KERO Wakulima wa Mpunga Kilosa tunateseka na Mashamba, wakati wa mavuno Halmashauri wanakuja na ushuru unaotuumiza

KERO Wakulima wa Mpunga Kilosa tunateseka na Mashamba, wakati wa mavuno Halmashauri wanakuja na ushuru unaotuumiza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Halmashauri ya Kilosa kuchukua Sh 2,000 kwa kila gunia la mpunga kwa Wakulima wa mpunga katika Kata ya KIMAMBA A na KIMAMBA B Wilayani KILOSA mkoani MOROGORO, ni maumivu makali kwetu kwa kuwa ni kama hawatusaidii chochote kisha

Wakulima wanaolima Bonde la Kimamba kwa sasa wanahangaika na mafuriko ya Mto Mkondoa mazao yao yanaenda na kuharibiwa lakini ikifika mwezi wa sita wakati wa mavuno gari la Halmashauri linakuja linaweka geti njia ya kutokea shambani.
photo_2026-03-28_23-53-19.jpg

photo_2026-03-28_23-55-04.jpg

photo_2026-03-28_23-55-05.jpg

Kila Mkulima anayepita na trekta la mzigo analipia Sh 2,000 kwa kila gunia wakati shamba amekodi yeye, mbegu zake na gharama zote na anatumia maji ya mvua kwanini halmashauri ije kuchukua pesa ya ushuru?

Hiyo buku mbili wanatoza kama ushuru wa kila gunia la mpunga linalotoka shambani, Mto Kondoa Wilayani Kilosa, mashamba tunayolima Wakulima tunategemea maji ya mvua, je, huo ushuru wanaoutoza wamewafanyia miundombinu gani shambani mpaka wachukue pesa kwa kila gunia?

Huu ushuru umekuwa kero sana na unatuumiza Wakulima maana tunaonewa, yaani Wakulima wanaivisha kwa kudra za mwenyezi Mungu.

Hawajui changamoto zote tunazopitia shambani ila wao muda wa mavuno wanakuja na gari lao kutoka Halmashauri na mgambo wanatoza ushuru.

Maana gharama tunazotumia shambani ni kubwa tena ukiwa unapeleka mazao stoo/ghalani kabla hujayafikisha wanaomba ushuru.
photo_2026-03-28_23-55-08.jpg

photo_2026-03-28_23-53-16.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Ngoja nitoe maoni kistaarabu kabisa.

Yani shamba langu, mbegu nimehangaika kuzipata mwenyewe, nimehangaika kuembeka mwenyewe na kulipa watu mvua na jua vimetushona

Barabara mbovu ya matope, maisha ya kilosa ni magumu kuliko hata Masasi, hospital hazina dawa nikiugua tunaenda kununua dawa na mahitaji mengine si ndio?

Sasa kodi wanayodai ni kwa ajili ya kazi gani na je walishiriki kwenye lolote kwenye ulimaji wangu kama jibu ni hapana

Yule Mzanzibar Shaka Hamdu Shaka atatuma Polisi waniue wallah naondoka na vichwa vya wote kwenye hilo gari siui tu nakata vichwa vyao
 
Back
Top Bottom