Askofu hawezi kukufanya uende peponi bali matendo yako ukiwa hai so hata ukizikwa na katekista kama ulikua mtenda mema utaenda peponi we fikiria watu waliokufa kabla hizi dini hazijaja Tanganyika miaka ya 1,500 huko je hawataenda peponi kisa hakukuwa na maaskofu maanake dini zimekuja juzi tu
Peponi ndio wapi? Tuanzia hapo kwanza, binadamu ni kama mnyama au majani, jani likikauka na kuoza ni mbolea kwa mimea mingineyo.
Huko Peponi hakujai? Huo uwanja wa parapanda ikilia siupatii picha utakuwaje maana Tangia tuambiwe kuhusu akina Zinjanthropus mpaka kizazi hiki cha kina Lisu sipati picha wameishi binadamu wangapi.
Jiulize tu, Noah eti alitengeneza safina iliyobeba wanyama na viumbe wote kwa pair, Watu walimsusia akatengeneza yeye mwenyewe na Familly yake, huo uwanja walipolitegesha ilo safina from the scratch mpaka linaisha kwangu haimake sense, labda kuwe na story mbadala wake kama ile ya kula tunda mtaani tunaambiwa ni kugegedana.
Mafundisho mengi ni mind control tu hamna kitu. Sali sana utakufa tu, kuwa chinjachinja utakufa tu, toa sana sadaka bado utakufa tu. Jifunzeni wanyama pori mfano ambao nao ni viumbe wa Mungu, Simba anakula Swala na yeye akiotewa na manyamela kina fisi analiwa vizuri tu. Mungu tu ndio ataishi milele.
Usiniambie eti sisi ni bora kuliko wanyama, utakuwa umechanganyikiwa, kata miti na mimea yote itowayo Oxygen uone kama wewe ndio bora sana, ondoa nyuki uone kama wewe utatengeneza asali.
Far from mental slavery.