Wakristo kazi mnayo aisee...

Wakristo kazi mnayo aisee...

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Mkristo ni barua ni lazima asomeke vizuri, aandikwe kwa mwandiko mzuri.

Mkristo ni chumvi ya ulimwengu, lazima atie ladha dunia ili dunia iwe mahali pazuri na salama kwa kuishi binadamu, wanyama, samaki, mimea na mazingira kwa ujumla.

Mkristo ni chombo cha haki, tetea haki inapodhulumia, tetea wanyonge na wanaoonewa. Haki za mashoga sio haki, hamna haki ya kutenda dhambi. Ushoga ni kama tu uuaji.

Mkristo ni chombo cha amani, hakikisha kwamba wewe ni mlinzi wa amani, sio unakuwa ndio mkorofi, mgomvi, mtukanaji na kila tabia mbaya ni yako.

Mkristo ni Wakili/ Mwakilishi wa Yesu Kristo. Hapa duniani hujaja kuzubaa, hapa unekuja kumwakilisha Yesu Kristo. Kumhubiri Kristo siyo lazima ushike microphone 🎤, matendo yako yanahubiri zaidi kuliko sauti. Wasaidie wahitaji, tembelea wagonjwa, wafariji wafiwa, hudumia jamii yako kikamilifu, tunza mazingira, hakikisha uko unique mpaka kila mtu atamani kuwa kama wewe. Sio ikitokea ajali wewe ndio unaenda kuwanyonga marehemu ili uwaibie simu zao.

Ndugu zangu Wakristo je tunasomekaje? Au sisi ndio wachawi namba moja kwenye mitaa tunayoishi?

Au sisi ndio kina Kaka Jambazi wenyewe? Tunavunja, tunaua, na kufanya kila ubaya?

Mathayo 6:33
[33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

But seek ye first the kingdom of God, and his righteousness; and all these things shall be added unto you.
 
Ukristo na CCM ni vitu viwili tofauti kwa jinsi nilivyosoma Mkristo anavyotakiwa awe.

CCM imejaa dhuluma, wenye haki hawapati nafasi sababu tu hawana hela ya kuhonga wajumbe, hawana makundi, nk.

CCM imejaa wanafiki, waongo, wazandiki, wenye husuda, wachawi, walafi na wasio na utu.
 
🤣🤪😅😂😆 akusikie johnthebaptist
 
"I love christianity but I hate christians" ..........Hatam Ghadhi
Ukristo ni mzuri sana, tatizo ni sisi Wakristo. Mkristo anadanga. Mkristo unaanzaje kuwa shoga? Mkristo tapeli, huaminiki, hata ukiagizwa buku tu ununue vocha unaila. Yaani hauko credible hata kidogo. Tusijitafutie laana kwa mambo ya kijinga
 
Ukristo na CCM ni vitu viwili tofauti kwa jinsi nilivyosoma Mkristo anavyotakiwa awe.
CCM imejaa dhuluma, wenye haki hawapati nafasi sababu tu hawana hela ya kuhonga wajumbe, hawana makundi, nk.

CCM imejaa wanafiki, waongo, wazandiki, wenye husuda, wachawi, walafi na wasio na utu.
Noma sana jambaa, you nailed it
 
Ukristo ni mzuri sana, tatizo ni sisi Wakristo. Mkristo anadanga. Mkristo unaanzaje kuwa shoga? Mkristo tapeli, huaminiki, hata ukiagizwa buku tu ununue vocha unaila. Yaani hauko credible hata kidogo. Tusijitafutie laana kwa mambo ya kijinga
Kilicho ua ukristo ni kutotenganisha capitalism na ukristo, pope ni mfanya biashara mkubwa anafanya deal za umafia nyingi
 
Juzi alikuwa na kikao cha dakika 45 na Mkurugenzi wa shirika la Jesuit wakiujadili ushoga. Tutege sikio tusikie mtikisiko mkubwa unaokuja
Kupenda pesa ndio chanzo cha uovu wote. (Pesa sio chanzo cha uovu, ila kuzipenda pesa ndio chanzo cha uovu)
Kilicho ua ukristo ni kutotenganisha capitalism na ukristo, pope ni mfanya biashara mkubwa anafanya deal za umafia nyingi
 
Wanadamu ni vyombo mikononi mwa Mungu, wanaotumiwa na Yeye kutimiza
Makusudi yake ya neema na rehema. Kila mmoja ana sehemu yake ya kutenda;kwa kuwa kila mmoja amepewa kiasi cha nuru(maarifa kutoka katika maandiko), itumikayo kulingana na mahitaji ya wakati wake na yenye kumtosha ili aweze kufanya kazi ambayo Mungu ametoa yeye kufanya.- E. G White.
 
Back
Top Bottom