Wakumbukeni Wastaafu wa umma pia. Ongezeni Pensheni zao

Motto61

Member
Joined
Jul 7, 2015
Posts
94
Reaction score
60
Napenda kumpongeza sana Rais Samia kwa maamuzi aliofikia ya kuongeza mishahara ya wafanyakazi wa serikali Mungu akubariki.

Aidha napenda kuwakumbusha kwamba kusahau ni kwa binadamu, wastaafu waliotumikia serikali na kujenga misingi yake, baadhi yao bado wako hai. Pesheni zao ni ndogo sana na kwa sheria za zamani hawakuruhusiwa kufanya biashara enzi hizo.

Baada ya mishahara kupanda bidhaa nazo kwa hakika zitapanda kwa kiasi kikubwa hawa wazee wanyonge wataishije? wakumbukeni wastaafu na wazee wenu pia.
 
Mtaanza na kudia mafao ya marehemu wa zamani yaongezwe Sasa ebu kubalini uhalisia kuwa mlistaafuu na pesa mliyopewa mda ule ilistahili na ilifaa tatizo wastaafu wa zamani wakiamini kurudi kijijini kwao ndio mpango mzima wakastaafu wakarudi maeneo ambayo hawakuwepo zaidi ya miaka therathini wengine wakakimbia na familia wakaenda kwa vibinti vya mjini
 
Umri wa kustaafu pia uangaliwe upya, Miaka 50 iwe ni kustaafu kwa hiari 55 iwe ni umri wa lazima ili vijana nao wapate ajira.
 
Mtaanza na kudia mafao ya marehemu wa zamani yaongezwe Sasa ebu kubalini uhalisia kuwa mlistaafuu na pesa mliyopewa mda ule ilistahili na ilifaa tatizo wastaafu wa zamani wakiamini kurudi kijijini kwao ndio mpango mzima wakastaafu wakarudi maeneo ambayo hawakuwepo zaidi ya miaka therathini wengine wakakimbia na familia wakaenda kwa vibinti vya mjini
Asante kwa mawazo haya.
Maoni yako ni haki yako.
Hata hivyo ungefahamu kiwango wanachopewa, uhalisi wa maisha yao na mengineyo huenda ungeandika tofauti.
Nahisi kuwa ungejipa muda wa kutosha kutafakari kwa kina kabla hujajibu hivyo ungetoa jibu bora zaidi linalosawiri haiba yako.
 
Napenda kumpongeza sana Rais Samia kwa maamuzi aliofikia ya kuongeza mishahara ya wafanyakazi wa serikali Mungu akubariki.

Aidha napenda kuwakumbusha kwamba kusahau ni kwa binadamu, wastaafu waliotumikia serikali na kujenga misingi yake, baadhi yao bado wako hai. Pesheni zao ni ndogo sana na kwa sheria za zamani hawakuruhusiwa kufanya biashara enzi hizo.

Baada ya mishahara kupanda bidhaa nazo kwa hakika zitapanda kwa kiasi kikubwa hawa wazee wanyonge wataishije? wakumbukeni wastaafu na wazee wenu pia.
Wastaafu ni kama yatima, hawana wa kuwasemea. Vyama vya wafanyakazi wanatetea kama Bado uko kazini, ukistaafu wanakuona useless.
Kuna wastaafu wanalipw 100,000 kwa mwezi, nani awatete, maisha magumu.
Nashauri vyama vya wafanyakazi teteeni wastaafu, walikuwa wanachama wenu
 
Asante kwa mawazo haya.
Maoni yako ni haki yako.
Hata hivyo ungefahamu kiwango wanachopewa, uhalisi wa maisha yao na mengineyo huenda ungeandika tofauti.
Nahisi kuwa ungejipa muda wa kutosha kutafakari kwa kina kabla hujajibu hivyo ungetoa jibu bora zaidi linalosawiri haiba yako.
Sasa mstaafu alipwe kwa uhalisia wa maisha ya Sasa anazalisha nini mjumbe, kipato alicholipwa kilimfaa mda ule kuandaa maisha yake ya sasa,

Cha msingi hapa nikukumbusha watu wlaiopo makazini kuandaa maisha yao ya kustaafu waakiwa bado wapo kwenye ajira hii itapunguza mambo kama haya
 
Kwa mawazo yako haya unadhani pensheni iliwekwa kwa akili ya nini? Siyo kwamba imsaidie huyu aliyetumikia Taifa wakati ameishiwa nguvu za mwili na kiuchumi? Mawazo yako yanakutuma mtumishi aliyestaafu Hana faida yoyote na unatamani pensheni ifutwe kabisa!
 
Sasa mstaafu alipwe kwa uhalisia wa maisha ya Sasa anazalisha nini mjumbe, kipato alicholipwa kilimfaa mda ule kuandaa maisha yake ya sasa,

Cha msingi hapa nikukumbusha watu wlaiopo makazini kuandaa maisha yao ya kustaafu waakiwa bado wapo kwenye ajira hii itapunguza mambo kama haya
Dogo, jitafakari Sana na chunga kinywa chako kwani uyanenayo Sasa yana tabia ya kupiga Kona na kurejea yalikotoka! Mungu fundi mno yaani atakupa maisha marefu ili aone Kama ulijiandaa na mwisho atakusaidia ulipwe pensheni Yako akuongoze kuipeleka ulikowanenea wengine ili watakaokuwepo waandike tofauti na wewe na au wakukumbushe!
Dunia Ina kanuni zake nenda nazo taratibu!
 
Ni rahisi kusema lakini utekelezaji ni mgumu sana! Hebu niambie mstaafu aliyestaafu na mshahara wa sh 600,000/= alipoanza kuajiriwa alikuwa anapata mshahara wa sh ngapi? Ujue huyu baadaye alioa na kupata watoto ambao alilazimika kuwahudumia kwa elimu nk. Akijitahidi Sana ataweza kuwa amejenga nyumba kwa msaada wa mikopo ambayo imemlazimisha Aishi maisha magumu akiwa kazini!!
Akija kustaafu ukute bado Kuna mtoto mmoja au wawili bado wako shuleni!! Ada ya chuo ni mamilioni Hadi wamalize!! Katika mazingira hayo angejiandaaje kwa mfano?
Kuna watu wengi wamestaafu wanaishi maisha magumu Sana. Wengi wao pensheni Yao ni kati ya 100,000/= na 450,000/=, na bado Wana wategemezi!!
 
Mtaanza na kudia mafao ya marehemu wa zamani yaongezwe Sasa ebu kubalini uhalisia kuwa mlistaafuu na pesa mliyopewa mda ule ilistahili na ilifaa tatizo wastaafu wa zamani wakiamini kurudi kijijini kwao ndio mpango mzima wakastaafu wakarudi maeneo ambayo hawakuwepo zaidi ya miaka therathini wengine wakakimbia na familia wakaenda kwa vibinti vya mjini
Usisahau na wewe siku moja utastaafu. Na wala siyo mbali saaana.

Kuna muheshimiwa mmoja alikuwa katibu mkuu ofisi ya raisi enzi zilee. Alikuwa akipelekewa file la mapendekezo ya marekebisho ya pensheni akiyapiga na chini. Siku ya siku alikuja kustaafu akaanza kulalamika eti pensheni ndogo sana. Alijisahau na kudhania angedumu kwenye ile post indefinitely.
 
Napenda kumpongeza sana Rais Samia kwa maamuzi aliofikia ya kuongeza mishahara ya wafanyakazi wa serikali Mungu akubariki.

Aidha napenda kuwakumbusha kwamba kusahau ni kwa binadamu, wastaafu waliotumikia serikali na kujenga misingi yake, baadhi yao bado wako hai. Pesheni zao ni ndogo sana na kwa sheria za zamani hawakuruhusiwa kufanya biashara enzi hizo.

Baada ya mishahara kupanda bidhaa nazo kwa hakika zitapanda kwa kiasi kikubwa hawa wazee wanyonge wataishije? wakumbukeni wastaafu na wazee wenu pia.
Naunga mkono hoja
 
Dogo, jitafakari Sana na chunga kinywa chako kwani uyanenayo Sasa yana tabia ya kupiga Kona na kurejea yalikotoka! Mungu fundi mno yaani atakupa maisha marefu ili aone Kama ulijiandaa na mwisho atakusaidia ulipwe pensheni Yako akuongoze kuipeleka ulikowanenea wengine ili watakaokuwepo waandike tofauti na wewe na au wakukumbushe!
Dunia Ina kanuni zake nenda nazo taratibu!
Huyu amenishangaza sana, kwa sasa yeye kama ni mtumishi mwenye umri mdogo atajiona ana akili sana, lakini huko mbele atayaona.
 
Napenda kumpongeza sana Rais Samia kwa maamuzi aliofikia ya kuongeza mishahara ya wafanyakazi wa serikali Mungu akubariki.

Aidha napenda kuwakumbusha kwamba kusahau ni kwa binadamu, wastaafu waliotumikia serikali na kujenga misingi yake, baadhi yao bado wako hai. Pesheni zao ni ndogo sana na kwa sheria za zamani hawakuruhusiwa kufanya biashara enzi hizo.

Baada ya mishahara kupanda bidhaa nazo kwa hakika zitapanda kwa kiasi kikubwa hawa wazee wanyonge wataishije? wakumbukeni wastaafu na wazee wenu pia.

Wazo lako ni Zuri sana Hakika Kila Mtu ni Mstaafu mtarajiwa[emoji736][emoji736][emoji736]
 
Sasa mstaafu alipwe kwa uhalisia wa maisha ya Sasa anazalisha nini mjumbe, kipato alicholipwa kilimfaa mda ule kuandaa maisha yake ya sasa,

Cha msingi hapa nikukumbusha watu wlaiopo makazini kuandaa maisha yao ya kustaafu waakiwa bado wapo kwenye ajira hii itapunguza mambo kama haya
Utakapostaafu utakumbuka kuwa ulichangia hoja kitoto Sana.
 
Back
Top Bottom