Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa

Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa

Ukiwa huna kitu tarajia kupuuzwa. Thamani ya Mtu ni kitu au vitu alivyo navyo! Huwezi kupata huduma ya mazishi yanayo endeshwa na Askofu kama wewe si maarufu, binafsi sijawahi ona kapuku akazikwa na Askofu wa kikatoliki.
 
Naomba kuuliza wakristo wenzangu kuhusu taratibu za msiba. Akifariki mtu wa kawaida basi Padre tu husimamia ibada. Lakini akifariki mtu maarufu au tajiri basi huja Askofu tena akiwa na viongozi wengine kuendesha hiyo ibada.

Kwanini Askofu asiendeshe hiyo misa hata angalau kwa msiba wa kapuku mmoja ili kuondoa hii hali ya kuonekana Askofu yuko kwa ajili ya watu fulani tu?

Kimsingi kama itawezekana Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa.
Karibuni tuchangie
Hakikisha unakuwa tajiri kabla hujafa ndiyo itakuwa salama kwako kuzikwa na watumishi high profile.
 
Mm nilivyo muona ngwajima nikajua kaja kumfufua kama anavyo dai hufufua wafu lkn nkaxhanga badala ya kumfufua et kamuombea tuweni makini na maaxkofu waongo
 
Wengine ni rafiki zao, na hiyo ni hata kwa mapadre, anaweza akaongoza misa ya rafiki yake aliyefariki, na mapadre wenyeji wakakaa pembeni.
 
MBONA YULE TAJIRI MREMA WA HOTEL ZA NGURDOTO, IMPALA NA KIBO PALACE. HAKUZIKWA NA PADRI NA ALIKUA NA PESA ZAKE ZA KUTOSHA? HALAFI MNAPASWA MJUE RATIBA YA MAASKOFU NI NGUMU KIDOGO HAWAPATIKANI KIRAHISI.
Wanafanya kazi gani sasa? Kama hawapatikani kirahisi !. Si unajua Yesu alikua simple na kanzu moja na huko miguuni sandrozi. Lakini Maasikofu wa Leo mbona naona wamevaa manguo mazito huku wameshika machuma hata waumini wanaogopa kuwasogelea. Nauliza tena huwa wanafanya kazi gani hao maasikofu wa dunia ya Leo hapa duniani ?
 
Ni ujinga tu, kujipa high status zisizo na tija yoyote. Akifa yeye au mimi wote tumekufa, hata mkiheshimu maiti yake vipi kesha kufa tu kama wafu wengine.
 
Sasa askofu hata akiongoza misa ya kapuku we utajuaje mana misiba ya watu ambao si maarufu huwa haioneshwi live kwny TV so kwangu mimi hoja yako haijakaa sawa mana hakuna ushaidi usioacha shaka kuwa hakuna kapuku aliyesaliwa na askofu
Basi anayesema wakatoliki wana ubaguzi, aseme na TBC wana ubaguzi... maana kuna misiba mingi tu hawajawahi tangaza, achia mbali kuonyesha live
 
Padri ni Daraja ya Kanisa, ni sakramenti. Askofu ni cheo sio daraja.

Hivyo, wote ni mapadri lakini Askofu anacheo. Kivingine twaweza sema wote no wanafunzi lakini mmoja ni kiranja.
.... na Papa?
 
Naomba kuuliza wakristo wenzangu kuhusu taratibu za msiba. Akifariki mtu wa kawaida basi Padre tu husimamia ibada. Lakini akifariki mtu maarufu au tajiri basi huja Askofu tena akiwa na viongozi wengine kuendesha hiyo ibada.

Kwanini Askofu asiendeshe hiyo misa hata angalau kwa msiba wa kapuku mmoja ili kuondoa hii hali ya kuonekana Askofu yuko kwa ajili ya watu fulani tu?

Kimsingi kama itawezekana Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa.
Karibuni tuchangie
Mkuu jibu lako lipo katika ufunguzi wa hoja yako mmoja ni mtu wa "kawaida"mwingine ni mtu "maarufu"
 
Lakini akifariki mtu maarufu au tajiri basi huja Askofu tena akiwa na viongozi wengine kuendesha hiyo ibada
Huu ni Utaratibu wa wanaadamu tu; Ambao sidhani ka unashida yoyote, Infact, There is no concern to GOD
Ieleweke kwamba wanadamu wanavyoishi hapa duniani kuna Taratibu zao kulingana na Mila zao na Desturi zao ama za makabila ama za Imani/Dini zao.

Mfano kuzika, Kuoa/kuolewa ni Suala la jamii, sio suala la Dini; Sasa kila Jamii ina taratibu zake, Jamii ya wakristo ina taratibu zake na jamii za waislamu; Ambayo pia Jamii ya waislamu wa Maeneo fulani wana tatofauti na jamii ya waislamu wa maeneo fulani etc.

Hivyo itoshe kusema tu kwamba, Padre/Askofu au mtu yeyote kumzika mtu ni taratibu tu ambazo wanaadamu wanakubaliana, hakuna Mahali Mungu aliweka taratibu kwa watu wake juu ya Kula, Kuzikana, Kuendesha Ibada, Kuoa na Kuolewa; Hakuna kabisa; Ukisoma Neno kwa makini utafahamu kwamba watu (Human) ndio waliweka taratibu zao; YESU alipokuja aliweka mambo wazi kabisa juu ya taratibu na kanuni za wanadamu;

NOTE: Mungu alitoa Huduma 4, Manabii, Mitume, Wainjilisti na Wachungaji ambao ni waalimu kazi yao kubwa ambayo wamepewa ni Kuhakikisha watu wanamjua YESU.
Huduma tofauti na Kumfundisha YESU ni extra curricular activities
 
Sasa askofu hata akiongoza misa ya kapuku we utajuaje mana misiba ya watu ambao si maarufu huwa haioneshwi live kwny TV so kwangu mimi hoja yako haijakaa sawa mana hakuna ushaidi usioacha shaka kuwa hakuna kapuku aliyesaliwa na askofu
Usiongee kitu ambacho hukijui ndugu, Juzi kuamkia jana tarehe 27-28 mwezi wa saba Katika wilaya ya kondoa Mhasham Baba askofu wa Jimbo Hilo aliomgoza ibada ya misa takatifu kwa muumini wa kawaida kabisa daraja la chini, Usichojua ni kuwa kanisa linahudumia waamini wote kwa usawa bila kujali hadhi zao.
 
Hiii inategemea amekufa nani na wapi sasa watu wanakufa kila siku misiba yote misa aongoze askofu tu?. Sijaona mantiki ya swali lako limekaa kishabiki sana halina maana
 
Naomba kuuliza wakristo wenzangu kuhusu taratibu za msiba. Akifariki mtu wa kawaida basi Padre tu husimamia ibada. Lakini akifariki mtu maarufu au tajiri basi huja Askofu tena akiwa na viongozi wengine kuendesha hiyo ibada.

Kwanini Askofu asiendeshe hiyo misa hata angalau kwa msiba wa kapuku mmoja ili kuondoa hii hali ya kuonekana Askofu yuko kwa ajili ya watu fulani tu?

Kimsingi kama itawezekana Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa.
Karibuni tuchangie

Swali lako unapashwa kulielekeza kwa wakristu/warumi, si wali la Wakristo.
 
Naomba kuuliza wakristo wenzangu kuhusu taratibu za msiba. Akifariki mtu wa kawaida basi Padre tu husimamia ibada. Lakini akifariki mtu maarufu au tajiri basi huja Askofu tena akiwa na viongozi wengine kuendesha hiyo ibada.

Kwanini Askofu asiendeshe hiyo misa hata angalau kwa msiba wa kapuku mmoja ili kuondoa hii hali ya kuonekana Askofu yuko kwa ajili ya watu fulani tu?

Kimsingi kama itawezekana Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa.
Karibuni tuchangie

Wakati huo upande wa pili wao kwanini yao ni kua mtu akishakufa afanyiwe mambo ma4

1 AOSHWE
2 AVIKWE SANDA
3 ASWALIWE
4 AZIKWE

simple & clear
 
Back
Top Bottom