mwezi ujumla yake milioni 4. Hivyo jumla kuu hadi Februari 2020 ni shilingi 14,700,000/=; kinachoendelea sasa ni kuzungushana tu, wapo kwenye mgogoro
 
Unakuta mtu kadakwa na hao jamaa halafu upande mwingine anapokea vitisho vya BRANCH!!!
 
Kalipe deni acha kelele
Kama mkopeshaji umiza mmoja anakuwa na kadi 600 za watumishi je itakuwa kosa kusema 80% ya kadi za watumishi wa umma Tanzania zipo kwa wakopeshaji umiza?
 
Mimi nadhani tatizo hapa siyo MTU KUKOPA ama KUKOPESHA ama KUKOPESHANA watu.....

Tatizo lililopo ni wakopeshaji ambao kwa kweli wengi wao wako kisheria na wamesajiliwa na BoT chini ya sheria ya "Micro finance services " kukiuka masharti yayowaongoza kufanya kazi zao....

Hivi vitaasisi vya fedha vidogo vidogo vya kukopesha vikifuata utaratibu ulioko kisheria, hawataweza kuhimili kuwepo sokoni kwa sbb wateja wengi wako absorbed na mabenki ambazo zinafanya jukumu hili kwa uwazi zaidi na kwa riba ndogo zaidi....

Wanachofanya hawa Mashailoki ni kutumia shida na "ujinga" wa watu wanaowakopesha kuwaibia kwa njia hii....

Wote tunafahamu kuwa shida haina adabu. Mtu ukiwa na shida inayohitaji fedha kutatuliwa, mara chache huwa hatukirii namna bora na salama ya kupata fedha hiyo. Njia yoyote inayokuja mbele yako inaweza kuwa sawa tu kwa wakati huo, madhara baadae...

Na kwa sababu hiyo ndiyo maana watu tunajikuta tumejiingiza kwenye madeni ya hatari kutoka kwa hawa jamaa na namna ya kujichomoa huko inakuwa ngumu kwelikweli....

Na mtu hugundua kuwa nilifanya maamuzi yasiyo sahihi huku akiwa tayari anaogelea kwenye madhara ya maamuzi yake yanayomuathiri yeye binafsi, kazi na familia ya wote wanaomtegemea....

Na hawa jamaa (Shylocks) wamefanya mambo yafuatayo kuvuta ndege wengi wajinase wenyewe.......;

1. Kwanza ukienda, wao wanazo keshi hapo hapo ofisini kwao. Huhitaji mzunguko wala mchakato kama ule wa kibenki amabao huchukua hadi wiki kupata fedha yako...m

2. Hawana mlolongo sijui usainishe fomu kwa mwajiri wako, ama serikali ya mtaa ama mahakamani nk nk

3. Wao fomu zao walishakula "deal" tayari na viongozi hawa na wana wanasheria wao na pengine mahakimu kabisa wa mahakama za chini ambao wote hawa wana fungu lao katika wizi na hujuma hii dhidi ya raia hawa masikiñi wa kipato na akili na upande mwingine Serikali kukosa mapato

4. Kinachotakiwa ni mteja kuwa na vitu viwili ama vitatu tu;
å Valid kadi ya benki unakopitia mshahara wako
å Bank statement ya unakopitia mshahara wako kuithibitisha hiyo akaunti yako

å Copy ya kitambulisho chako cha kazi

Ukiwa na hivi vitu utajaza fomu yao hapo hapo fast fast na kupewa fedha yako CASH hapo hapo. Kama utaenda baa kunywa, unaenda. Kama una akili utazielekeza kwenye kusudi la kukopa....

KWA HIYO;

å Ni kweli kabisa riba (accumulated interest) yao ni kubwa kupita kiasi na ni kati ya 40% na 50%......

√• Mfano, unachukua Tsh. 1,000,000 kwa muda wa miezi 6 na kama interest ni 50% , maana yake utarejesha Tshs. 1,500,000 ÷ 6 = 250,000 kila mwezi...!!

5. Sharti moja ni kuwa WEWE MTEJA HAWAKuRUHUSU UENDE AMA KUKUPA NAKALA YA MKATABA ULIOJAZA...!!

Hivi ndivyo biashara hii nono inavyofanyika...

Hata hivyo wakopeshaji wengi wameshaingia kwenye mgogoro na baadhi ya wateja wao (wajanja na wenye akili) waliowakopesha baada kuigundua janja hii na kugoma kulipa....

Nimeishudia kesi hii mwenyewe ikimhusu mtumishi wa umma (idara kapuni) na mkopeshaji (jina kapuni) ktk wilaya ya Shinyanga...

Kilichofanyika, ndugu huyu alienda akakopa Tshs 1,000,000 kwa riba ya 40% kwa marejesho ya miezi 5 sawa na Tshs 1,400,000 ÷ 5 = 280,000....

Ndugu huyu akafanya rejesho moja tu.....

Miezi iliyofuata na kwa kuwa kadi ya benki aliacha kwa mkopeshaji kama dhamana, alichofanya ni kwenda benki na kui - block kadi hiyo na akapewa kadi mpya.....

Mkopeshaji kila alivyoenda benki kuchukua chake, akawa hana access, kupata fedha, Card blocked....!

Baada ya muda fulani wakamfungulia kesi ya madai huyu ndugu. Kosa moja wakafanya hawa jamaa. Wakatumia kanuni na ujanja janja wao wa kimahesabu na kuliongeza deni hadi ikazidi principal amount aliyokopa huyu ndugu mara mbili....!

Alikuwa anadaiwa 1,120,000, sasa deni ni karibu 3,500,000+....!!

Kesi iliunguruma kwa kama miezi miwili hivi. Amini usiamini, mkopaji alishinda na kuamuliwa na mahakama alipe hela ileile aliyokopa....

Hapa tatizo hili kweli lipo na haliwahusu walimu ama manesi tu bali ni watumishi wote kada ya umma ama binafsi na hata watu wa kawaida tu wenye shughuli/biashara zao binafsi ili mradi wanakopesheka na wana dhamana fulani....

TUKUMBUKE PIA KUWA;

å Kisheria mtu mwingine kukaa na kadi ya benki ya mtu mwingine ni kosa....

å Vivyo hivyo katika Sera ya fedha na mikopo za taasisi za fedha hakuna riba ya kiwango cha 40%+....

å Kwa tafsiri ya haraka na ya wazi ni kuwa, wanachofanya hao Mashailoki ni WIZI kwa wateja wao na ni WIZI wa mapato ya serikali....!!

Narudia tena KUKOPA na KUKOPESHANA wala siyo tatizo na siyo dhambi....

Tatizo linakuja NIA na DHAMIRA za pande zote mbili (mkopaji & mkopeshaji) ni nini....

ALL in ALL, biashara hii ni nzuri sana lakini it's totally illegal....

Maana kama una mtaji wa 10,000,000 tu na ukawa na wateja 100 tu na unawakopesha kwa staili hii na wote wakawa wanakurejeshea bila shida.....

Kwa kweli ndani ya muda mfupi sana wewe unakuwa milionea...!!

Tatizo ni WIZI...
Mkuu umefafanua vizuri sana,Watu wanadhani watumishi wanapenda kujiingiza kwenye hizi shida.Mimi mara kadhaa nimewasikia wakuu wa wilaya wakiwashangaa na kuwalaumu watumishi wanaoacha kadi kwa wakopeshaji wa aina hii, mwenye shibe hamjali mwenye njaa .Mimi nina uhakika kabisa kuna hadi wakuu wa Idara wenye mishahara minono na marupurupu wamewahi kukopa .Shida inapokuja huo muda wa kusubiri mlolongo wa kuchakata namna ya kupata pesa bila kuumia haupo.Ingawa pia kuna watumishi wameingia kwenye shida hizi kwaajili ya starehe tu.Kuna wakuu wa wilaya walio wahi kuwa walimu nao walipita kwenye mfumo wa uachaji kadi kwa wakopeshaji hawa, lakini baada ya kuwa kwenye green pasture sasa wamekuwa wakiwakejeli wanaotatua matatizo yao kwa kuacha kadi ili wapate fedha kwa haraka.
 
Back
Top Bottom