Ndahani
Platinum Member
- Jun 3, 2008
- 18,160
- 9,151
Naomba kuuliza wakristo wenzangu kuhusu taratibu za msiba. Akifariki mtu wa kawaida basi Padre tu husimamia ibada. Lakini akifariki mtu maarufu au tajiri basi huja Askofu tena akiwa na viongozi wengine kuendesha hiyo ibada.
Kwanini Askofu asiendeshe hiyo misa hata angalau kwa msiba wa kapuku mmoja ili kuondoa hii hali ya kuonekana Askofu yuko kwa ajili ya watu fulani tu?
Kimsingi kama itawezekana Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa.
Karibuni tuchangie
Aliyenacho anaongezewa na asiyenacho ndio hivyo tena. Hata hivyo kuzikwa ma maaskofu sio mtaji wa kupata wepesi huko mbele ya safari. Tuishi maisha mema ya kumpendeza Mungu ili iwe mtaji wetu