Wakulima mwakani tunategemea muwe matajiri

Longoshe

Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
52
Reaction score
66
ndugu zangu wana JF nimefuatilia mijadala mbali mbali juu ya bei za nafaka kupanda, ila watu wana mitazamo tofauti tofauti kama ifuatavyo

1. kuna wanaosema kwa sasa wakulima wananufaika kwani bei zipo juu

2. kuna wanaosema wakulima hawanufaiki kwani anaye uza ni mtu wa katikati kati ya mkulima na mtumiaji

3. kuna wanaosema kwamba hali ya sasa hivi ni bora kwani kipindi cha nyuma Magufuli alifunga mipaka hivyo ikapelekea bei ya nafaka kuwa chini

Swali langu ni je sisi watumiaji wa mwisho tutaishi maisha gani kama uwezo wetu wa kununua nafaka hizi itakuwa ni mdogo??

Na je serikali ya mama samia inachukulia vipi swala hili la bei za nafaka kuwa juu??

Je furaha ya wakulima mazao kuwa juuu inatokea wapi ikiwa ruzuku wanazopewa Wakulima ni za Watanzania wote??
 
Bei zipo juu masokoni sio mashambani. Pia hapo pembejeo zitapanda bei, mvua zitaanza kuringa, wanaomwagilia watapandishiwa bei ya Maji na ofisi za Bonde, wanaobeba (wenye mafuso) watapandisha wakilalamika wese, blah blah blah
 
Mkulima hawezi kua tajiri atabaki kua maskini wengi mazao wameyauza mapema kwa wanunuzi shambani wengine mazao yalikaukia shambani mkulima kua tajiri ni kitu kigumu ni kama ngombe kuangalia t.v
 
Unajua Bei ya mbolea?

Ukitaka kuwa maskini nchi hii kuwa mkulima.
 
Mkulima wa tanzania huyu wa jembe mkononi awe tajiri sahau..hata alime vipi kwakilimo cha mvua hivi pembejeo za kubahatisha na feki.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wakulima wengi tu watatajirika msimu huu ila wawe wale waliolima mashamba makubwa na walitunza nafaka hizo hadi sasa
Kwa wale wanaosema mtu hawezi kutajirika kupitia kilimo nampa pole maana wakulima wengi tu ni matajiri eg.RUTO na the late SUMMRY , Kuaminishana kwamba kilimo hakiwezi kumtoa mtu kwenye umasikini ni ujinga kama ujinga mwingine tu
 
Kama hela ipo, wekeza kwenye kilimo; kinachopandisha bei, walaji ni wengi kuliko wazalishaji.

Kopa, milioni 20, wekeza kwenye kilimo; rudisha deni, kula faida
 
Naam na muhimu uwe ushajifunza na kuona kwa vitendo how possible you can run this
Wanaosema kilimo hakina pesa ni hawahawa wanawalaumu wakulima kupandisha bei ya mazao.

1 acre ya mahindi inaweza kukupatia 1-4 milions per year kutegemea na bei , kama umelima kwa standard inayotakiwa.
Mtu atakucheka ohh one milion per year ndo ukae unaisubiri tu !? Wanasahau maisha ni hatua kama leo nimepata 3mil per year means nikipambana naweza kupata 6m next year maana nitaongeza shamba , after 5 years watu wanaambiwa unaingiza milion 25-30 per year kwenye kilimo hichohicho utasikia wanasema wewe ni freemason
 
Mtu atakucheka ohh one milion per year ndo ukae unaisubiri tu !? Wanasahau maisha ni hatua kama leo nimepata 3mil per year means nikipambana naweza kupata 6m next year maana nitaongeza shamba , after 5 years watu wanaambiwa unaingiza
Kilimo kinalipa sana; tunakoelekea mkulima mfanyabiashara atakuwa na maisha mazuri kuliko muajiriwa
 
Hakika serikali wamefanya vizuri sana kuamua kujitenga na ishu ya kumpangia bei mkulima na wakiendelea hivi mkulima atampita mfanyakazi kitambo sana
Mkulima hawezi kumpita mfanyakazi acha kuwazuga
 
Kama hela ipo, wekeza kwenye kilimo; kinachopandisha bei, walaji ni wengi kuliko wazalishaji.

Kopa, milioni 20, wekeza kwenye kilimo; rudisha deni, kula faida
Kilimo hakina dhamana chonde chonde mtu usikope ukalime vinginevyo uwe na kilimo cha uhakika kama kilimo cha miwa kule turiani
 
Wakulima wengi tu watatajirika msimu huu ila wawe wale waliolima mashamba makubwa na walitunza nafaka hizo hadi sasa
Kwa wale wanaosema mtu hawezi kutajirika kupitia kilimo nampa pole maana wakulima wengi tu ni matajiri eg.RUTO na the late SUMMRY , Kuaminishana kwamba kilimo hakiwezi kumtoa mtu kwenye umasikini ni ujinga kama ujinga mwingine tu
Sumri alienda kwenye kilimo huku akiwa ni tajiri
 
Kilimo hakina dhamana chonde chonde mtu usikope ukalime vinginevyo uwe na kilimo cha uhakika kama kilimo cha miwa kule turiani
Ni kweli, kutegemea mvua ni tatizo pia, hali ikiwa nzuri, utavuna; ila ikiwa mbaya ni hasara
 
Mimi ni mkulima mdogo, nimelima kwa jembe la mkono, nina gunia 22 ndani nasubiri January niuze angalau Tsh 130000 kwa gunia, je hapo nitakua sijapata mtaji? Hakuna mipaka kufungwa, anaeona nafaka iko juu, arudi kijijini alime
 
Naam na muhimu uwe ushajifunza na kuona kwa vitendo how possible you can run this
Wanaosema kilimo hakina pesa ni hawahawa wanawalaumu wakulima kupandisha bei ya mazao.

1 acre ya mahindi inaweza kukupatia 1-4 milions per year kutegemea na bei , kama umelima kwa standard inayotakiwa.
Mtu atakucheka ohh one milion per year ndo ukae unaisubiri tu !? Wanasahau maisha ni hatua kama leo nimepata 3mil per year means nikipambana naweza kupata 6m next year maana nitaongeza shamba , after 5 years watu wanaambiwa unaingiza milion 25-30 per year kwenye kilimo hichohicho utasikia wanasema wewe ni freemason
Hii kitaalamu inaitwa THE COMPOUND EFFECT [emoji123]
 
Back
Top Bottom