Wakulima bila kuwa na chama chenye Veto Tanzania, mtanyanyasika sana na watu wanaoshinda Twitter huko mjini

Wakulima bila kuwa na chama chenye Veto Tanzania, mtanyanyasika sana na watu wanaoshinda Twitter huko mjini

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Nyie wakulima msipoungana na kuwa na chama Chenye maamuzi ya veto Mtanyanyasika Sana na Wanaoshinda Twitter kusema maisha magumu.

Na Serikali ya CCM isiyojielewa ndio inawasikiliza hao na kuwaacha nyie 70% kwenye umaskini uliotopea.

Haiwezekani Serikali ya ccm inaagiza chakula Nje ya Nchi msimu wa mavuno unaoenda kuanza mwezi wa 4.

Hapo hapo wanasema Vijana waende kwenye Kilimo ila Watoto wao hawawepeleki,bila incentives ya bei hakuna Kilimo.

Najua hao Jamaa wa Serikali watakwambia mwaka huu wao ndio watanunua mazao Ili kuwapooza lakini tunajua ambavyo Huwa na masharti na malingo na kama huna mzigo mkubwa hawanunui.

Sasa Jiandaeni Kisaikolojia bei za shambani zitakuwa 25,000-30,000 mpunga na 15,000-25,000 Kwa mahindi na watazuia mipaka Kwa kuweka vikwazo kibao.

Nawakumbusha tuu ndugu wakulima kwamba Kenya wameingiza mazao hasa mahindi kutoka Nje so hakuna soko mwaka huu mtaimba Kila wimbo na watu wa Mjini waliokataa kutoa tozo hamtakaa muwasikie wakiwasaidia..

Way forward undeni chama Chenye Nguvu ambacho kitakuwa kinawapa muelekeo kama mzalishe vyakula vyenu au mzalishe ziada ya biashara vinginevyo Bora kuacha Kilimo mkafanya uchuuzi mjini.
 
Hii ndio status yenu
Wanaowatetea wanapigwa vita ila msipoungana kuwapa Nguvu mtaishia kuwa mafukara

Screenshot_20230207-084644.jpg
 
Tatizo ni kuwa
Wanaolilia serikali kuwa bei ni kubwa ndo hao hao wanalilia serikali kuagiza nje chakula ni makosa

Siasa, Siasa, Siasa
 
Hiu nchi ngumu sana. Wakulima mlitukana watu kuwa "kama bei iko juu kalimeni nyie".

Leo gia imebadilikia angani mnaanza kulaumu serikali kwa kujaribu kutatua tatizo la bei.


Ngoja tuone, ni suala la muda.
Kwanza mm sio mkulima ni mtu kati ambae nanunua mazao kiasi bei ikiwa nzuri mjini tunawalipa vizuri huko shambani kama mwaka Jana msimu wa mavuno mahindi tuliwalipa 60,000 na mpunga 80,000-100,000 ila Kwa Mwendo huu watarajie maumivu maana Mimi nitanunua Kwa bei ndogo na naweka stoo hata miaka 2 Kwa uzoefu Wetu misimu.huwa haifuatani so wataomboleza wao sio mimi.
 
Wakulima wa wapi? Wakulima ndio wako Twitter huko? Au jf?
Mimi nazunguka vijijini,nashuhudia hohehae wanavyo haha kununua unga na mchele kwa hizi bei..unakuta ndani hana akiba yoyote..mazao yote aliwauzia walanguzi kipind cha mavuno tena kwa bei ya chini..mlanguzi akaweka stoo,na sasa anawauzia kwa bei kubwa (mara nne ya aliyo nunulia)
 
Mimi nazunguka vijijini,nashuhudia hohehae wanavyo haha kununua unga na mchele kwa hizi bei..unakuta ndani hana akiba yoyote..mazao yote aliwauzia walanguzi kipind cha mavuno tena kwa bei ya chini..mlanguzi akaweka stoo,na sasa anawauzia kwa bei kubwa (mara nne ya aliyo nunulia)
Hao ni wachache sana,wengi Wana akiba.

Sasa kama anategemea Kilimo kukidhi mahitaji kikakutana na bei mbaya kabisa itakuaje Sasa kwenye hayo mambo mengine? Utampa kibalua kulima heka Kwa 15,000 Kwa sababu Sokoni pesa ni ndogo
 
Wakinunua alfu 25,nakula mwenyewe kwani shida nin?
 
Hao ni wachache sana,wengi Wana akiba.

Sasa kama anategemea Kilimo kukidhi mahitaji kikakutana na bei mbaya kabisa itakuaje Sasa kwenye hayo mambo mengine? Utampa kibalua kulima heka Kwa 15,000 Kwa sababu Sokoni pesa ni ndogo
we hata kulima hujawai wala biashara ya mazao huifahamu ,serikali ipo sawa
 
HII NCHI SIYO YA WAKULIMA TU.

Ni jukumu la serikali kuwapa nafuu wananchi wote. Mfymuko wa bei umekuwa mkubwa kuliko kipato cha mtanzania wa kawaida. Ni lazima serikali iingilie kati.

Wakulima wasitafute huruma ya kuumiza wengine. Wao waendelee kuuza kwa bei wanatoitaka na kujipangia, lakini serikali ina ulazima wa kuwasaidia wengine wenye kipato kidogo.
 
HII NCHI SIYO YA WAKULIMA TU.

Ni jukumu la serikali kuwapa nafuu wananchi wote. Mfymuko wa bei umekuwa mkubwa kuliko kipato cha mtanzania wa kawaida. Ni lazima serikali iingilie kati.

Wakulima wasitafute huruma ya kuumiza wengine. Wao waendelee kuuza kwa bei wanatoitaka na kujipangia, lakini serikali ina ulazima wa kuwasaidia wengine wenye kipato kidogo.
Wakulima na nyie wengine wapi wanaongoza Kwa umaskini hapa Tanzania tena wa kutengenezewa na watu wa Mjini wenye Nguvu za maamuzi?

Wakulima jitambueni zalisheni chakula chenu tafuteni kazi zingine za kufanya muingize kipato
 
Shida hiko wapi wakulima wanataka wauze wanapotaka kwa bei ya soko na serikali aijazuia wao kufanya ivyo; sasa malalamiko ya nini si waendelee kupeleka hiko chakula walicho nacho Congo, Rwanda, Burundi, Zambia, Kenya na sijui wapi kwengine wanapouza.

Vinginevyo hivi vilio inakuwa ni kutaka serikali iendelee kuwatetea watu wanao hodhi mazao ya chakula na kuendelea kufaidika na bei za anasa kutokana na uhaba uliopo nchini.

Now that is not free market isipokuwa ni collusion ya oligopoly and profiteering. Mambo ya aina hii ata m hiyo serikali ya marekani ambapo idea yao ya free market mpaka jela zipo privatised, lakini ata wao wanamipaka serikali yao aiwezi promote anti competition policies kwenye maswala ya basic needs za raia wake. Hizo ni akili za Bashe tu na watu wasio na huruma.
 
Ushauri Wakulima ongezeni ubora wa mazao yenu mkauze Nje ya Nchi maana mchele wa Tanzania kwenye soko ni Bora kuliko huo wa Nje ya Nchi.

Kwa hapa Tanzania watu wengi ni maskini hivyo hawana uwezo wa kununua mchele wa Tanzania so only soko la uhakika ni Nje ya Nchi tuu.
 
Nyie wakulima msipoungana na kuwa na chama Chenye maamuzi ya veto Mtanyanyasika Sana na Wanaoshinda Twitter kusema maisha magumu...
Mbona kelele zimekuwa nyingi? Nyinyi si mkauze mazao yenu nje ya nchi kama alivyo ruhusu Waziri wenu Bashe, ili mpate faida kubwa!

Iacheni serikali iruhusu chakula kiingie nchini ili sisi ambao siyo wakulima tuweze kununua kwa bei yenye uhalisia! Hamuwezi kutuuzia kilo ya mchele kwa 3800, halafu tuwachekee tu. Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Back
Top Bottom