Jamaa rafiki yangu ( 37 )ni single father with 3 kids ana mchumba wake mganda ambae nae ni single.mother ( 37 yrs) with one kid. Alikuwaga rafiki yake wakati wakisoma chuo wakaja kukutana tena miaka kadhaa baada ya ku graduate jamaa anaishi Dar mrembo anaishi kampala wakaanzisha uhusiano.
Muda wa kwenda kutoa mahari ulikuwa Mwezi uliopita.
Nilikuwa mmoja katika ujumbe ulio ongozana na rafiki yangu na matchmaker ( mshenga) wake .
Wakati wa kunegotiate mahari
Wazazi wakaanza na 15 million Ugandan ambayo ni kama milioni 9 ya Tanzania. ( Walitaja idadi ya ng'ombe then ikawa converted to cash)
Tukakomaa wakashusha mpaka milioni kumi ya Uganda.
Tutakomaa wakashusha mpaka milioni tano ya Uganda.
Mwisho kabisa wakakomea shilingi milioni nne na point kadhaa ya Uganda ambayo ni sawa na milioni tatu ya Tanzania.
Hapo wakasema haipungui hata mia.
Tukaomba tupewe muda tukatafakari kisha tutatoa taarifa ni lini tutarejea tena ukweni kukamilisha hiyo mahari.
Kumbuka hapo tumefikia hotelini.
Basi tulipo enda kujadiliana tukamuuliza muoaji kama bajeti yake ina mruhusu kulipa milioni tatu cash akasema no way out hawezi kulipa mahari yote hiyo.
Akasema alitegemea wangesema milioni moja halafu yeye angetoa laki tano au saba huku akitoa ahadi ya kumalizia mahari iliyo baki
( Waganda hakunaga kubakiza mahari. Wakati hapa Tz kuto kumalizia mahari ni heshima kubwa sana kwa wakwe kwa sababu KWANZA Inaonyesha kwamba bibi harusi sio bidhaa unayo weza kuinunua dukani na kwamba wazazi wa bibi harusi wame kutunuku binti yao ukaanzishe nae familia lakini pili Inaonyesha kwamba wewe muoaji unampenda sana mkeo kiasi kwamba haupo tayari kusubiri mpaka upate mahari kamili )
Mshenga akamuuliza bwana harusi. Hauna alternative mahali kwingine ? Yani hauna mchumba mwingine.
Jamaa akajibu nina mchumba mwingine yupo Tanzania ila yeye ni muislamu na kwao wanataka tufunge ndoa ya kiislamu.
( Mshenga akajibu nilitaka kushangaa unakosaje alternative)
Kisha akamuuliza. Upo tayari kutunga ndoa ya kiislamu? Jamaa akajibu yupo tayari.
Mshenga akajibu tunasubiri nini?
Mshenga akaenda kutoa taarifa ukweni kwamba tunarudi Dar kujipanga na tutarejea tutakapo kuwa tayari.
Jamaa karudi dar ndani ya hizo wiki mbili kavuta jiko na harusi ikafanyika kwa gharama ya kawaida sana na mtoto mwenyewe mbichi kabisa ndo KWANZA kamaliza form four ( anaweza kuwa bado hajawa dis flowered)
Baada ya kuoa jamaa kamjulisha mchumba wake wa uganda kwamba hayupo tena interested na ndoa kwa sababu hizo gharama haziwezi na kwamba ameamua kuoa sehemu nyingine..
Mwanamke wa kiganda kachanganyikiwa sasa hivi anawalaumu wazazi wake tu.
Wakristo hizo zama za wanaume kutoa mahari za mamilioni hazipo tena..
Jifunzeni kwa waislamu..mnawakosesha binti zenu ndoa kwa sababu ambazo hazina msingi.
KWANZA karne hii ukiona mtu "amepandwa na kichaa " cha kutaka kuoa Unapaswa kumpa mke haraka kabla kichaa hakija toweka, ili kichaa kiondoke tayari akiwa na mke ndani ndo akumbuke ' kumbe mimi fala hiviii'
N.B: kwa sababu ya complications zake, familia nyingi za kikristo huwa zina experience ndoa chache sana ikilinganishwa na familia za kiislamu. Dini ya kiislamu imerahisisha sana.suala la.ndoa.
Matokeo yake familia nyingi za kikristo huwa hazi fahamu saikolojia/ siasa za waoaji.
Ni hivi muoaji anapo kuja kwenye familia yako, usifikiri hajaona mwanamke mwingine au hana option nyingine. Most of the time muoaji anapo fikia hatua ya kuja kujitambulisha nyumbani kwenu tayari anakuwa na option zingine kama mbili, tatu au hata nne.
Nikija kwenye familia yako kuchumbia, halafu ukaniletea complications ngumu, mimi nitakacho kifanya nita kuachia binti yako nitaenda kwenye familia ambayo haitaniwekea complications ngumu..
Ninapo kuja kwenye familia yako usinichukulie KWANZA kama mtu ambae ninataka kumuoa binti yako, nichukulie kwanza kama.mtu ambae nimekuja kutazama kama familia yako ina complications au la