Wakopeshaji umiza kwa watumishi wa umma ni matokeo ya sera za CCM


Pole yake sana huyo ndugu....

Lakini tukumbuke kuwa dawa ya deni ni kulipa. Na kwa kweli kama alichukua pesa, basi sharti ailipe kwa mujibu wa makubaliano yao ya awali.....

Shida inakuja kwa aliyekopesha kutaka kumkomoa mteja wake na kwa kutumia hesabu ambazo hazijulikani ziko ulimwengu gani kulikuza deni kwa zaidi ya 250%.....

Haiwezekani mtu akope milioni 4 alipe milioni 14.7 hata kama deni lina umri Mkubwa kiasi gani....

USHAURI:

å Asimkimbie mkopeshaji wake. Na kamwe asiliogope deni. Vunginevyo litamharibia maisha yake kabisa. Muhimu ni kukubali kuwa alikopa fedha na ikasaidia kutatua shida yake ya kifedha wakati huo....

å Aende na wakae mezani na kujadili kwa pamoja ili aone namna ya kurejesha pesa ya mtu aliyemkopa pamoja na riba kidogo kulingana na muda aliyokaa nayo....

å kama katika milioni 4, si vibaya akarejesha hata milioni 5 kwa maana awape na milioni 1 ya ziada....

å Wasipoelewana, kesi iendelee mahakamani. Muhimu ni yeye kujenga hoja thabiti....

å Sema tu kuwa hawa jamaa huwa wana ujanja fulani ambao huutumia huutumia kumweka mdeni wao mahali wanapotaka awe kisheria ili iwe rahisi kwao kumwibia...

å Watakuita ofisini kwao. Wanakushawishi kuwa ukubali umekopa 14.7M huku ukweli ukiwa kuwa ulikopa ni Milioni 4 tu + accumulated interest ya 40% (mfano) ambapo kwa ujumla deni lote linakuwa 5,600,000...

å Kwa ushawishi wa hali ya juu, utaingia kingi. Hapo jamaa wanakuwa hata tayari kukupa pesa nyingine hata Milioni moja kabisa....!

Kukubali maana yake, utanasaini makaratasi yao.. Hilo linakuwa kosa lako na ndiyo watakapokunyongea hapo mkifika mahakamani....!

Na usipopata mwanasheria mahiri, utashindwa na utazilipa ama kutaifishiwa chochote chenye thamani hiyo iwe nyumba, gari nk....

√• Lakini kama màandishi watakayokwenda nayo mahakamani ni yale ya Sh. Milioni 4 + accumulated interest ya 40% ambayo ni sawa na Tshs. 5,600,000 basi uwezekano wa kushinda kesi ni Mkubwa na mahakama itaamuru ulipe 5.6M hiyo hiyo hata kama amekaa nayo miaka 10...!!
 
Kwa maelezo uliyoyatoa ni wazi kabisa kuwa wewe ni moja kati ya mashailock wanaotuumiza sisi watumishi.. Ila yote kwa yote Malipo ni hapahapa Duniani.
 
Kwa maelezo uliyoyatoa ni wazi kabisa kuwa wewe ni moja kati ya mashailock wanaotuumiza sisi watumishi.. Ila yote kwa yote Malipo ni hapahapa Duniani.

Hapana mimi siyo "Shylock" na sijawahi kopesha mtu kwa njia hii...

Isipokuwa mimi ni muathirika (victim) pia wa biashara ya watu hawa na kunipa uzoefu wa kutosha na nikajifunza sana juu ya mikopo.....
 
Hapana mimi siyo "Shylock" na sijawahi kopesha mtu kwa njia hii...

Isipokuwa mimi ni muathirika (victim) pia wa biashara ya watu hawa na kunipa uzoefu wa kutosha na nikajifunza sana juu ya mikopo.....
Ulichoandika ndo kinachotokea mtaani Mimi pia ni victim ambaye ninapambana kujitoa japo sijamaliza hata wiki toka nimetoka kukopa kwa hao watu.. Umeandika vitu on point kabisa mpaka nikawa nahisi wewe ndo uliyenikopesha.
 
Ulichoandika ndo kinachotokea mtaani Mimi pia ni victim ambaye ninapambana kujitoa japo sijamaliza hata wiki toka nimetoka kukopa kwa hao watu.. Umeandika vitu on point kabisa mpaka nikawa nahisi wewe ndo uliyenikopesha.
Wewe ni mwalimu? Hii tabia niliikua naiona sana Kasulu, Kigoma
 
aisee . . . naomba nikuambie kitu mzee. Sio watumishi wote wanapenda maisha hayo. Kipato kisipokidhi mahitaji ndio huko wengi wanapoangukia. Ila pia masharti mengine ni uchuro kabisa. Eti nikupe ATM card yangu, hivi unaijua hela wewe ?
 
Kweli hao wakopeahaji nimewaahuhudia sana mkoa wa MARA.
 
Mkuu nazidi kuishabikia na kukubali JF ni bahari ya maarifa; nashukuru sana na msaada wa mawazo hivyo nitamshauri ndugu yangu kwa kifua aende kuonana na jamaa wakae mezani kwa majadiliano namna ya kumalizana kwa faida ya pande zote mbili
 
Serikali inapaswa kulitafutia ufumbuzi wa kudumu hili swala.Tatizo no kwamba swala hili linatumika kutafuta sifa za kisiasa.Baadhi ya wakuu was mikoa wanalitumia pia kujipatia sifa binafsi kwa kuanika wahusika kwenye makamera waonekane kweli wanafanya kazi.Luna wafanyakazi ufanisi wao kazini umeshuka kwa. Hofu ya kutafutwa na hawa wakopeshaji, wengine wameugua hadi maradhi ya moyo.Kinachofanyika taasisi za kitapeli zimewashika wakurugenzi na maafisa utumishi yani fomu ya mkopo inapelekwa asubui mchana unaingiziwa hela yako.Upande was pili zile benki kubwa hazitoi rushwa kwa maafisa utumishi wala wakurugenzi yaani mfanyakazi unapeleka fomu yako inakaa kwenye failing hadi wiki nne afisa utumishi hataki kusaini kwa sababu hujampa chochote.Wale matapeli kama Bayport, platnam na faidika hela utaipata Siku hiyohiyo wana mtandao had I hazina kote huko wametoa hela.Sijui kwa nini inawalea hawa watu yani riba zao ni kubwa mno hata ukitaka kuwalipa ujitoe hawakubali au watakubambikia deni kubwa mpaka uchanganyikiwe.Tatizo serikali haijaamua kumaliza huu utapeli
 
Sio makaratasi tu na ATM card Yangu.
Daaah aisee kwaio unaweza kuta baada ya miezi 6 deni linaisha unafika unakuta unadaiwa milioni 9 zingine wameshachakachua form za mikopo etc..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…