NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Huwa nashangaa sana ni vipi kila kiumbe ambacho Mungu alituruhusu kula huwa kinalika bila tatizo na ni salama kwetu lakini linapokuja suala la viumbe ambavyo alivikataza huwa kuna ubaguzi, mfano viumbe kama nzi, nyau, punda, mjusi na panya watu wanabagua lakini kwa wakati huo huo wanakula vingine vilivyokatazwa kama nguruwe na nyau, ni kwanini ?
Wanyama safi na halali kuliwa ni wenye sifa hizi zote : kwato katika miguu yake + mwenye miguu ya kupasuka kati + mwenye kucheua,.... wanyama kama sungura, nguruwe na paka hawaruhusiwi
"Sifa za viumbe wengine"
Samaki walio halali kuliwa na watu ni lazima awe na mapezi + magamba
Ndege wote wanafaa kasoro tai, furukombe, kipungu, mwewe, kozi, kunguru, mbuni, kirukanjia, dudumizi, kipanga, bundi, mnandi, bundi, mumbi, mwari, mderi, korongo, koikoi, hudihudi, popo.
Wadudu halali kwetu ni wale wenye miguu mirefu maalum kwajili ya kuruka juu na chini kama panzi, senene na nzige
Reptiles wote hawafai : chura, nyoka, vinyonga, kenge, n.k.