Wakumbukeni Wastaafu wa umma pia. Ongezeni Pensheni zao

Wakumbukeni Wastaafu wa umma pia. Ongezeni Pensheni zao

Usisahau na wewe siku moja utastaafu. Na wala siyo mbali saaana.

Kuna muheshimiwa mmoja alikuwa katibu mkuu ofisi ya raisi enzi zilee. Alikuwa akipelekewa mefinitelapendekezo ya marekebisho ya pensheni akiyapiga na chini. Siku ya siku alikuja kustaafu akaanza kulalamika eti pensheni ndogo sana. Alijisahau na kudhania angedumu kwenye ile post indefinitely.
Kulikuwa na wkt iliundwa wizara yenye jina "Wazee", lkn hakukufanyika lolote lililowapa faida wazee. Kila ukiuliza, wanakuambia "matibabu bure", wakatengnezewa vitamblisho lkn hapakuwa na dawa, hakuna zaidi. Baadae jina hilo likaondolewa, lilionekana kuwasuta viongozi.
Lilionekana kama linaongeza gharama - yaani mzee ni gharama!

Walijua kuwa nao watazeeka, wakatengneza mfumo utakaowahakikishia maisha bora uzeeni kupitia mishahara minono, hivyo hawawajali wazee.
Pia serikali imekopa sana kwny mashirika ya pensheni na wameshindwa kulipa ambapo pia mashirika haya yamewekeza sana kwny maujenzi yasiyo na tija hivyo kuwaongezea mzigo wa kupandsha pensheni inaonekana ni kuwatesa.
Mwanasiasa kajihakikishia pensheni nzr wkt wa kima ch chni ch mshahara anaiona dunia chungu.
Mifumuko ya bei haichagui mzee wala kijana na sera na maamuzi pia hayatakiwi kubagua.
Serikali iwapandishie wastaafu pensheni zao kama wanavojipandishia mishahara wao
 
Mtaanza na kudia mafao ya marehemu wa zamani yaongezwe Sasa ebu kubalini uhalisia kuwa mlistaafuu na pesa mliyopewa mda ule ilistahili na ilifaa tatizo wastaafu wa zamani wakiamini kurudi kijijini kwao ndio mpango mzima wakastaafu wakarudi maeneo ambayo hawakuwepo zaidi ya miaka therathini wengine wakakimbia na familia wakaenda kwa vibinti vya mjini
Umeandika ujinga mtupu.
 
Umri wa kustaafu pia uangaliwe upya, Miaka 50 iwe ni kustaafu kwa hiari 55 iwe ni umri wa lazima ili vijana nao wapate ajira.
Kama nchi gani inayofanya hivyo au sis ndio tuwe wa kwanza duniani
 
Sasa mstaafu alipwe kwa uhalisia wa maisha ya Sasa anazalisha nini mjumbe, kipato alicholipwa kilimfaa mda ule kuandaa maisha yake ya sasa,

Cha msingi hapa nikukumbusha watu wlaiopo makazini kuandaa maisha yao ya kustaafu waakiwa bado wapo kwenye ajira hii itapunguza mambo kama haya
Nadharia unaonekana upo sahihi.
Waulize walio ulingoni ndipoutaelewa kuwa kustaafu ni mziki mneme.
Unawaona hao wastaafu hawakujindaa.
Vijana wengi wanaona wao wana akili nyingi.
Ukifanya utafiti utafuta kauli yako.
Utaomba radhi.
 
Kuna mstaafu alipewa milioni 70 zote zikaishia kwenye bia ndani ya miezi mitatu. Wastaafu ni kweli muongezewe pensheni ila na nyie muwe na nidhamu ya pesa.
Hukumu yako imejikita kwa hiyo mmoja Kati ya mamilioni ya wastaafu.
Kwa maana hiyo serikali isiongeze mshahara kwa kuwa baadhi ya watumishi [huenda kama wewe] wanafuja mshahara?

Nashauri ni vema serikali iwaandae vema wastaafu tarajali.
 
Back
Top Bottom