SubiriJibu
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 1,805
- 1,876
Daaah... nakumbuka nilikuwa nikinunua kachori nakimbia kwenda kujificha kwenye Korongo. ili wenzangu wasiniombe.. siku moja nilikimbilia kule kumbe sikujua kulikuwa na madondola ya linipiga sindano za uso , Aise niliumuka sasa kama maandazi yaliyowekwa Amira
Sent using Jamii Forums mobile app
Gubiti ni nini?Kila siku mapumziko kumikuwa na jamaa anauza gubiti. Wakitoa hela wengi naingiza mkono nachomoa.
Siku moja akaniona akanikimbiza akanikamata bwana.
Alinipiga mtama nikaangukia kisogo huku shule nzima inaona. Toka siku hiyo nikaacha wizi wa gubiti.
Sijui gubiti zikipotelea wapi.
Gubiti ni nini?
Owkay mkuu nmekupataKama ulikulia Mwanza miaka hiyo gubiti ilikuwa ni aina ya sukari guru inakaangwa hlafu viakatwa vipande vidogovidogo unakula kwa kulamba kama hizi ice cream za njiti za sasa.
Madam Salome Haule kama upo humu jf mm ni mwanafunzi wako,ulihama shule ile (huko simiyu) baada ya sisi kumaliza,ninakumbuka mambo mengi ulinitendea mazuri na yaliyofungua njia ya mafanikio yangu,nimejitahd sana kukutafta kwny mitandao ya kijamii sijafanikiwa kukupata,Tafadhali sana madam,mm mwanafunzi wako nakutafta sana japo niseme asante kwako,nafsi inanilazmisha nihtaj kuonana naww ila nashindwa sabab sjui nianzie wapi,please ukisoma ujumbe huu jua mwanafunzi wako BUFFET anakutafta sanaBinafsi nimesoma Shule ya msingi Jamhuri mjini Moshi, nilikuwa naishi Police line.Mambo nayoyakumbuka nilipokuwa nasoma Primary:
1.Kupigana siku ya kufunga shule.
2.Kutoroka darasani kwa kupitia dirishani Mwl wa Hisabati anapofundisha.
3.Kwenda Uzunguni kuangua maembe na kuchuma zambarau.
4.Kutoka Police line hadi Kwa Fonga TPC kuchukua miwa.
5.Kwenda CCP na karandinga la Polisi kuangalia michezo mbalimbali iliyokuwa inajumuisha Polisi wa Mikoa yote Bara na Visiwani.
6.Nawakumbuka baadhi ya wachezaji wa Polisi waliokuwa na mashuti makali kama Mohamed Ndutu,Brown Mwaitegete, Pius aliyekuwa Kikosi cha Kutuliza Ghasia na wengine wengi.
6.Kutoroka darasani kwenda kusaka kware.
7.Mechi ya mpira kati watoto wa Police line na wale watoto wa ng'ambo Police Dog Section, kila tukicheza nao lazima tuwafunge na ngumi lazima zipigwe.
8.Kushindanishwa shule kitaaluma Korongoni, Muungano,Mwenge, Jamhuri na Mawenzi, shule yetu kila tukishindanishwa tunakamata nafasi ya pili, licha ya kuwa na watoto watukutu wa line.
Wewe unakumbuka nini enzi ukisoma Primary?