Binafsi nimesoma Shule ya msingi Jamhuri mjini Moshi, nilikuwa naishi Police line.Mambo nayoyakumbuka nilipokuwa nasoma Primary:
1.Kupigana siku ya kufunga shule.
2.Kutoroka darasani kwa kupitia dirishani Mwl wa Hisabati anapofundisha.
3.Kwenda Uzunguni kuangua maembe na kuchuma zambarau.
4.Kutoka Police line hadi Kwa Fonga TPC kuchukua miwa.
5.Kwenda CCP na karandinga la Polisi kuangalia michezo mbalimbali iliyokuwa inajumuisha Polisi wa Mikoa yote Bara na Visiwani.
6.Nawakumbuka baadhi ya wachezaji wa Polisi waliokuwa na mashuti makali kama Mohamed Ndutu,Brown Mwaitegete, Pius aliyekuwa Kikosi cha Kutuliza Ghasia na wengine wengi.
6.Kutoroka darasani kwenda kusaka kware.
7.Mechi ya mpira kati watoto wa Police line na wale watoto wa ng'ambo Police Dog Section, kila tukicheza nao lazima tuwafunge na ngumi lazima zipigwe.
8.Kushindanishwa shule kitaaluma Korongoni, Muungano,Mwenge, Jamhuri na Mawenzi, shule yetu kila tukishindanishwa tunakamata nafasi ya pili, licha ya kuwa na watoto watukutu wa line.
Wewe unakumbuka nini enzi ukisoma Primary?