Kuna nguvu kubwa katika uamsho/ wokovu usipokuwa makini utashindwa kubalance mambo ya mwilini na rohoni.
Ni hivi, ukishaokoka unakuwa unaongozwa na Roho Mtakatifu, hapo mwili unakuwa kama umelala Sasa unaongozwa na Roho...
Sijui niwekeje muelewe, yaani yule Donatila wa ndani anakuwa active zaidi ya Donatila wa mwilini.
Ukiokoka haya mambo ya Dunia, unaona kawaida sana, hata ndoa, yawezekana unapenda tendo la ndoa ila ghafla kiu inapotea.
Yaani Kuna wakati unamuona mumeo kama kaka yako tu, sorry si kwa ubaya.
Najaribu kuwaelewesha maana nimepitia haya 2023, yaani hakuna aliyeweza kunielewa hata mume wangu.
Hitimisho:
Kuna umuhimu wa elimu ya Uamsho/ Wokovu kwa watu wote hasa waliooana yaani wanandoa. Kwakuwa Uamsho ukiingia ndani yako unabadili na kuathiri hali ya mwilini sana.
Ni muhimu kujifunza kubalance ili uweze kufanya vyote kwa pamoja.
Ikumbukwe Uamsho/ Wokovu unamaana kubwa katika kueneza injili ya Bwana Yesu.