Wakristo tuna maoni gani kwenye kutumia dawa za kufanya maiti isivunde haraka ili ichelewe kuzikwa kinyume na maandiko?

Wakristo tuna maoni gani kwenye kutumia dawa za kufanya maiti isivunde haraka ili ichelewe kuzikwa kinyume na maandiko?

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Hapo zamani kabla ya ugunduzi wa dawa za maiti za kuchelewesha kuoza na kukata shombo la kuoza, watu walikuwa wanazikwa kawaida.

Hii dawa huwa ina kemikali nyingi sana ili kufanya maiti isioze haraka.

Ni vema kukubaliana na uumbaji kwamba kwa jinsi tulivyoumbwa kwamba mtu akifa anaanza kuoza na kunuka, kumchakachua aoze taratibu na kukata shombo kwa kuchelewesha mazishi ni kumkosoa muumbaji.

Kwanini tusiiache maiti kama ilivyo izikwe.
 
Mkuu naomba kifungu Cha Biblia kinachopinga hayo mambo
Hakuna mtu aliepakwa chochote kwenye biblia ili mwili wake usioze

Na hizi dawa zimeanza kugunduliwa miaka ya mbele kabisa, hapo zamani ilikuwa mtu anazikwa kabla hajaanza kutoa harufu
 
Mtu unakuwa mzuri ukiwa hai tu ukifa uwii unanuka na kunuka balaaa yaan hatuna maana kabisa
 
Unatakiwa ujue siku hizo mochwari za kuhifadhia maiti hazikuwepo ndo maana walikuwa wanazika haraka.
Kwa hiyo Hakuna ubaya wa kuhifadhi maiti kwa kutumia madawa
 
Mwisho wa siku utaulizia pafyum tunazopuliziwa tukiwa kwenye jeneza. Maisha ni mbwembwe tu
 
Siyo dhambi kwa mwili ukihifadhiwa kwa muda,dunia ya sasa watu wametawanyika sehemu mbalimbali haitegemewi mtu anaishi Bukoba baba yake anafariki Arusha halafu asisubiriwe kwenda kumzika mpendwa wake.

Ni technology nzuri na imesaidia wengi,marehemu hakugombana na watu mpaka muanze kumkimbiza kaburini
 
Sayansi ya kutunza miili iloyokufa ilianza tangu kwa wamisri.Mwili wa aliyekufa kutunzwa ni dhambi? Hapana maana Ikiwa mama au mtoto yupo mbali na angependa kushiriki mazishi njia bora ni kuutunza
 
Muda mwingine pia mtu aliyekufa kifo chake kinawalakini hivyo inabidi watumie dawa kuutunza wakiendelea na uchunguzi
 
Hapo zamani kabla ya ugunduzi wa dawa za maiti za kuchelewesha kuoza na kukata shombo la kuoza, watu walikuwa wanazikwa kawaida.

Hii dawa huwa ina kemikali nyingi sana ili kufanya maiti isioze haraka.

Ni vema kukubaliana na uumbaji kwamba kwa jinsi tulivyoumbwa kwamba mtu akifa anaanza kuoza na kunuka, kumchakachua aoze taratibu na kukata shombo kwa kuchelewesha mazishi ni kumkosoa muumbaji.

Kwanini tusiiache maiti kama ilivyo izikwe.
Nawashangaa hata wanaooga. Kuoga na kuondoa uvundo wa jasho ni kumkufuru Muumba
 
Wakristo tuna maoni gani kwenye kutumia dawa za kufanya maiti isivunde haraka ili ichelewe kuzikwa kinyume na maandiko ?
Ni vyema ukaweka hayo maandiko yanayosema kwamba mtu akifa maiti isiwekewe dawa ya kuhifadhi
 
Vipi na ule utaratibu wa kuwazungusha marehemu kutoka eneo moja kwenda lingine, kwa ajili ya kuagwa? Na wenyewe ni utaratibu mzuri, au nao tuachane nao?
 
Hakuna mtu aliepakwa chochote kwenye biblia ili mwili wake usioze
Na hizi dawa zimeanza kugunduliwa miaka ya mbele kabisa, hapo zamani ilikuwa mtu anazikwa kabla hajaanza kutoa harufu
Si umesema ni kinyume na maandiko, leta basi hayo maandiko ili tukione kinyume chake kinachofanyika
 
Back
Top Bottom