Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Nyakati hizi, karibu kila mahali duniani, Shetani anaushambulia Ukristo kwa njia mbalimbali. Anatumia mapepo, watu na mitazamo ya kijamii ili kuupiga vita ujumbe wa Yesu Kristo. Yanayoendelea kule Nigeria ni mfano tosha. Mashambulizi haya ni vita vya kiroho vyenye lengo la kuwakatisha tamaa na kuwarudisha gizani Wakristo waliopata zawadi ya wokovu aliouleta Yesu duniani.
Shetani ndiye adui mkuu wa Wakristo. Ukristo unatangaza ukweli kwamba wokovu unapatikana kwa njia ya Yesu Kristo. Jambo hili linamkera Shetani, kwa sababu hataki watu waokoke na kwenda mbinguni. Furaha yake ni kuona watu wanaenda motoni.
Kwa hiyo, Wakristo, shetani akiwapiga vita, akiwaletea mateso kama ya Ayubu, akiwachukia kwa sababu mnaishi nuruni na tiketi ya kwenda mbinguni mnayo, msilielie. Badala yake furahini kama Petro na Mitume wenzake. Walichapwa viboko kwa ajili ya Kristo na kuonywa wasifundishe tena kwa jina la Yesu! Walivyoachiliwa, walitoka wakiwa wamejaa furaha, kwa sababu walistahili kuaibishwa kwa ajili ya jina la Yesu(Mdo 5:40-41).
Hivyo kama umeokoka. Kama unaishi maisha matakatifu, tambua shetani atakushambulia tu kwa namna moja au nyingine. Akiwatumia watu kukupiga vita, usiwaombee mabaya, usiwalaumu, usiwakasirikie, usiwalaani na kamwe usinyooshe mkono wako kushindana nao.
Kumbuka wanatumiwa tu na shetani. Wasamehe bure kama Yesu alivyowasamehe waliomsulibisha, maana hawajui walitendalo. Kumbuka maneno ya Paulo kwamba hatupaswi kushindana na wanadamu. Vita vyetu ni vya kiroho, dhidi ya shetani na mapepo yake(Efe 6:12).