Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
- Thread starter
- #21
Homa ya Dunia by Solo ThangDunia ilivyovurugana ni balaa
Bila upevu wa fikra kung’amua hii homa ni ndoto
Madaktari, waganga wote chamtoto
Bado wanaitafuta pimajoto, kwani dunia ina homa kali mithili ya moto
Wanasayansi wamelala maabara, Wanaitafuta tiba
Kwani homa ya dunia ishaleta madhara,
Hakuna masihara, vipofu wamesikia, homa ya dunia, viziwi bado wanalia
Mabubu wanataka kusimulia.
Dunia ni sawa na meli inayozama polepole,
Nani ataziba tundu hakuna kidole.
-CHORUS-
Machozi yanatoka ishara homa ya dunia,
Binadamu, wanyama, ndege wote mbona mnali?
Parapanda italia, mito milima, mabonde vyote vitaangamia
Madaktari waganga ujuzi washautumia
Wamemzunguka mgonjwa homa ya dunia
Waumini wamemsalia na bado mikononi akawafia.
-Verse 2-
Zifuatazo dalili, dunia imeishiwa nguvu za asili, Ona inatetemeka
Kusema kweli imeshazeeka
Maji yamenyauka na ardhi imepasuka
Binadamu, kama muuguzi amedhoofika,
Kiakili, kiroho hata kimwili
Kemikali, zitupwazo ndani ya bahari
Moshi mzito wa sumu unaotanda juu ya sayari
Na mrundiko wa dhambi za binadamu
Vinazidisha homa kali
Tamaa kali, za kutaka kuonja kila kitu
Zinamaanisha akili siyo maarifa ya mtu
Huyu mgonjwa kupona, ah! Thubutu
Dunia imewekwa najisi na watu wanayoikalia
Wameziasi sharia na siku inakaribia
Binadamu wote watalia na haitasaidia
Inakuja siku ya ghadhabu, Siku ambayo….
Binadamu wote watafunzwa adabu, Siku ambayo….
Hakuna swali bila jawabu
(Machozi yanatoka ishara homa ya dunia,
Binadamu, wanyama, ndege wote mbona mnali?
(Rudia Chorus)
-VERSE 3-
Ilivyochoka dunia sawa na tambarabovu
Binadamu wanawindana kwa wavu
Ama kweli mtoto wa moto majivu
Umetoweka usikivu, dhambi kama kamchezo
Binadamu kaibeba dunia pasipo uwezo
Na wengi wameponzwa na dezo
Wasichana wamesagana
Wavulana wameoana
Kama mimi ndiyo macho sitaki hata kuona
Binadamu hana nidhamu
Kama ipo basi ya uoga
Wananuka uovu kama mizoga
Wanapaka marashi ili wanukie swafi
Bora ifike tamati.
Magereza mengi vibaka hawashtuki
Magonjwa mengi wagoni hatuelimiki
Na kama binadamu angejua, angeukataa ufanisi finyu wa pua
Robo unavuta hewa, robotatu bangi tumbaku
Hizi akili timamu za binadamu siyo za chatu
Mdomo mfereji unapita vinywaji haramu
Watu wanakunywa damu
Huu uchambuzi wangu ni walii, mboni zangu zina mabaki ya kinabii.