The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Ubarikiwe sana. Umenipa elimu kubwa sana, itanisaidia jamaa yangu alikopa shilingi milioni 4 kila mwezi tiba ni 670,000/= mwisho atapaswa alipe principal ya milioni 4. Kwa vile katikati ya muda wa marejesho, kapagawa kwa vile malipo wanataka alipe milioni 4 jumlisha rejesho miezi 10 ni 6,700,000/= na faini ya kuchelewa kulipa rejesho ni laki 4 kwa mwezi ujumla yake milioni 4. Hivyo jumla kuu hadi Februari 2020 ni shilingi 14,700,000/=; kinachoendelea sasa ni kuzungushana tu, wapo kwenye mgogoro
Pole yake sana huyo ndugu....
Lakini tukumbuke kuwa dawa ya deni ni kulipa. Na kwa kweli kama alichukua pesa, basi sharti ailipe kwa mujibu wa makubaliano yao ya awali.....
Shida inakuja kwa aliyekopesha kutaka kumkomoa mteja wake na kwa kutumia hesabu ambazo hazijulikani ziko ulimwengu gani kulikuza deni kwa zaidi ya 250%.....
Haiwezekani mtu akope milioni 4 alipe milioni 14.7 hata kama deni lina umri Mkubwa kiasi gani....
USHAURI:
å Asimkimbie mkopeshaji wake. Na kamwe asiliogope deni. Vunginevyo litamharibia maisha yake kabisa. Muhimu ni kukubali kuwa alikopa fedha na ikasaidia kutatua shida yake ya kifedha wakati huo....
å Aende na wakae mezani na kujadili kwa pamoja ili aone namna ya kurejesha pesa ya mtu aliyemkopa pamoja na riba kidogo kulingana na muda aliyokaa nayo....
å kama katika milioni 4, si vibaya akarejesha hata milioni 5 kwa maana awape na milioni 1 ya ziada....
å Wasipoelewana, kesi iendelee mahakamani. Muhimu ni yeye kujenga hoja thabiti....
å Sema tu kuwa hawa jamaa huwa wana ujanja fulani ambao huutumia huutumia kumweka mdeni wao mahali wanapotaka awe kisheria ili iwe rahisi kwao kumwibia...
å Watakuita ofisini kwao. Wanakushawishi kuwa ukubali umekopa 14.7M huku ukweli ukiwa kuwa ulikopa ni Milioni 4 tu + accumulated interest ya 40% (mfano) ambapo kwa ujumla deni lote linakuwa 5,600,000...
å Kwa ushawishi wa hali ya juu, utaingia kingi. Hapo jamaa wanakuwa hata tayari kukupa pesa nyingine hata Milioni moja kabisa....!
Kukubali maana yake, utanasaini makaratasi yao.. Hilo linakuwa kosa lako na ndiyo watakapokunyongea hapo mkifika mahakamani....!
Na usipopata mwanasheria mahiri, utashindwa na utazilipa ama kutaifishiwa chochote chenye thamani hiyo iwe nyumba, gari nk....
√• Lakini kama màandishi watakayokwenda nayo mahakamani ni yale ya Sh. Milioni 4 + accumulated interest ya 40% ambayo ni sawa na Tshs. 5,600,000 basi uwezekano wa kushinda kesi ni Mkubwa na mahakama itaamuru ulipe 5.6M hiyo hiyo hata kama amekaa nayo miaka 10...!!