Wakristo kazi mnayo aisee...

Wakristo kazi mnayo aisee...

Dunia ilivyovurugana ni balaa
Homa ya Dunia by Solo Thang

Bila upevu wa fikra kung’amua hii homa ni ndoto
Madaktari, waganga wote chamtoto
Bado wanaitafuta pimajoto, kwani dunia ina homa kali mithili ya moto
Wanasayansi wamelala maabara, Wanaitafuta tiba
Kwani homa ya dunia ishaleta madhara,
Hakuna masihara, vipofu wamesikia, homa ya dunia, viziwi bado wanalia
Mabubu wanataka kusimulia.

Dunia ni sawa na meli inayozama polepole,
Nani ataziba tundu hakuna kidole.

-CHORUS-

Machozi yanatoka ishara homa ya dunia,
Binadamu, wanyama, ndege wote mbona mnali?
Parapanda italia, mito milima, mabonde vyote vitaangamia
Madaktari waganga ujuzi washautumia
Wamemzunguka mgonjwa homa ya dunia
Waumini wamemsalia na bado mikononi akawafia.

-Verse 2-

Zifuatazo dalili, dunia imeishiwa nguvu za asili, Ona inatetemeka
Kusema kweli imeshazeeka
Maji yamenyauka na ardhi imepasuka
Binadamu, kama muuguzi amedhoofika,
Kiakili, kiroho hata kimwili
Kemikali, zitupwazo ndani ya bahari
Moshi mzito wa sumu unaotanda juu ya sayari
Na mrundiko wa dhambi za binadamu
Vinazidisha homa kali
Tamaa kali, za kutaka kuonja kila kitu
Zinamaanisha akili siyo maarifa ya mtu
Huyu mgonjwa kupona, ah! Thubutu
Dunia imewekwa najisi na watu wanayoikalia
Wameziasi sharia na siku inakaribia
Binadamu wote watalia na haitasaidia
Inakuja siku ya ghadhabu, Siku ambayo….
Binadamu wote watafunzwa adabu, Siku ambayo….
Hakuna swali bila jawabu

(Machozi yanatoka ishara homa ya dunia,
Binadamu, wanyama, ndege wote mbona mnali?

(Rudia Chorus)

-VERSE 3-

Ilivyochoka dunia sawa na tambarabovu
Binadamu wanawindana kwa wavu
Ama kweli mtoto wa moto majivu
Umetoweka usikivu, dhambi kama kamchezo
Binadamu kaibeba dunia pasipo uwezo
Na wengi wameponzwa na dezo
Wasichana wamesagana
Wavulana wameoana
Kama mimi ndiyo macho sitaki hata kuona
Binadamu hana nidhamu
Kama ipo basi ya uoga
Wananuka uovu kama mizoga
Wanapaka marashi ili wanukie swafi
Bora ifike tamati.

Magereza mengi vibaka hawashtuki
Magonjwa mengi wagoni hatuelimiki
Na kama binadamu angejua, angeukataa ufanisi finyu wa pua
Robo unavuta hewa, robotatu bangi tumbaku
Hizi akili timamu za binadamu siyo za chatu
Mdomo mfereji unapita vinywaji haramu
Watu wanakunywa damu
Huu uchambuzi wangu ni walii, mboni zangu zina mabaki ya kinabii.
 
Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
 
Warumi 14: 7 “Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake.

8 Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.

9 Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.”

Yesu Kristo pekee ndiye aliyepewa mamlaka yote ya vitu vya mbinguni na vya duniani..utasema mbona biblia inasema “shetani ndiye mungu wa ulimwengu huu”…Ndio! Shetani ni mungu wa ulimwengu huu, kwa ruksa maalumu..Amepewa mamlaka atawale kwa kitambo tu, na mamlaka hayo kapokea kutoka kwa Yesu Kristo, …lakini itafika wakati leseni yake itaisha muda..atafungwa kwa miaka 1000, kupisha utawala wa Amani wa Bwana wetu YESU KRISTO kufanya kazi hapa duniani, na baadaye atafunguliwa kidogo ili kutimiza kusudi fulani na kisha atatupwa katika lile ziwa la moto. Hivyo tunaposema anamaliki sasa ulimwengu haimaanishi anafanya lolote kwa kujiamulia hapana! Anayo mipaka akitaka kufanya jambo lazima apate kibali kutoka juu kama alivyokwenda kufanya kwa Ayubu..

Kwahiyo unaweza ukauona ukuu alionao Bwana wetu Yesu Kristo sasa…kwamba vitu vyote sasa vipo chini ya himaya yake..kakabidhiwa kila kitu, yaaani tunaposema kila kitu maana yake hakuna kilichosalia…hata wanyama wa porini, hata mimea, hata waovu, hata yule mbwa au paka, au bundi au yule fisi unayemwona kule porini, hata kuzimu na malaika wote…vyote kwasasa vipo chini yake (anavimiliki) ana uwezo wa kufanya chochote atakacho juu yao. Nimependa kulizungumza hili kwasababu wapo wachache ambao bado hawajapata Neema ya kulielewa hili kwa undani..yaani mamlaka Yesu Kristo aliyonayo sio ya kimlinganisha na kitu kingine chochote.

Alisema katika Mathayo 28: 18 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani”.

Lakini leo kwa Neema za Bwana..hatutaingia sana huko, bali tutajifunza juu ya MSHAHARA WA DHAMBI.

Siku moja nilikuwa napita mahali Fulani mahali walipokuwa wanauza mahindi karibu na mashine ya kusaga..sasa pembezoni mwa mtaro nikaona baadhi ya punje za mahindi zimeanguka na nyingine zilikuwa zimeshaanza kumea. Nikajiuliza kwa nini zile mbegu zimeota pale na wakati hakuna mtu aliyekusudia kuzipanda pale? Wakati natafakari hilo kitu kikaingia ndani mwangu na nijikuta ninasema…”hakika apandacho mtu ndicho atakachovuna kama watu wanavyosema”…haijalishi hiyo mbegu ilipandwa kwa makusudi au kwa bahati mbaya, kwa kujua au kwa kutokujua lakini mwisho wa siku kile kilichopandwa kitamea tu..

Wengi wetu tunafikiri mkulima ni Yule tu aliyetoka na mbegu zake nyumbani na kwenda kuzipanda shambani..lakini ni zaidi ya hapo, mkulima ni hata Yule aliyeangusha mbegu njiani pasipo yeye kujijua na ikamea…Naye pia anastahili kupata malipo ya kazi yake..Ni majibu ya Mungu kwa kile alichokipanda…hata kama alikuwa hajui..Mungu ameshamjibu! Ndio maana ile mbegu ikamea hata kama alikuwa hajui.

Hali Kadhalika na sisi katika maisha yetu..Yapo mambo mengi tunayapanda ambayo aidha kwa kujua au kwa kutokujua..hiyo haizuii chochote ni lazima yalete majibu. Ukipanda mbegu njema utavuna mema…na ukipanda mbegu mbaya utavuna hizo hizo..

Ukitenda dhambi kwa kutokujua kuwa umetenda dhambi au ukitenda dhambi kwa kujua…zote mbili zinaleta matokeo yanayofanana…na matokeo yenyewe ni mauti…kwasababu biblia inasema mshahara wa dhambi ni mauti. Ni sawa na mtu aliyepanda mbegu yake shambani na mwingine aliiangusha pasipo kujua mtaroni na kuendelea na shughuli zake…wote wawili mbegu zao zitamea tofauti ni kwamba mmoja atakuwa anaona na kufuatilia hatua za ukuaji, mwingine atakuwa haoni wala hafahamu kuwa alichokipanda kinaendelea kuota huko…lakini utakapofika msimu wa mavuno, mavuno yote yatakomaa kwa wakati mmoja.

Kama wewe ni mwasherati, na unajua kabisa uasherati ni dhambi, au ni mlevi, au mtazamaji pornography, au mwizi, au mlawiti, au mfanyaji masturbation, au msagaji, au mtoaji mimba, au msengenyaji..na unafanya hayo kwa makusudi kabisa..kuwa na uhakika kabisa mbegu hizo Mwisho wa siku mbegu hizo zitakuzalia mauti..

Halikadhalika kama mwingine ni mwizi, au muasherati, au mfanyaji masturbation, au mtukanaji au mlevi, na hana habari kuwa mambo hayo ni mabaya na ni dhambi mbele za Mungu..huyo naye ni sawa na mtu aliyeiangusha mbegu yake kwenye mtaroni kando ya barabara pasipo kujijua..ambapo itamea na wakati ukifika kazi yake itaonekana na watu wote hata kama yeye hajui..Hivyo na yeye pia mbegu zake zitamzalia MAUTI!! Atakufa katika roho na katika mwili.

Mfano leo hii ukienda kubaka mwanafunzi, serikali haitaki kujua kuwa ulikuwa unaifahamu sheria au la, hiyo si kazi yao…Kazi yao ni moja tu kukuhukumu kulingana na sheria inavyosema ,utakwenda gerezani miaka 30.
 
Wakristo wabongo wako busy na mambo yafuatayo;
1. kushindana na Qur'an (hata kama hawaifahamu)
2. kukashfu Waislamu,
3. kuchukia waarabu kwa kuwanasibisha na kila baya wanalolifahamu au kulisikia dunia hii,
4. Kuupigania ushoga kwa vile umeshamiri na unaendelea kushamiri kwa wazungu (wanaamini ni wakristo wenzao). Katika kuwapoteza maboya watu hapa, hutumia nguvu nyingiiii kuwaaminisha (dhambi ya kusingizia) watu kuwa ulawiti hufanywa sana na waarabu na watu wa pwani.
5. Kutenda ushirikina eg Mbeya, Iringa n.k ingawa wanatumia nguvu kuubwaa kujaribu kuwaaminisha watu kuwa ushirikina upo pwani na sio kwao.

Umefanya vizuri kuwakumbusha!
 
mama D na johnthebaptist watang'aka[emoji16]
Ukristo na CCM ni vitu viwili tofauti kwa jinsi nilivyosoma Mkristo anavyotakiwa awe.
CCM imejaa dhuluma, wenye haki hawapati nafasi sababu tu hawana hela ya kuhonga wajumbe, hawana makundi, nk.

CCM imejaa wanafiki, waongo, wazandiki, wenye husuda, wachawi, walafi na wasio na utu.
 
Wakristo wabongo wako busy na mambo yafuatayo;
1. kushindana na Qur'an (hata kama hawaifahamu)
2. kukashfu Waislamu,
3. kuchukia waarabu kwa kuwanasibisha na kila baya wanalolifahamu au kulisikia dunia hii,
4. Kuupigania ushoga kwa vile umeshamiri na unaendelea kushamiri kwa wazungu (wanaamini ni wakristo wenzao). Katika kuwapoteza maboya watu hapa, hutumia nguvu nyingiiii kuwaaminisha (dhambi ya kusingizia) watu kuwa ulawiti hufanywa sana na waarabu na watu wa pwani.
5. Kutenda ushirikina eg mbeya, iringa n.k ingawa wanatumia nguvu kuubwaa kujaribu kuwaaminisha watu kuwa ushirikina upo pwani na sio kwao.

Umefanya vizuri kuwakumbusha!
Sio kweli,
 
Mkristo ni barua ni lazima asomeke vizuri, aandikwe kwa mwandiko mzuri.
Mkristo ni chumvi ya ulimwengu, lazima atie ladha dunia ili dunia iwe mahali pazuri na salama kwa kuishi binadamu, wanyama, samaki, mimea na mazingira kwa ujuml...

1 Timotheo 6:10
Kwa maana kupenda sana fedha ni chanzo cha uovu wote. Watu wengine wametamani sana kupata fedha hata wakatangatanga mbali na imani, na wameivunja mioyo yao kwa huzuni nyingi.
 
Wakristo wabongo wako busy na mambo yafuatayo;
1. kushindana na Qur'an (hata kama hawaifahamu)
2. kukashfu Waislamu,
3. kuchukia waarabu kwa kuwanasibisha na kila baya wanalolifahamu au kulisikia dunia hii,
4. Kuupigania ushoga kwa vile umeshamiri na unaendelea kushamiri kwa wazungu (wanaamini ni wakristo wenzao). Katika kuwapoteza maboya watu hapa, hutumia nguvu nyingiiii kuwaaminisha (dhambi ya kusingizia) watu kuwa ulawiti hufanywa sana na waarabu na watu wa pwani.
5. Kutenda ushirikina eg mbeya, iringa n.k ingawa wanatumia nguvu kuubwaa kujaribu kuwaaminisha watu kuwa ushirikina upo pwani na sio kwao.

Umefanya vizuri kuwakumbusha!
 
Wakristo wabongo wako busy na mambo yafuatayo;
1. kushindana na Qur'an (hata kama hawaifahamu)
2. kukashfu Waislamu,
3. kuchukia waarabu kwa kuwanasibisha na kila baya wanalolifahamu au kulisikia dunia hii,
4. Kuupigania ushoga kwa vile umeshamiri na unaendelea kushamiri kwa wazungu (wanaamini ni wakristo wenzao). Katika kuwapoteza maboya watu hapa, hutumia nguvu nyingiiii kuwaaminisha (dhambi ya kusingizia) watu kuwa ulawiti hufanywa sana na waarabu na watu wa pwani.
5. Kutenda ushirikina eg mbeya, iringa n.k ingawa wanatumia nguvu kuubwaa kujaribu kuwaaminisha watu kuwa ushirikina upo pwani na sio kwao.

Umefanya vizuri kuwakumbusha!

na kuhodhi viwanja vikubwa kila sehemu ya nchi kwa kusaidiwa na mwendazake nyerere na kuchukua nyumba za waislamu na kuzifanya NHC
 
unaweza kuthibitidha bila shaka?
Wewe mshamba kabisa wewe ndo ujui kwamba uchumi wa vetecan unamilikiwa na pope au Air Italian share 70 ni za pope, pumbavu kibisa mnajificha uko vijijini amjui world economy
 
Back
Top Bottom