Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa

Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa

Naomba kuuliza wakristo wenzangu kuhusu taratibu za msiba. Akifariki mtu wa kawaida basi Padre tu husimamia ibada. Lakini akifariki mtu maarufu au tajiri basi huja Askofu tena akiwa na viongozi wengine kuendesha hiyo ibada. Kwanini Askofu asiendeshe hiyo misa hata angalau kwa msiba wa kapuku mmoja ili kuondoa hii hali ya kuonekana Askofu yuko kwa ajili ya watu fulani tu? Kimsingi kama itawezekana Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa.
Karibuni tuchangie
Mengi tuuu hayapo sawa

Sent from my TECNO K9 using JamiiForums mobile app
 
Waongoza Misa leo walikuwa maaskofu wa Iringa na sijui wapi kule kusini, hivi Dar hakuna askofu au Pengo hana msaidizi? sijui hili limekaaje, hebu tufafanulieni mnaojua ni utaratibu gani ulitumika maaskofu wa mbali hivyo kuja Dar kuongoza ibada ili hali wa Dar au Morogoro wapo
Mkuu Kwanza nikufahamishe kwamba Pengo sio Askofu wa DSM kwa Sasa,Askofu wa DSM ni Ruwaichi na kwa sasa hana msaidizi kwasababu msaidizi wake ameteuliwa kuwa Askofu wa mpanda.

Lakini pia Hao maaskofu uliowaona Leo kwa mtazamo wangu hawakuja mahsusi kwa ajili ya huo Msiba,bali Walikuja kwaajili ya ibada ya kumuaga Askofu msaidizi wa DSM iliyofanyika jmosi Kwasababu ni maaskofu wa ukanda wa Mashariki.

Maaskofu waliokuja Kwasababu maalum ni Maluma ambaye ni mwenyekiti wa baraza la RUCU na Ngalalekumtwa ambaye ndiye chuo kipo kwake Kwasababu marehemu alitoa Mchango mkubwa ktk uwepo wa chuo hicho.
 
Asante kwa kunielimisha... kwa hiyo Jumanne tutawaona Maaskofu wa Dar mahala pao stahiki ?
 
Sasa askofu hata akiongoza misa ya kapuku we utajuaje mana misiba ya watu ambao si maarufu huwa haioneshwi live kwny TV so kwangu mimi hoja yako haijakaa sawa mana hakuna ushaidi usioacha shaka kuwa hakuna kapuku aliyesaliwa na askofu
 
Yule Ngalekumtwa wa Iringa ndo mkuu wa Baraza la maaskofu TEC( Sijui anaitwa Rais wa TEC/mwenyekiti)

Kwa maana hiyo ndio kiongozi wa Maaskofu wote wa Katoliki Tanzania
Ngalalekumtwa alishamaliza muda wake, kwa sasa raisi wa TEC ni Askofu Gervas Nyaisonga
 
Sasa askofu hata akiongoza misa ya kapuku we utajuaje mana misiba ya watu ambao si maarufu huwa haioneshwi live kwny TV so kwangu mimi hoja yako haijakaa sawa mana hakuna ushaidi usioacha shaka kuwa hakuna kapuku aliyesaliwa na askofu
Bro fuatilia ataona.
 
Asante kwa kunielimisha... kwa hiyo Jumanne tutawaona Maaskofu wa Dar mahala pao stahiki ?
Sidhani Kama j4 kutakuwa na ibada nyingine,kwa utaratibu ibada ya pili itakuwa huko anakozikwa.

Kutokuwepo kwa askofu Ruwaichi haimaanishi kuwa amepokwa mamlaka yake laa hasha,askofu wa Jimbo ana uwezo wa kutoa ruksa au kumuomba Askofu wa Jimbo jingine kuendesha ibada jimboni kwake.
Vile vile Ruwaichi angeweza kuwepo lakini asiwe mkuu wa ibada(main celebrant)
 
Naomba kuuliza wakristo wenzangu kuhusu taratibu za msiba. Akifariki mtu wa kawaida basi Padre tu husimamia ibada. Lakini akifariki mtu maarufu au tajiri basi huja Askofu tena akiwa na viongozi wengine kuendesha hiyo ibada. Kwanini Askofu asiendeshe hiyo misa hata angalau kwa msiba wa kapuku mmoja ili kuondoa hii hali ya kuonekana Askofu yuko kwa ajili ya watu fulani tu? Kimsingi kama itawezekana Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa.
Karibuni tuchangie
Haijalishi nani anakuzika au kinachotakiwa ni kujua wapi unakwenda baada ya kifo maana maandalizi yako ni ukiwa hai sio kusubiri sala za marehemu

Bibilia inasema ya kwamba imetupasa kufa mara moja na baada ya kifo hukumu (Waebrania 9:27). Wale waliotakaswa wataenda kwa uzima wa milele mbinguni, lakini wasioamini watapelekwa kwa hukumu ya milele ama jehanamu (Mathayo 25:46)
 
Hivi kuna utofauti gani kati ya Askofu na Padre/Padri ? Itakuwa vyema zaidi kama mtanioa maana ya wawili hawa.

Ahsanteni.
Padri ni Daraja ya Kanisa, ni sakramenti. Askofu ni cheo sio daraja.

Hivyo, wote ni mapadri lakini Askofu anacheo. Kivingine twaweza sema wote no wanafunzi lakini mmoja ni kiranja.
 
Padri ni Daraja ya Kanisa, ni sakramenti. Askofu ni cheo sio daraja.

Hivyo, wote ni mapadri lakini Askofu anacheo. Kivingine twaweza sema wote no wanafunzi lakini mmoja ni kiranja.
Ahsante. Mtu anakuwaje Padri ?
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Inategemea kuna Padri wa shirika au Jimbo. Utaratibu kwa ufupi ni Kama hivi;

1. Malezi
2. Seminary kusoma Theology na Philosophy.
3. Utume
4. Padri
Hapa kwenye Utume sijalewa, ukinipa ufafanuzi itakuwa vyema zaidi.
 
Yaani unataka wewe kapuku mchango wako kanisani hakuna, sadaka elfu 1 halafu unafariki waje maaskofu na mapadre kibao kufanya nini? kwanza unajua kuja hapo ni gharama kubwa pia.
 
Utume ndiyo kwenda Field Sasa, yaani utaskia hasa kwa Kanisa Katoliki mtu anaitwa shemasi ujue ndo utume huo akimaliza Basi anapata daraja ya upadri.
Poa.
 
Levels baby...ipo world wide hiyo sio kwenye dini peke yake.
 
Back
Top Bottom