Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa

Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa

Yan mtu mzima analeta Uzi km huu? Lazima tutii mamlaka zilizopo. Akifariki Rais wa nchi ama mstaafu lazima atazika tofauti na mie mkulima wa kawaida huku Njombe.

Lazima tutambue kuwe vidole havilingani wala havifanani.

Akifa tajiri atazikwa tofauti pia.
 
Nakuhakikishia 100% kwamba hakuna Padre wa Kanisa Katoliki anayeweza kuendesha hata ibada tu ndani ya Parokia nyingine bila ya ruhusa ya Paroko wa hiyo Parokia. Huenda alienda kuchukua mchungaji fulani tu, lakini kwa muundo wa utendaji wa Kanisa Katoliki HAIWEZEKANI kuleta Padre wako kimya kimya
Kwa nini isiwezekane? Ungesema labda taratibu zilikiukwa tu.

Ni mambo mangapi hayapo kwenye utendaji wa kanisa na yanafanywa na mapadre?
 
Swali hilo nimekuwa nikijiuliza bila kupata jibu. Duniani haki imepokonywa na wenye mamlaka
 
Naomba kuuliza wakristo wenzangu kuhusu taratibu za msiba. Akifariki mtu wa kawaida basi Padre tu husimamia ibada. Lakini akifariki mtu maarufu au tajiri basi huja Askofu tena akiwa na viongozi wengine kuendesha hiyo ibada.
Labda tuanze kimataifa. Huyo mtu wa kawaida akifa, salamu za rambirambi kutoka nchi za nje huwa zinatolewa? Bendera huwa inapepea nusu mlingoti? Lazima ukubali, msiba wa Rais mstaafu ni msiba mkubwa, usiuchukulie poa. Vivyo hivyo, hata dini huuchukulia kwa uzito wake
 
Si afadhali hata huyo anayezikwa na Padre,wale wanaozikwa na makatekista/shemasi jee??

All in all hata ukizikwa na Papa,kama ni wa jehanum wa jehanum tuu,haya mambo ya kujilisha upepo kwa kuzikwa na tabaka flan wala si tiketi ya kuufikia uzima wa milele.
 
Si afadhali hata huyo anayezikwa na Padre,wale wanaozikwa na makatekista/shemasi jee??

All in all hata ukizikwa na Papa,kama ni wa jehanum wa jehanum tuu,haya mambo ya kujilisha upepo kwa kuzikwa na tabaka flan wala si tiketi ya kuufikia uzima wa milele.

Ni hivi...
Ibada ya mazishi sio kwa lengo la kumtoa mtu jehanamu kwenda peponi ila ni kama ishara ya maombolezo na kuonyesha mshikamano na Mkristo aliyekufa.
 
Hayo ni masuala ya protocal tu. Mtu mashuhuri kama Mkapa anapo kufa mazishi yake yanahudhuriwa na watu mashuhuri wakiwemo maaskofu. Kwa kufuata protocal kama askofu yupo basi afanye misa akisaidiwa na mapadre. Mfano papa John Paul II alikuwa mgonjwa sana lakini alitaka kuhudhuria ibada ya Christmas hivyo hakukuwa na namna zaid ya yeye kufanya misa japo hata kunyanyua mikono alikuwa hawezi.
 
Back
Top Bottom