Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Baada ya Tume ya Uchaguzi kuthibitisha kwamba haikuwa sahihi kuwaengua Wagombea wa Upinzani kama ilivyofanywa na Wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wanachama wa CCM, kuna haja ya kuwaondoa kabisa wakurugenzi hao kwenye usimamizi wa uchaguzi huu ili kuepusha maafa.
Hawaaminiki tena na wala hata wao wenyewe hawajiamini, kwa mfano Mkurugenzi wa Ubungo Beatrice Dominic, pichani
Hapaswi kuwa msimamizi wa uchaguzi wa eneo hilo kwa vile anazo chuki binafsi na Mstahiki Meya wa Zamani wa Manispaa hiyo ambaye pia ni mgombea ubunge wa CHADEMA wa Jimbo la Ubungo, mama huyu akiachwa ataleta machafuko ambayo hayatakuja kukoma, aondolewe mapema msije kusema hatukuwaambia, sambamba na huyu wakurugenzi wengine wote walioboronga waondolewe, hawaaminiki tena.
Hawaaminiki tena na wala hata wao wenyewe hawajiamini, kwa mfano Mkurugenzi wa Ubungo Beatrice Dominic, pichani