Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu Zangu Watanzania,
Nimemsikia Mbunge wa Arusha Mjini Mheshimiwa Mrisho Gambo akisema na kulalamika kuwa ni aibu Kwa Arusha kukosekana kwa Stendi kubwa na ya kisasa Mkoani Arusha.
Lakini ikumbukwe na kuwakumbusheni na kumkumbusha Mheshimiwa Mrisho Gambo kuwa Kabla ya kuwa Mbunge Amekuwa DC na RC wa Arusha, lakini bado hakufanikisha kupatikana kwa stendi anayoitaka.
Sasa ni Mbunge na vilevile ni Diwani kwa nafasi yake ya Ubunge. Nafasi inayompatia nguvu na mamlaka ya kushiriki vikao vyote vya halmashauri ambavyo vina majukumu makubwa sana ya kufanya maamuzi kama hayo juu ya wapi ijengwe stendi na waanze vipi na hatua ipi kufanikisha jambo hilo.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Namshauri tu kuwa kwa sasa Mkoa wa Arusha upo chini ya Mwamba Mwenyewe na kijana jasiri kuwahi kutokea kusini Mwa jangwa la Sahara Mheshimiwa Paul Makonda, kiongozi mbunifu, mchapakazi, shupavu, madhubuti, mwenye ushawishi na nguvu ya Hoja.
Kama Mheshimiwa Gambo anataka kufaniskisha jambo hilo ambalo yeye binafsi limemshinda kwa miaka yote ya utumishi wake tangia akiwa mkuu wa wilaya ,Mkoa na sasa Mbunge aliyebakisha miezi michache kabla ya Bunge kuvunjwa. Ahakikishe Anakaa karibu na kushirikiana na Huyo Mwamba. Na ifahamike kuwa Kwa nguvu za huyo Mwamba stendi itapatikana na kukamilika tu ndani ya muda mfupi ujao.
Ifahamike kuwa mpaka sasa Mwamba Mwenyewe Makonda hana muda mrefu tangia ametua Arusha . lakini sote ni mashahidi wa namna alivyoipaisha Arusha katika secta mbalimbali hususan za utalii na biashara na kuongezeka kwa Mapato ya mkoa mzima kwa ujumla. Amefanya wana Arusha sasa kufanya biashara muda wote na jiji kuchangamka vizuri sana na kuwa kivutio cha wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Ndio maana kila mtu ni shahidi wa namna ambavyo kwa sasa mikutano na vikao mbalimbali vimekuwa vikifanywa na kufanyika Arusha.jambo ambalo lina matokeo Chanya kiuchumi.kwa sababu ni fursa kwa watu wa mahoteli,Maduka,Gest , usafirishaji n.k. kufanya biashara wakati wote na kujipatia kipato huku mapato yakikodi nayo yakiongezeka.
Kikumbwa Mheshimiwa Mrisho Gambo ashiriki vikao vya mashauriano ya Mkoa (RCC)Ambavyo Mheshimiwa Mwamba Mwenyewe Paul Makonda alisema waziwazi hadharani kuwa Mheshimiwa Mbunge amekuwa akivikwepa na kutohudhuria.
Mheshimiwa Mbunge ahakikishe anashirikiana na viongozi wote wa Mkoa badala ya kuwa katika misuguano ya hapa na pale kama ambavyo tulikuwa tukiona na kusikia kupitia vyombo vya habari siku za nyuma namna ambavyo amekuwa akiwa kwenye migogoro na watendaji mbalimbali wa serikali pamoja na wawakilishi wa wananchi.
kama ambavyo alikuwa akivurugana hadi kutoleana maneno makali hadharani na aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA Mheshimiwa Godbless Lema.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Soma Pia: Pre GE2025 - Mrisho Gambo: Nitaenda kuwajibu nini wananchi wa Arusha. Jiji kama Arusha linakosaje stendi?