Wakumbuka nini enzi za shule ya msingi?

Nilikuwa mkorofi sana darasani. Siku moja nikafumwa nikabananishwa na walimu. Mbona nilitoka na dirisha.

Ila juzi juzi hapa mwaka huu nilitoa hela lile dirisha nililovunja lijengwe.

Achana na mimi kabisaaa.....!!!
 
nakumbuka tu nilivyokuwa naporwa barafu pindi ninunuapo aiseeeeeeeeeeeee
 
Kuomba vitu mapumzikoooo, Nilikuwa natafuta rafiki ambaye mda wa kula ana nunua vitu vizurii
 
Tabia ya kupigana kesi kila wakati home sharti langu la shule vifungo vitatu au viwili mama kashona kachoka.
 
Nakumbuka ilikua j3 siku ya ukaguz /usafi.jpil nilichelewa kufua nguo sasa inafka siku ya j3 asubuh shat la shule alijakauka nikaona isiwe kesi nikakata kola ya shat kisha nikalipiga pasi vizuri nikavaa na sweta langu Ile kola nikaitoa kwa nje.mda tukiwa mstarini mwalim Kafika kwangu kwa nyuma akabinua kola yangu aone kama nimefua.kakuta kola ina ng'aa balaah akaanza kuni mwagia sifa kede kede.dadek kimbembe nikaambiwa nitoke mbele nivue sweta wanione nilivyo smart kilicho tokea Mungu anajua 🤣🤣🤣
 
Mm nilikuwa mwizi sana hasa wakati wa michezo ya umitashumta. Nilikuwa mtaalamu wa kudokoa vyakula vya wale kinamama Waliokuwa wanakuja kuuza. Sasa kuna fimbo ndefu walikuwa wanakaa nayo ili kulinda Mali zao, inaitwa 'nnlo'. Sasa wakiniona tu, utasikia chukua nnlo amekuja. Hata hivyo kwa utaalamu niliokuwa nao, nilikuwa nawasukumizia wanunuaji wengine waliosimama kwa wale kina mama then mm natoka na karai la ndizi kiulani!!! Hata hivyo nilishaenda kutubu, na nina imani nilishasamehewa hahaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahahaha dah jeiefu ni mwisho wa matatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SI
KUWAHI KUVAA MPAKA NILIPOFIKA DARASA LA NNE, TENA SIKU YA MTIHANI WA TAIFA. NA NILIAZIMA KWA MANZI JIRANI YETU NILIYESOMA NAE CLASS MOJA
 
Daaah... nakumbuka nilikuwa nikinunua kachori nakimbia kwenda kujificha kwenye Korongo. ili wenzangu wasiniombe.. siku moja nilikimbilia kule kumbe sikujua kulikuwa na madondola ya linipiga sindano za uso , Aise niliumuka sasa kama maandazi yaliyowekwa Amira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mm kwakweli nakumbuka kuwekea watu vioo chini ili niwachungulie,pia nakumbuka siku ya usafi likuwa ni j3 na alhamisi nilikuwa nafua lesso ili kucha zing'ae
mkuu kuwawekea vioo waschana ili kuwa chungulia sin umalaya huo??
 
Tulikuwa tunapenda sana kuchezea maji na utelezi hasa mvua inponyesha tena bila viatu kama picha hii inavyoonyesha

nilikuwa mchelewaji afu muoga kupindukia!!! nilikuwa namtanguliza mlw mkuu mbele afu mimi ndo naingia shule kama waziri wa elimu!!! (as if mi ndo nilimwajiri)

siku moja alinibamba akaniambia nimsubiri ofcn kwake...kama alinipata......
umenikumbusha mbali saaana mkuu!YOU HAVE MY THANKS
Bila kusahau kuruka ukuta na kutokea dirishani hasa wakati wa kwenda kufagia viwanja na kunyeshea maua sie "wajanja" tulikuwa tunasepa

Ppp
 
Nlikua naingia mchana, kwahiyo kumwagilia maua mbele ya darasa letu na kiranja alikua ana tick madumu 15 kila mtu ole wako usifikishe [emoji23]
 
Nakumbuka tulitangaziwa kwamba tujiandae atakuja mtangazaji wa redio Tanzania kuturekodi kipindi cha watoto yaani mashairi, hadithi na ngonjera. Nikachaguliwa.

Siku iliyofuata mwalimu akapunguza majina na mimi akaniondoa, nikagoma kwa hoja kwamba ninaweza.

Darasa zima likashangaa mimi kumkatalia mwalimu. Sasa akasema basi atanitoa kwenye hadithi na ataniingiza kwenye shairi. Lakini shule haitatunga shairi bali mimi nitunge shairi na nilisome mwenyewe redioni.

Nilikuwa brilliant kuliko wote darasani lakini mwalimu alinikomoa kunipa shairi unajua wakati ule mashairu walikuwa wanakaririr wasichana tu.

Darasa zima na mwalimu wakajua ntashindwa na akanipa siku mbili niwasilishe shairi kabla mtangazaji hajaja.

Yule mwalimu hakujua uwezo wangu wa kujua na ktunga mashairi. Ndani ya siku moja nikampelekea na toka siku hiyo wasichana wakaniogopa kwenye mashairi.
 
Shule yetu ilikuwa imepakana na masista wa kanisa katoliki wana mti wa mapera. Tulikuwa tunaiba kila siku wanatufukuza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…