Wakristo tuna maoni gani kwenye kutumia dawa za kufanya maiti isivunde haraka ili ichelewe kuzikwa kinyume na maandiko?

Wakristo tuna maoni gani kwenye kutumia dawa za kufanya maiti isivunde haraka ili ichelewe kuzikwa kinyume na maandiko?

Soma kitabu cha Mwanzo sura ya 50, hapo utaona namna Yakobo alivyofariki akapakwa dawa ya kumfanya asioze....aliombolezwa kwa muda wa siku 70 kabla hajazikwa. yaani maiti ilikaa miezi miwili na siku 10 watu wakiomboleza kabla ya mazishi.

Mwanzo 50Biblia Habari Njema (BHN)​

1. Hapo Yosefu akamkumbatia baba yake akilia na kumbusu.
2. Kisha, akawaagiza waganga wake wampake Israeli, baba yake, dawa ili asioze, nao wakafanya hivyo.
3. Kama kawaida, siku arubaini zilihitajika kwa kazi hiyo. Wamisri nao wakaomboleza kifo cha Yakobo kwa muda wa siku sabini.
4. Baada ya matanga kumalizika, Yosefu akawaambia watu wa jamaa ya Farao, “Ikiwa nimekubalika mbele yenu, tafadhali zungumzeni na Farao kwa niaba yangu kwamba baba yangu aliniapisha, akisema,
5. ‘Mimi karibu nitafariki. Yakupasa kunizika katika kaburi nililojichongea katika nchi ya Kanaani.’ Kwa hiyo namwomba aniruhusu niende kumzika baba yangu, kisha nitarudi.”
 
Mleta mada wewe fanya kwa ndugu zako marehemu wakifa chap kwa haraka nenda kazike,waachie wengine wahifadhi maiti kwa kemikali.
Shida iko wapi aisee au wamekuomba pesa ya kuhifadhia maiti?
Nyuzi nyingine mnaanzisha ni za kingese sana,huna mume au mke mkapeane utamu kuliko kuandika ugoro humu ndani?
 
Hakuna mtu aliepakwa chochote kwenye biblia ili mwili wake usioze

Na hizi dawa zimeanza kugunduliwa miaka ya mbele kabisa, hapo zamani ilikuwa mtu anazikwa kabla hajaanza kutoa harufu
Acha uongo huo hujui historia wewe.....nenda Misri yake
Mpaka leo miili ya mafarao ambao kabla ya Yesu kuzaliwa imeifadhiwa
 
Hapo zamani kabla ya ugunduzi wa dawa za maiti za kuchelewesha kuoza na kukata shombo la kuoza, watu walikuwa wanazikwa kawaida.

Hii dawa huwa ina kemikali nyingi sana ili kufanya maiti isioze haraka.

Ni vema kukubaliana na uumbaji kwamba kwa jinsi tulivyoumbwa kwamba mtu akifa anaanza kuoza na kunuka, kumchakachua aoze taratibu na kukata shombo kwa kuchelewesha mazishi ni kumkosoa muumbaji.

Kwanini tusiiache maiti kama ilivyo izikwe.
Mmh hapana nadhani huijui historia vizuri, hakuna watu walikuwa magwiji wa kuhifadhi maiti kama watu wa zamani.. Kuna baadhi zimechimbuliwa zikiwa fresh kabisa..soma habari za mummies
 
The Sleeping King"

Face of Seti I (1323-1279 BC) is one of most well preserved in all of ancient Egyptian mummy. He ruled when Egypt was at one of its most affluent peaks. He was the father of Ramesses II.

When he died, Egyptian Mummification was at its peak of perfection.
20230217_150707.jpg
 
Kwann tukiugua tunajitibu? Tena kwa namna mbali mbali ili uhai uendelee? Kwann tumkosoe muumba kwa kurekebisha afya?

Sent from my 2201117TG using JamiiForums mobile app
 
Siyo dhambi kwa mwili ukihifadhiwa kwa muda,dunia ya sasa watu wametawanyika sehemu mbalimbali haitegemewi mtu anaishi Bukoba baba yake anafariki Arusha halafu asisubiriwe kwenda kumzika mpendwa wake.

Ni technology nzuri na imesaidia wengi,marehemu hakugombana na watu mpaka muanze kumkimbiza kaburini
Mtu akifa azikwe mara moja akakute alichokitanguliza.
 
Hujatoa hayo maandiko yanayokataza. Vinginevyo huo ni uzushi
 
The Sleeping King"

Face of Seti I (1323-1279 BC) is one of most well preserved in all of ancient Egyptian mummy. He ruled when Egypt was at one of its most affluent peaks. He was the father of Ramesses II.

When he died, Egyptian Mummification was at its peak of perfection.View attachment 2520432
mtu akisha kufa kawa mzogo tu hana tofaoti na mzoga wa myanyama kutomzika kujidanganya
 
Hapo zamani kabla ya ugunduzi wa dawa za maiti za kuchelewesha kuoza na kukata shombo la kuoza, watu walikuwa wanazikwa kawaida.

Hii dawa huwa ina kemikali nyingi sana ili kufanya maiti isioze haraka.

Ni vema kukubaliana na uumbaji kwamba kwa jinsi tulivyoumbwa kwamba mtu akifa anaanza kuoza na kunuka, kumchakachua aoze taratibu na kukata shombo kwa kuchelewesha mazishi ni kumkosoa muumbaji.

Kwanini tusiiache maiti kama ilivyo izikwe.
mtu akisha kufa kawa mzoga hana thamani tena si kwa watoto wake mkewe wazazi ndugu nk thamani yake ni kuwaishwa kuzikwa hili hasinuke
 
Hakuna mtu aliepakwa chochote kwenye biblia ili mwili wake usioze

Na hizi dawa zimeanza kugunduliwa miaka ya mbele kabisa, hapo zamani ilikuwa mtu anazikwa kabla hajaanza kutoa harufu
Wapo wliopakwa dawa MF,yakobo na yusufu
 
Hakuna mtu aliepakwa chochote kwenye biblia ili mwili wake usioze

Na hizi dawa zimeanza kugunduliwa miaka ya mbele kabisa, hapo zamani ilikuwa mtu anazikwa kabla hajaanza kutoa harufu
Mkuu acha kukariri mambo.

Teknolojia ya kuhifadhi maiti (mummification) ilianzia Misri ya kale kuhifadhi waheshimiwa wao na watu wenye nasaba bora katika jamii, ili wakizikwa wasioze.

Si jambo lililoanza miaka ya karibuni kama unavyotaka kuaminisha watu.

Hayo mengine ya dawa gani inatumika, yaweza kuwa ni mabadiliko na maendeleo ya teknolojia tu.
 
Back
Top Bottom